Mbowe: CHADEMA hatutashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 (bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi)

Hebu sasa wapiganie hiyo Katiba Mpya kwa nguvu zote tuone mwisho wake utakuwa nini, na asijedanganywa na juice za ikulu alegeze msimamo, huo msimamo uwepo mpaka mwisho.
 
Haya ndo mambo
 
Tunaunga mkono hoja
 
Hata msiposhiriki poa tu maana hamna la maana, wahuni tu nyie
 
Kuna rasmu ya katiba iliyokuwa tayari kupigiwa kura na wananchi lakini Chadema wakiwa katika umoja wa UKAWA waliipinga rasmu ile.

Kama Rais Samia aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba ataamua kuwasikiliza kitu pekee ataweza kufanya ni kukamilisha mchakato wa katiba mahali ulipoishia.

Sijui Chadema wanataka katiba ipi Rasmu iliyokuwa tayari kupigiwa kura au mchakato wa katiba urudiwe upya?
 
Rais ukiiruhusu mashinikizo nchi haitatawalika hii,maana kinachofuata ni maandamano ya kudai katiba.
Baada ya hapo utashangaa wafanya kazi wataandamana kudai nyongeza ya mishahara.Machinga wataandamana kupinga kufukuzwa maeneo waliyo zoezu kuuzia bishara zao.
Dhibiti mapema.
 
Kama rais akiwa kubalia tunataka ile Raimu iliyopendekeza ukomo wa Wabunge kugombea.
 
Angekuwa hapendwi mgekuwa mnamuongelea hadi leo? Imagine mtu ana miezi 3 kaburini lakini kila siku ni kumjadili yeye tu.

Mzee aliwashika pabaya wafanyabiashara kanjanja msiolipa Kodi, wauza ngada, misheni town, vyeti feki, wahujumu uchumi, Wala rushwa na mafisadi. Kwa hasira mlizo nazo sishangai mtaendelea kumuongelea kwa miaka mingi ijayo.
 

mara kibao tu tunawaambia lissu yupo mwenyewe kwenye icho chama hamuelewi tu, chadema ni mali ya ccm
 
Upuuzi mtupu watanzania wanataka kusikia SGR ,Bwawa la umeme vimekamilika
 
Wanataka mchakato wa katiba uanze upya
 
Hiyo ndiyo sababu kuu ccm huwa wana muogopa sana mh Mbowe.
 
Huyu jamaa anaua upinzani, yaani jana tu katoka kusema anamuunga mkono mama then leo tena hawatashiriki uchaguzi. Chadema mwangalieni huyu mwenyekiti.
Tatizo lako hujui hata kiswahili masikini ya Mungu.

Kuna tofauti ya kumuunga mkono mama Samia na kukubali kushiriki uchaguzi bila ya kutimizwa kwa masharti husika.
 
Huyu jamaa anaua upinzani, yaani jana tu katoka kusema anamuunga mkono mama then leo tena hawatashiriki uchaguzi. Chadema mwangalieni huyu mwenyekiti.
Kwa taarifa yako ni kwamba hapo hakuna chama cha upinzani kinacho uawa maana chama cha upinzani hapa Tanzania ni C H A D E M A.
 
Mkuu@Saint Ivuga: huoni huo uamuzi wa mh Mbowe kuwa ni mwanzo wa kuanzisha vuguvugu la kudai hiyo katiba?

Unadhani au kufikiria chama kama ACT na CUF na TLP na wengine wanaweza kuamua uamuzi mgumu na wa kuumiza kama huo?
 
Kiswahili nahisi kinakupiga chenga wewe kumuunga mkono na na kutoshiriki uchaguzi ni vitu viwili tofauti.
Tangu lini Wanyarwanda wakajua kiswahili?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…