Mbowe: CHADEMA hatutashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 (bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi)

Ubaya ni kwamba chama cha upinzani si kimoja kwa sasa. Vyama vingine vikishiriki show inapigwa tena kali mno na kijani inabaki madarakani.
Yes Zito Kabwe atashiriki na chama chake kitashinda na kuwa chama kikuu cha upinzani nchini
 
Mbna iblis na farao wanazungumziwa kila kukicha????
 
Hivi nyie binadam wenzangu mpoje mnajuaje Kama mama Samia at survive mpaka 25
sio tu ku survive!,wanajuaje 2025yr,atagombea SSH!? wanahangaika tu nao hawa.muda hutoa majibu yote!tuliwaambia mbowe sio kabisa,ni dalali.wakawa wanang'aka humu.
 
Swala la katiba mpya linakuwa shida kwa sababu ccm wanafahamu fika kwa asilimia mia moja kwamba hii katiba yao ndio mungu wao na kwamba siku isipokuwepo na wao hawatakuwepo.

Lakini siku wazungu wakitaka Tanzania ipate katiba mpya, tutaipata ndani ya masaa 24 tu. Walipotaka mabadiliko ya urais yafanyike yamefanyika mara moja na rais aliyeko kama hawezi kuelewa somo basi zoezi linaweza kurudiwa.
 
Oya tujenge uchumi wadau

Ujenz unaanzia chin tudai marekebisho ya sheria ndogondogo znazotunyonya kila siku zkishughulikiwa tuendlee na nyingne.
 
Oya tujenge uchumi wadau

Ujenz unaanzia chin tudai marekebisho ya sheria ndogondogo znazotunyonya kila siku zkishughulikiwa tuendlee na nyingne.
Sheria zipi hizo
 
Shida nayoiona Chadema wanataka katiba mpya ya Taifa lakini Katiba ya Chadema inampa mwanya mtu moja tu kuwa Mkiti miaka yote kwanini?
 
Mbowe huwa ana hekima iliyo kubwa kuzidi umri wake. Ninaona mkakati wake hapa anaiangalia 2030 kwa sababu anajua kwa sasa hivi hayuko sawa sana kwa ajili ya 2025. Kwa hiyo anaamua kuiachia 2025 but at a price ambayo inaweza kuja kumlipa 2030 kama atafanikiwa kujiweka sawa kati ya 2025 na 2030. Ni option moja ya busara sana na iliyotumia hekima ya hali ya juu sana. Wapinzani wake inabidi waiangalie option hii kwa jicho la hekima sana

Kuna siku mwaka jana aliwahi kusema "tarehe 01/04/2020 tunaanza mikutano ya kisiasa nchi nzima" lakini wakati huo huo karibia dunia nzima ilikuwa inaingia kwenye lockdown. Mbowe huwa wakati mwingine anatumiwa kutabiri matukio yajayo. Ni mtu mwenye hekima tu anayeweza kutumiwa na Mungu kwa namna hiii
 
Huwa mnajipa moyo sana
 
Huwa mnajipa moyo sana
Akina nani, sisi wapinzani?
Tunaweza pia tusiwe ni wapinzani, ila watu ambao tunazijua fair grounds za kisiasa kiasi kwamba huwa tunatoa ushauri kwa kuangalia mazingira halisi namna yalivyo pasipo kuwa na ushabiki wowote ule wa kisiasa
 
Aisee. Wafuasi wa Mbowe mna matatizo ya akili.
 
Mheshimiwa Mwenyekit Mh Mbowe anasemaje kuhusu uchaguzi wa kipima joto wa serikali za mitaa utakofanyika 2024?
 
Uchaguzi wa kidemokrasia bila Tume huru? Wachekesha sana wewe. Si itawasaidia muweze kupata nafasi ya kuokoteza wa kuunda Covid # wengine.
Tume iko Huru, nenda kasome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Ibara ya 74 (11) utaelewa ndugu yangu usipotoshe watu.
 
Shida nayoiona Chadema wanataka katiba mpya ya Taifa lakini Katiba ya Chadema inampa mwanya mtu moja tu kuwa Mkiti miaka yote kwanini?
Kwa nini hiyo ikupe shida wewe, kwani ni mwanachama wao? Kama ni mwanachama, basi lifikishe chamani litatuliwe.

CHADEMA kuhimiza katiba mpya ya nchi haizuiwi kwa wao kutokuwa na katiba mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…