Mbowe: Hatutompa muda Rais na hatukubali. Viongozi wa CHADEMA watakiwa kujiandaa kuanza mikutano nchi nzima

Rais anawajibu kistaarabu kuwa wampe muda(hajakataa),alafu mtu anajibu kuwa hawezi kumpa muda,yeye kama nani? Kwa mantiki hiyo anaruhusu kupimana nguvu na SHH?
Huwezi kufikia lengo hata siku moja kama tabia yako ni ya kuweka ahadi bila kujiwekea ahadi hiyo utaitimiza katika muda gani.

Waongo wote duniani ndivyo hivyo walivyo, hawezi kamwe hata siku moja kukupa ahadi ya uhakika atakayoitimiza kwenye muda maalum.

Na tabia hizi ndizo zinazosababisha mambo yetu kama nchi yawe ni ya hovyo hovyo, kwa sababu hatujiwekei kipimo na muda wa kutimiza

Huu uswahili swahili huu ni tatizo kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.

Mtu mzima, tena rais, anaongoka mbela za watu, halafu 'chawa' wanaanza kuweka 'spinning' zao.

Huku ni kuwadharau wananchi wa nchi hii. Mnawaona kama majuha.
 
pointi
 
Hahahah Muroto Giles ana mikwara ya kukata na shoka😂😂😂
 
Mkuu, hivi Magufuli angekuwepo, unajuwa kwamba CHADEMA wasingedai hayo wanayodai kwa vile alikuwa mbabe, una uhakika huo?

Unaamini Samia akiwa '"mbabe" katiba mpya watu wataacha kuidai? Unao uhakika huo?
Akiamuru wana usalama wafanye kazi yao kikamilifu hamna choko atakaeleta fyoko! Wote wataloana mapema tu na kukimbilia al jazeera na bbc kulia lia kwamba wameonewa ila adabu hawana!
 
kama hawampi muda si wabadilishe wenyewe tu
maana wanavyojisemea wao ndio wanchi pekee
 
Mna haki ila Not to that extent😂😂😂,,,Not to that extent!
 
Hamia Marekani mkuu.
 
Jpm ndio kiboko yao. Aliwanyoosha mpaka wakakimbilia jengo la EU kusemelea...
 
Wewe mkuu haki gani ya kikatiba usiyoipata wewe mwananchi wa kawaida inayokufanya ukose nahitaji yako ya msingi
Ivi tz mwananchi wa kawaida ni yupi , unaona mnavyotengeneza matabaka , mbona KWA mungu matabaka hamna ,Sasa nyie viburi vya kutengeneza matabaka unavitoa wapi?

Alafu sikia kila mwana nchi ana kipaumbale chake kwenye maisha yake Kama haki yake ya msingi na lazima kueshim, mfano mziki,siasa,mpira, n.k ,hivyo Kuna wengine ukizuia mikutano ya vyama vya siasa umegusa maisha yao, au ukazuia mpira tiyari unakua umewaumiza,

Hizi kauli za kuita watu kwamba ni wa kawaida, izi ni kauri za kikaburu ,na kibaguzi ndo maana viongozi wakishakua madarakani wanajiona Vip, Yani alikupeleka madarakani amekua mtu wa kawaida, katiba MPYA lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…