Mbowe ashikiwa bango kutafuna milioni 800 za ujenzi wa ghorofa la Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA

Mbowe ashikiwa bango kutafuna milioni 800 za ujenzi wa ghorofa la Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA

Tulishakuwa na mpango kama wa CCM kuwa na chuo kama hicho na tuliahidi kukiita chuo cha uongozi cha Edwin Mtei.

Sasa kama ofisi ya Makao makuu imetushinda, ndio tutaweza chuo?
Isikurupuke kwa jambo usilolijua, chuo hicho kimejengwa kwa msaada wa serikali ya China. Serikali ya Marekani ikitoa msaada wa kuwajengea choo Chadema huenda chama kikafutwa kwa kuhusisha wageni kufanya siasa nchini!
 
Tuna marafiki zetu huko Ujerumani na Denmark. Hujui hilo?
 
Tulishakuwa na mpango kama wa CCM kuwa na chuo kama hicho na tuliahidi kukiita chuo cha uongozi cha Edwin Mtei.

Sasa kama ofisi ya Makao makuu imetushinda, ndio tutaweza chuo?
Nadhani unasahau kwamba kwa sasa CCM inapata zaidi ya sh bil moja kwa hela za walipa kodi Kama ruzuku. Pia CCM inamiliki majengo viwanja vya michezo viwanja vya ardhi na mali zingine ambazo kimsingi no mali za watanzania ambazo zimebinafsishwa na CCM na kuzifanya ni mali zao. Pamoja na hayo kuna uwezekano mkubwa sana kiasi kikubwa cha gharama za ujenzi huo zikatolewa na serikali. Kumbuka hayati Mkapa alijisifu kwenye kitabu chake kuwa alitumia hela ya serikali kulipia gharama za uchaguzi za CCM mwaka 2005. Hawatashindwa kufanya hivyo tena sasa ukizigatia kuwa kwa sasa bunge no lao peke yao hakuna wa kuwauliza.
 
Chama kisichotaka mabadiliko ya katiba kuwa na majengo mapya haikisaidii.
Huu uzi ufungwe sasa. Chama kinachoshabikia kujenga chama badala ya kujenga nchi hicho sio chma.
Chama kinachofikiria kushinda uchaguzi tu kila siku badala ya kuwaletea wananchi maendeleo, hicho sio chama cha siasa, ni kikundi cha kimafia chenye lengo la kuhakikisha wao,watoto wao, wajukuu wao, vitukuu vyao na watu wao wa karibu wanaendelea kuila keki ya taifa peke yao miaka nenda miaka rudi bila ya usumbufu.
Pale Uzunguni - Dodoma,tulioishi na kukulia pale miaka ile ya 1975 mpaka 1995, tunaelewa ni kwa nini viongozi wa CCM hawapo tayari kuona CCM inatolewa madarakani kwa kura au kwa njia yoyote ile.
Watoto wengi wa waliokuwa viongozi wa CCM ndio viongozi wa sasa chamini,serikalini, mashirikani na idarani.
Ukifuatilia kama wameingia huko kwa "merits", utakuta kwa zaidi ya asilimia 75 hawana sifa za kuwa hapo walipo,ila ni mfumo wao wa kurithishana wa CCM ndio unatumika.
Uwenzetu/mwenzetu.
Mfumo huo wa CCM umesababisha chama kama chama kukosa kabisa rasilimali watu wenye uwezo na weledi kwa ajili ya kutumika kuleta maendeleo zaidi ya kusifu, kuabudu na kujipendekeza ili waonekane na kuteuliwa.
Kijana mwenye ufahamu wa kutosha, mhojaji na asiyependwa kuburuzwa katu huwezi mkuta anashabikia CCM. Mifano ipo na ndio maana mwendazake na wenzake wakaanzisha kampeni ya manunuzi ya binadamu "wenye ufahamu wao" toka vyama vya upinzani na kuwapa nafasi za uongozi.
CCM wanaendesha siasa za kiukoo.
 
Tulishakuwa na mpango kama wa CCM kuwa na chuo kama hicho na tuliahidi kukiita chuo cha uongozi cha Edwin Mtei.

Sasa kama ofisi ya Makao makuu imetushinda, ndio tutaweza chuo?
Kwanza chuo hicho siyo cha CCM. Ni chuo cha vyama vya Ukombozi Kusini mwa Africa .... Wamejengewa bure na Wachina.

Pili kuwa na vyuo kama hivyo ni kuwa ajili ya kuindoctrinate wafuasi na kuwalisha itikadi. Hayo ni mambo ya communism na utayakuta China, Cuba na North Korea. Hicho chuo ni kama kilivyokuwa chuo cha kivukoni. Ni kwa ajili ya kutengeneza wapiga propaganda wa chama. Hii siyo dalili njema kwa nchi ..... Wataturudisha enzi zile.
 
Kuna KM mmoja wa zamani wa CCM aliwahi ulizwa swali na mwandishi wa habari wa gazeti la MotoMoto kuwa kama CCM wana risiti za manunuzi za viwanja vyao vyote vilivyopo karibu kila kata mijini,alijibu kuwa hawakununua bali walipewa na serikali.
Ukweli kwa sisi tuliokuwepo miaka ile ya 1970,majengo na viwanja vingi vya CCM walivyojimilikisha baada ya mfumo wa vyama vingi kurudi tena,vilichangwa na Watanzania wote bila kujali itikadi, ila CCM kwa umafia wake baada ya mfumo wa vyama vingi kurudi tena, ikajimilikisha vyote wakati kiuhalisia havikuchangiwa na wanaCCM pekee.
 
Kwanza chuo hicho siyo cha CCM. Ni chuo cha vyama vya Ukombozi Kusini mwa Africa .... Wamejengewa bure na Wachina.

Pili kuwa na vyuo kama hivyo ni kuwa ajili ya kuindoctrinate wafuasi na kuwalisha itikadi. Hayo ni mambo ya communism na utayakuta China, Cuba na North Korea. Hicho chuo ni kama kilivyokuwa chuo cha kivukoni. Ni kwa ajili ya kutengeneza wapiga propaganda wa chama. Hii siyo dalili njema kwa nchi ..... Wataturudisha enzi zile.
Ndugu The Khoisan , yaani inashangaza sana jinsi uongozi wa CCM na serikali kwa ujumla wasivyoona jinsi Uchina inavyohangaika na kutulisha ukomunisti ili tuukubali na kuufuata. Napata shida sana kuwaelewa hawa watu kuwa wanawaza Wachina wanawapenda sana sana!!!!
Tunajisifia kwa chuo hicho kujengwa Tanzania bila kufikiria nnje ya boksi kuwa wamejenga kwetu kwa kuwa sisi tunaonekana ni tupo usingizini bado, tuna rasilimali nyingi sana ambazo Uchina anazitolea macho na ushawishi tulionao kwa hizo nchi tulizosaidia kuzikomboa.
 
Back
Top Bottom