Ndio maana nilikuwa namsubiri kwa hamu sana huyu mtu azungumze, kwasababu nilijua tu, linapokuja suala la maslahi ya taifa hajui kumun'gunya maneno.
Nashangaa kuna vipofu walikuwa wanaulizia kwenye ule mkataba miaka 100 iko wapi, wao wakadai hawaioni, wakashindwa kutazama vipengele vingine kwenye ule mkataba, kisha wajumlishe na zao kichwani ili wapate jibu.
Kwa akili ya kawaida tu, kama mkataba hauna kipengele cha duration, at the same time panakuwepo na kipengele cha confidentiality, hapo anayejielewa hatakiwi kuuliza namba 100 iko wapi? common sense kwa baadhi yetu is not common!.
Rais na watendaji wake wanatakiwa kuhukumiwa vifungo virefu gerezani kwa hii dhambi waliyolitendea taifa letu, dhambi itakayoviumiza mpaka vizazi vijavyo, hawana huruma kwetu hawa viumbe, walaaniwe!.