Mbowe: Hatutompa muda Rais na hatukubali. Viongozi wa CHADEMA watakiwa kujiandaa kuanza mikutano nchi nzima

Ndio maana mlikuwa mnapewa makesi kesi mkiachwa free, akili zenu zinakuwa hazijazoea shuruba. Ingieni barabarani mnyooshwe. FFU wana miaka 6 hawajatia virungu chadema
 
Hahahahahah na hapo ndipo hasira ya Jiwe dhidi ya hawa wapuuzi ilichipukia! Wanakera sana kmmmke they dont let a nigga breathe thus why walifanywa hakuna na hata ubunge wakanyang’anywa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Wajinga sana kawa, hivi kwa kauli kama hizo ni nani mwenye mamlaka anaweza kuvumilia? Tena bora hiyo kauli itoke kea kwa hawa makapuku wa jF kidogo mtu anaweza kupotezea,eti inatoka kwa kiongozi kabisa? Hata mimi wangeniita dikteta tu, mtu kama huyu ni lazima ningeingia nae kwenye mapambano.
 
Hii inaitwa Shusha nanga pandisha Nanga.
 
Mkuu, hivi Magufuli angekuwepo, unajuwa kwamba CHADEMA wasingedai hayo wanayodai kwa vile alikuwa mbabe, una uhakika huo?

Unaamini Samia akiwa '"mbabe" katiba mpya watu wataacha kuidai? Unao uhakika huo?
Watu tunaamini hivyo kwakua hizi kelele zenu hazikuwepo kabla ya Magufuli kufariki,hivyo basi mnamdharau sana Samia.

Kimsingi hiyo kauli ya Mbowe inaamsha hisia za SSH,kutaka kuwaonyesha makucha yake na mwisho wa siku tutarudi kulekule.
 
Hovyo. Watu kufanya mikutano ya kisiasa kuna uharamu gani. Mbona makanisa na maharusi tunafanya umeshasikia jinai yoyote katika hilo.

Leo kongamano limefanyika kwa mafanikio makubwa je umesikia kuna hata sisimizi kakanyagwa??

Hivi nyie wafusasi wa shetani mwendazake nani aliwaloga??
 
Watu tunaamini hivyo kwakua hizi kelele zenu hazikuwepo kabla ya Magufuli kufariki,hivyo basi mnamdharau sana Samia.

Kimsingi hiyo kauli ya Mbowe inaamsha hisia za SSH,kutaka kuwaonyesha makucha yake na mwisho wa siku tutarudi kulekule.
Kelele zilikuwepo na ndio maama Magufuli alidhamilia kuua kila mpiga kelele mwisho wa siku akafa yeye
 
Kelele zilikuwepo na ndio maama Magufuli alidhamilia kuua kila mpiga kelele mwisho wa siku akafa yeye
Kufa ilikuwa ni lazima afe,hata kama asingewaua hao wapiga kelele,kimsingi kila unayemuona itafika muda atakufa tu hata kama atakuwa mwema kama malaika.


Turudi kwenye hoja,yani Rais anawajibu kistaarabu kuwa wampe muda(hajakataa),alafu mtu anajibu kuwa hawezi kumpa muda,yeye kama nani? Kwa mantiki hiyo anaruhusu kupimana nguvu na SHH?
 
Mwambie atumie mahakama na siyo risasi.

 
Tatizo ilikuwa kamanda Muroto tu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ akipiga biti moja tu nchi kimya!!!
anakwambia sisi tunawaambia hawa kinamama wamesema watavaa kanga nyeusi sisi tunasema wavae bukta tutawapigisha mazoezi mepesi halafu tutawapa maji ya kuoga watachagua ya baridi au moto hapo pembeni yake kuna wadada wamegonga gwanda hizo kama wanaenda mwezini hahahaha...
 

Wewe mkuu haki gani ya kikatiba usiyoipata wewe mwananchi wa kawaida inayokufanya ukose nahitaji yako ya msingi
 
Haya maneno ya kibabe ndio yaliwasababishia wakakimbilia Kenya, Dubai na Ubeligiji πŸ˜‚
Watafanya kazi yao muhimu kuwa ngumu sana wasipotumia akili.

Ni kazi inayotakiwa kufanywa lakini kwa akili kubwa ili wasiwaache wananchi nyuma.

Ni lazima watafute njia za kuwa na wananchi bega kwa bega, hasa wakati wa mwanzo wa mapambano. Yatakapokorea zaidi, watawahitaji wananchi kwa wingi kuwa upande wao, na si kuwatia hofu kabla ya mapambano kuanza.
 
Naona wewe ni mshamba wa siasa. Rais Samia ni mwanasiasa pia. Siasa ni mashinikizo kwa kutumia hoja. Kwani kamtukana au anahatarisha Usalama wa Rais au amempindu?

Uache ushamba
 
Watu tunaamini hivyo kwakua hizi kelele zenu hazikuwepo kabla ya Magufuli kufariki,hivyo basi mnamdharau sana Samia.

Kimsingi hiyo kauli ya Mbowe inaamsha hisia za SSH,kutaka kuwaonyesha makucha yake na mwisho wa siku tutarudi kulekule.
Umejuwaje kwamba hizo "kelele" unazozizungumzia wewe na mimi nimo kwenye kupiga kelele hizo.

Kwa kufanya hivyo tu nakudharau.

Kuhusu Magufuli kama angekuwepo, bado hujaeleza kama CHADEMA wangeacha kupiga kelele hizo, vinginevyo, basi wewe ni mmoja wao, kiasi kwamba unajua mipango yao yote.

Mnamdanganya Samia, hataweza kufanya lolote kuzuia mabadiliko ambayo ni lazima yatokee.

Sasa wakati umewadia, wa Tanzania kuondokana na ukoloni wa humu humu nchini unaofanywa na wanaojiona nchi ni yao na siyo ya waTanzania tena.

Kama kwa kuandika haya utaniona mimi kuwa mtu wa CHADEMA, hilo likusumbue wewe mwenyewe, mimi halinihusu.
 
Wakoloni weusi ni wabaya zaidi kuliko wakoloni wazungu
 
Kati ya Mbowe na Jiwe nani mjanja?? Jitu kimetoka huko shamba chato likaparamia mjini ona sasa yako wapi?

Ukija mjini njoo taratibu. Ulimbukeni umemponza yeye na genge lake sasa hivi wanakula tegoπŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…