Mbowe anasema mkataba ni zaidi ya miaka 100, hauna ukomo. Ni life time

Mbowe anasema mkataba ni zaidi ya miaka 100, hauna ukomo. Ni life time

Rais na watendaji wake wanatakiwa kuhukumiwa vifungo virefu gerezani kwa hii dhambi waliyolitendea taifa letu, dhambi itakayoviumiza mpaka vizazi vijavyo, hawana huruma kwetu hawa viumbe, walaaniwe!.
Swali muhimu la kuuliza hapa ni kwa nini watu, tena viongozi wa nchi, wenye akili timamu wanaweza kufanya jambo kama hili. Kwa nini?
 
Tigo Postpaid Bando za bei nafuu sana kwa Tsh 15 unapata Gb 15 mwezi mzima , karibu pm kwa maelezo zaidi. Na kujiunga
We naye Kuna jukwaa la matangazo sio humu kwenye agenda muhimu unaingiza mambo yako, poor strategy
 
umeongea kipuuzi sana bila ku-reason,ni lini ushaona kiongozi bora akawa mzizi wa matatizo ya africa???

africa inahitaji mfumo bora wa kiutawala na sio kiongozi bora.......kiongozi awe kama pambo tu ila wanaotawala nchi wawe watu makini,wenye maono na uzalendo wa hali ya juu na ambao wanaweza wakamfundisha rais jinsi ya kufanya kazi na sio rais awafundishe wao jinsi ya kufanya kazi

Hii hufanywa na almost nchi zote zilizo endelea duniani...............

BE OPEN MINDED
Tatizo lenu mna matamanio ya matokeo na siyo mchakato wa kupata hayo matokeo.

Mnatamani nchi za africa zifuate mifumo ya nchi za america na ulaya za kisiasa bila kujiuliza hawa jamaa ilikuwaje wakafikia hapo.

Nchi za africa zina mifumo Mizuri ya uongozi na nchi zingine zina mifumo sawa na nchi za wa wazungu, ila ni kwa nini shida bado zipo pale pale?

Unajua weakness ya kuwa na mfumo imara bira ya kuwa na kiongozi imara?

Human intervations ndo great weakness ya mifumo. Kwa mwafrika bado hatujawa stable kuwa na uwezo wa kuongozwa kwa mifumo. Mifumo ni project za wazungu ili kuweka urahisi wa kupenyeza sera zao na kuiba raslimali.

Mifumo ipo tiyari na inatumika ndo maana nchi za africa zinajiendesha, ila kinachokosekana ni msimamizi wa mfumo .

Mnajipigisha makelele ili mpate uongozi mlambe asali. tumewashtukia.
 
Punguza uongo, usihamishe magoli. Magufuli mwenyewe aliwachukia CHADEMA Sana.
Mtu mwenye akili timamu atakubalije wendawazimu wenu?

1. Unawajengea barabara ila bado wanakuona hufanyi kazi,
2. unawanulia ndege mpya na wanazipanda ila bado wanakusema.
3. Unawatengenezea bwawa la umeme na wanautumia ila bado wanaongea ujinga.
4. Unawafanyia mazuri mengine mengi lakini wao bado wanaendeleza midomo mibovu.

Kiukweli Magu alikuwa anahuruma sana kwenu, ningekuwa mimi ningekamata mmoja baada ya mwingine mpaka niwamalize na siyo viongozi tuu hadi nyie rais.
 
Ndio maana nilikuwa namsubiri kwa hamu sana huyu mtu azungumze, kwasababu nilijua tu, linapokuja suala la maslahi ya taifa hajui kumun'gunya maneno.

Nashangaa kuna vipofu walikuwa wanaulizia kwenye ule mkataba miaka 100 iko wapi, wao wakadai hawaioni, wakashindwa kutazama vipengele vingine kwenye ule mkataba, kisha wajumlishe na zao kichwani ili wapate jibu.

Kwa akili ya kawaida tu, kama mkataba hauna kipengele cha duration, at the same time panakuwepo na kipengele cha confidentiality, hapo anayejielewa hatakiwi kuuliza namba 100 iko wapi? common sense kwa baadhi yetu is not common!.

Rais na watendaji wake wanatakiwa kuhukumiwa vifungo virefu gerezani kwa hii dhambi waliyolitendea taifa letu, dhambi itakayoviumiza mpaka vizazi vijavyo, hawana huruma kwetu hawa viumbe, walaaniwe!.
Unapolalamika na kuongea ongea kila siku, unakuwa kama mbwa. No time for talking again
 
Mkataba huo ni wazi kuwa unakuja kuwapa umaarufu wapinzani na kuidunisha CCM, kwahilo CCM wote lazima wahusishwe na hili swala.
Kwanza movement zote za wabunge wetu kwenda dubai zilianza kutia mashaka. Haya tuje tuangalie mnara uliowashwa dubai. Aise ninaomba niseme kuwa Tanzania tunahitaji mbuzi wa kafara kuikomboa.
 
Tatizo akikumbuka asali atadai viongozi wa dini wamemshauri wakae meza moja Ili Sasa apewe kibuyu kabisaa.
 
Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai umeacha maswali mengi na kuamsha hisia za kudai Katiba mpya kwa nguvu zote.

Ni mkataba ambao ulisainiwa kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari juu ya madhara yake yaliyo dhahiri. Mkataba huu haukubaliki kwa sababu nyingi Sana.

Moja , ni mkataba wa milele kwa sababu hauna ukomo. Najua wapo waliosema ni wa miaka 100 na wapo waliosema ni wa miezi 12.

Hawa wote sijui wametoa wapi huo muda wa mkataba. Ibara ya 23 ya mkataba na randama zake (appendixes) zake hakuna popote zinaonyesha mkataba huu ni wa muda gani. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kudumu.

Ni kweli unaweza kuwa miaka mia lakini pia hakuna Cha kuzuia uwe wa miaka 1000.

Pili, mkataba huu unanguvu kuliko Sheria za Tanzania pamoja na Sheria za kimataifa (Takes precedent over national and international law)

Mathalani Ibara 23( 4) hairuhusu kuvunja mkataba huu hata pakiwa na ukiukwaji mkubwa (material breach) au kukitokea hali inayopelekea mkataba usitekelezeke (fundamental change of circumstances) ambalo ni Takwa la mkataba wa kimataifa uitwao Vienna Convention on the Law of Treaties,1969 ambao Tanzania imejifunga nao.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba baada ya kusaini mkataba huu hata Dubai wakikiuka kabisa hatuwezi kujitoa. Hicho ni kitu Cha ajabu mno dunia itatushangaa.


Mbaya zaidi mkataba hausemi je una nafuu ili mbadala ukiachilia mbali kuvunja mkataba.

Kifungu Cha 23( 4) kinaenda mbali zaidi na kusema ikitokea sababu yeyote inayotambulika kwenye Sheria za kimataifa ya kupelekea kuvunja mkataba bado mkataba huu hautavunjwa.Tafsiri yake ni kwamba tumeingia kwenye shimo ambalo halina pa kutokea( coup de sac) .

Tatu, mawanda (scope) ya mkataba pia ni mapana, ni Kama hayana ukomo. Ibara ya 2(1) itaruhusu muwekezaji kujenga na kuendesha miradi ya bandari za Bahari na maziwa yote.

Mkataba unakwenda mbali zaidi hata kwenye kile kinachoitwa (logistic parks na trade corridors) ambazo bahati mbaya hazijatafisiriwa kwenye mkataba.

Kwa namna mkataba huu ulivyo sisi tutakuwa tumepoteza udhibiti wa bandari zote za bahari na maziwa yote.

Mkataba ungeweka wazi ni bandari zipi hasa kwa sababu kwa namna ya Sasa hata usalama wa nchi unaweza kuwekwa rehani.

Nne, mkataba hausemi sisi tutapata nini( consideration) kwa maana ya faida za mradi. Je sisi tutakusanya Kodi tu? Au tutakuwa wabia?

Tano , mkataba hauonyeshi nafasi ya mamlaka ya bandari( TPA) ni ipi katika uendeshaji wa mkataba. Kumbuka kwa mujibu wa sheria TPA ndo chombo chenye mamlaka ya kuendesha bandari zote. Sasa je mkataba huu umefuta sheria hiyo? Kwa mamlaka gani?

Mkataba hauelezei kuhusu usalama wa mapato yetu bandarini na nafasi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwaajiri ya usalama wa nchi yetu hasa kwenye marine.

Nafasi pekee ya TPA kwa mujibu ya randama ya kwanza imeachiwa kuendesha na kusimamia " DHOW AND WHARF TERMINAL" ya bandari ya Dar es Salaam.


Sita, pamoja na kuweka kipengele Cha local content ili kunufaisha wazawa kwenye ajira na manunuzi kwenye ibara 13( 2) ibara hiyo haina maana yoyote Kwanza kwa sababu haiweki wazi kwamba threshold ya wazawa kwenye ajira itakuwaje.

Pili hata procurement( manunuzi) ya vitu au items au huduma zinazopatikana ndani hailindwi na mkataba kwa sababu kwa mujibu wa ibara ya 6(2) ya mkataba huu serikali yetu hauruhusiwi kufanya usumbufu wowote (interference) yoyote hata kwenye manunuzi yanayokiuka Sheria isipokuwa tu Kama yanahatarisha usalama( safety and security).

Sasa je wakiamua kuagiza mbao Dubai wakati hapa nchini zipo utawazuia kwa kigezo Cha usalama?

Saba, mkataba hausemi nani atawajibika kulipa fidia yoyote inayotokana na utekelezaji wa mradi pamoja na watumishi ambao ajira zao zinaweza athiriwa na mradi.

Nane , pamoja na kwamba ibara ya 26 ya mkataba inaelekea kuruhusu reservation utagundua kwa namna ibara ya 24 ilivyo imepoka kwa mkono mwingine haki ya reservation iliyopo kwenye ibara ya 26 hivyo sioni uwezekano wa nchi yetu kufanya reservation kwenye makubaliano bila kukwaza mkataba.

Kwa namna ya mkataba huu tukifanya reservation Sasa ivi inaweza kupelekea nchi iingie kwenye mgogoro wa kukiuka mkataba.

Tisa, hata kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge tayari umefanyika nje ya muda.

Ibara ya 25(2) ilitaka mkataba uridhiwe ndani ya siku 30 tu na leo ni zaidi ya miezi Saba.

Kumi, kwa mujibu wa ibara ya 8(3) (c ) mkataba huu ni kama unatoa umiliki wa ardhi kwa mwekezaji kinyume na Sheria ya ardhi.

Kwa mujibu wa sheria ya Ardhu Sura ya 113 Kampuni ya kigeni hairuhusiwi kumiliki ardhi Tanzania.

Tulitegemea mkataba useme ardhi zitakuwa chini ya TPA au mamlaka nyingine za serikali na wao watapata derivative rights badala ya kuwapa ardhi kwa mgongo wa lease hold.
 
Ndio maana nilikuwa namsubiri kwa hamu sana huyu mtu azungumze, kwasababu nilijua tu, linapokuja suala la maslahi ya taifa hajui kumun'gunya maneno.

Nashangaa kuna vipofu walikuwa wanaulizia kwenye ule mkataba miaka 100 iko wapi, wao wakadai hawaioni, wakashindwa kutazama vipengele vingine kwenye ule mkataba, kisha wajumlishe na zao kichwani ili wapate jibu.

Kwa akili ya kawaida tu, kama mkataba hauna kipengele cha duration, at the same time panakuwepo na kipengele cha confidentiality, hapo anayejielewa hatakiwi kuuliza namba 100 iko wapi? common sense kwa baadhi yetu is not common!.

Rais na watendaji wake wanatakiwa kuhukumiwa vifungo virefu gerezani kwa hii dhambi waliyolitendea taifa letu, dhambi itakayoviumiza mpaka vizazi vijavyo, hawana huruma kwetu hawa viumbe, walaaniwe!.
Hatari hatari
 
Atakuja Wilson Mahela na UVCCM na kuanza kusema wananchi hawahitaji bandari, wananchi wanahitaji maji, wananchi wanahitaji barabara, wananchi wanahitaji huduma za afya, wananchi wanahitaji SGR[emoji2]
Na kuna mtu ana PHD hukohuko
 
Back
Top Bottom