Kama atatenda kosa sawa ila kama hakutenda kosa lolote watampeleka kwa uonevu ?Unafikiri ndiyo amemaliza zamu yake na hawezi enda tena huko akitaka tena. Hizi ni dalili za kutaka kwenda huko. Nyie mcheeni tu Mama.
Unajadiliana vipi na watu ambao hawako tayari kujadiliana.?Tatizo la Chadema siyo wanasiasa ni wanaharakati,hawajui kwamba kwenye siasa Kuna hitaji mchakato,majadiliano ya muda mrefu mpaka mnakubaliana na kwenye muafaka siyo lazima upate yote Kuna kupata na mengine kukosa.Wakiendelea na siasa za aina hii watakosa yote hawatapata katiba mpya Wala tume huru ya uchaguzi.
Ikiandikwa katiba mpya nzuri ya kidemokrasia CCM itadhoofika.Nguvu kubwa ya CCM ni kuchangamana na dola na katiba hii iliundwa mahsusi kuipendelea CCM.Kwahiyo hata Chadema kingekuwa chama tawala isingekubali katiba mpya.Hivi ccm wanachoogopea katiba mpya ni nini?
Mbowe ni kiongozi mkubwa sana ila anafeli sehemu ndogo sana mara kwa mara
Kiongozi mkuu hatakiwi kutoa kauli kwa kukurupuka
Kwa mfano, anavyosema "...viongozi wa chadema wajiandae kufanya mikutano ya hadhara..." tafsiri yake ni nini?
Viongozi wake ni wakupokea order tu na kutekeleza bila kuwa na majadiliano?
Ikitokea viongozi kadhaa wakaja na hoja yenye mashiko (mfano kuepuka mikusanyiko kwa sababu ya corona) na hivyo kufifisha "agizo" lake haoni Kama inampunguzia credit yeye Kama top leader?
Halafu Mbowe alitakiwa asome upepo, kuja na matamko Kama haya watu wenye kudadisi sana watakuja na conclusion kuwa kumbe na yeye ni muoga Kama waoga wengine maana enzi za Magufuri hakutoa hivi vitisho, kwanini alishindwa wakati katiba inawaruhusu?
Hata hivyo, asome upepo vizuri wa wananchi maana ni "Kama" wanamuelewa elewa Rais huyu hivyo wanaweza kujikuta wanaandamana viongozi wao tu na boda hoda mtaani
Teh ngoja tuoneHatutakubali hatutakubali, mara Never Never !
Utafikiri tunao huo uwezo wa kufanya chochote kitu[emoji1787]
Mungu hahangaiki ni bangi kama hiziKama atatenda kosa sawa ila kama hakutenda kosa lolote watampeleka kwa uonevu ?
Mungu atatenda kazi yake
Hawa jamaa wameshaanza sarakasi zao Mama itakubidi ukorome kidogo la sivyo watakutawala.
Rais kakataa lini?Rais alisema ataonana na wapinzani,nafikiri Jambo la muhimu ni kumsisitizia/kumkumbusha aonane nao halafu mazungumzo yaanze.Unajadiliana vipi na watu ambao hawako tayari kujadiliana.?
Jamaa zangu wa CDM mnaona jamaa yenu alivyo mwehu???
Jinga kabisa, kamuandalie chai ya jioni Nikki, ulisema igizo limekwama hakuna wajumbe sasa hivi unasema wajumbe walevi, utakuwa baamedi wewe ukitoroka kuosha vyombo kwa Nikki unakimbilia bar.Katiba inadaiwa na walevi? Mkutano umejaa walevi watupu kuanza mwenyekiti hadi wajumbe.
Wazee wa faru John, sipati picha baadae mtavyolewa
mama siyo dikteta kama jpmYaani Mbowe anamtisha Rais wa nchi? Huyu mama awe makini, kipindi cha JPM hizi kauli kama za Mbowe hakuna aliethubutu kuongea, na Ikitokea umeongea lazima uchakae
Hizo mbwembwe hazijaanza jana.Teh ngoja tuone
Mkuu wewe ni miongoni mwa members ambao kwa kweli wakini-quote huwa nawaheshimu sana. Heshima yangu kwako ipo juu sana mkuu...Raisi amehimiza lugha za staha.
..Sasa ndugu zangu kama mmeamua kumuunga mkono Raisi msiwe mnatumia lugha mbaya dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani.
..Mnapomuunga Rais mkono kwa upande mmoja, halafu upande mwingine mkawa mnawatukana wapinzani, jamii inaweza ikadhani mmetumwa na Raisi kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa kudumu wa CHADEMA amemuonya Rais Samia kuwa asikubali kuliruhusu bunge lililopo sasa hivi lianze mchakato wa katiba mpya.
Mbowe amesema Rais akiruhusu hilo wao kama chama cha upinzani nchini hawatakubali kamwe.
"Kwanza tuna amani mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni haki ya kikatiba kisheria na ni wajibu wetu, ombi la mama Samia kwamba tusubiri, tumpe muda hatuko tayari kumpa muda."Freeman Mbowe
====
wenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan, aunde Tume ya Katiba, itakayoshirikisha makundi yote kwa ajili ya kufufua mchakato wa katiba mpya “na hatutakubali Bunge hili lililopo, litutengenezee katiba mpya.”
Ombi la Mama Samia kwamba tumpe muda hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza.
Tunapendekeza kuwe na Bunge la Katiba na lisiwe Bunge hili linaloendelea sasa wala wasituambie Bunge hili la sasa ndio liunde Katiba, ichukuliwe rasimu ya Warioba na Katiba na kisha iundwe rasimu ya Katiba mpya, sio gharama na tukiamua tutapata Katiba mpya mwaka huu.
Katiba ni mali ya Wananchi na sio mali ya Viongozi, miongoni mwa mambo ambayo Rasimu ya Katiba ya Warioba ilibainisha ni kupunguza majukumu ya Rais,Warioba alipendekeza tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Tuwe na Mgombea Huru.