Mbowe: Hatutompa muda Rais na hatukubali. Viongozi wa CHADEMA watakiwa kujiandaa kuanza mikutano nchi nzima

Mbowe: Hatutompa muda Rais na hatukubali. Viongozi wa CHADEMA watakiwa kujiandaa kuanza mikutano nchi nzima

Rais anawajibu kistaarabu kuwa wampe muda(hajakataa),alafu mtu anajibu kuwa hawezi kumpa muda,yeye kama nani? Kwa mantiki hiyo anaruhusu kupimana nguvu na SHH?
Huwezi kufikia lengo hata siku moja kama tabia yako ni ya kuweka ahadi bila kujiwekea ahadi hiyo utaitimiza katika muda gani.

Waongo wote duniani ndivyo hivyo walivyo, hawezi kamwe hata siku moja kukupa ahadi ya uhakika atakayoitimiza kwenye muda maalum.

Na tabia hizi ndizo zinazosababisha mambo yetu kama nchi yawe ni ya hovyo hovyo, kwa sababu hatujiwekei kipimo na muda wa kutimiza

Huu uswahili swahili huu ni tatizo kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.

Mtu mzima, tena rais, anaongoka mbela za watu, halafu 'chawa' wanaanza kuweka 'spinning' zao.

Huku ni kuwadharau wananchi wa nchi hii. Mnawaona kama majuha.
 
Huwezi kufikia lengo hata siku moja kama tabia yako ni ya kuweka ahadi bila kujiwekea ahadi hiyo utaitimiza katika muda gani.

Waongo wote duniani ndivyo hivyo walivyo, hawezi kamwe hata siku moja kukupa ahadi ya uhakika atakayoitimiza kwenye muda maalum.

Na tabia hizi ndizo zinazosababisha mambo yetu kama nchi yawe ni ya hovyo hovyo, kwa sababu hatujiwekei kipimo na muda wa kutimiza

Huu uswahili swahili huu ni tatizo kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.
pointi
 
anakwambia sisi tunawaambia hawa kinamama wamesema watavaa kanga nyeusi sisi tunasema wavae bukta tutawapigisha mazoezi mepesi halafu tutawapa maji ya kuoga watachagua ya baridi au moto hapo pembeni yake kuna wadada wamegonga gwanda hizo kama wanaenda mwezini hahahaha...
Hahahah Muroto Giles ana mikwara ya kukata na shoka😂😂😂
 
Mkuu, hivi Magufuli angekuwepo, unajuwa kwamba CHADEMA wasingedai hayo wanayodai kwa vile alikuwa mbabe, una uhakika huo?

Unaamini Samia akiwa '"mbabe" katiba mpya watu wataacha kuidai? Unao uhakika huo?
Akiamuru wana usalama wafanye kazi yao kikamilifu hamna choko atakaeleta fyoko! Wote wataloana mapema tu na kukimbilia al jazeera na bbc kulia lia kwamba wameonewa ila adabu hawana!
 
Baada ya Rais kusema kuwa anataka apewe muda ili ajenge uchumi kwanza na mambo ya katiba na mikutano ya hadahara itafata baadae.

Mh Mbowe leo amesema wazi kuwa hawatompa muda Rais samia na hawatakubali bali watafanya mikutano ya hadhara na watadai katiba kwa njia yeyote ile inayofaa na ikiwezekna wataingia barabarani kuidai katiba... na kwa sasa swala la katiba ni lazima watake wasitake ni lazima katiba ipatikane.

“Ombi la Rais Sami kwamba tumpe muda kuhusu suala la katiba, hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza".

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza leo kwenye Kongamano la BAVICHA Tabata, DSM.

"Tutaidai Katiba mpya asubuhi, mchana hadi usiku. Kama wanataka tukae mezani, turidhie. Kama wasiporidhia, tutakutana barabarani. Hatutaridhia kushiriki Uchaguzi wowote bila kuwa na Katiba mpya au Tume Huru ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza leo kwenye Kongamano la BAVICHA Tabata, DSM.

My take:
Chaedema na Mbowe wameamua kumjaribu Mama? Wataweza kweli?
kama hawampi muda si wabadilishe wenyewe tu
maana wanavyojisemea wao ndio wanchi pekee
 
We najua unampenda mbowe,mshauri aachane na siasa za uhasama,hazina tija,,kama sio maneno ya shombo,saa hizi wangeshakaa na mh na kujadili mambo kistaarabu,
Alibugi mno,,hata JPM, kina mbowe,lema na henche ndio walimfanya achukie kukaa meza moja na wapinzani,
Cdm wazito mno kujifunza,,hivi mnafikili hiyo katiba mtaandika nyie,iwe kama mnavotaka?.
Mchakato ukianza ccm wakaingia kazini,,matokeo ni yale yale,,mtatia mpira kwapani..
Pesa zitakuwa zimepotea bure,,
Mna haki ila Not to that extent😂😂😂,,,Not to that extent!
 
Kweli Afri

Yaan Africa ,tunatumiwa vibaya sana.USA uwezi kusikia Republic wanafanya au wanataka mikutano baada ya uchaguzi.Baada ya uchaguzi ni kazi tuu.Sio kingine.Mbowe anajua vijana wengi hawana kazi na pia hawataki kazi.Kwa hiyo ni siasa tu.Ujinga mtupu.Miongoni mwa mabadiliko ya katiba ,ni kuondoa mikutano ya siasa baada ya uchaguzi.Tunacheleweshwa kufanya kazi.
Hamia Marekani mkuu.
 
Jpm ndio kiboko yao. Aliwanyoosha mpaka wakakimbilia jengo la EU kusemelea...
 
Wewe mkuu haki gani ya kikatiba usiyoipata wewe mwananchi wa kawaida inayokufanya ukose nahitaji yako ya msingi
Ivi tz mwananchi wa kawaida ni yupi , unaona mnavyotengeneza matabaka , mbona KWA mungu matabaka hamna ,Sasa nyie viburi vya kutengeneza matabaka unavitoa wapi?

Alafu sikia kila mwana nchi ana kipaumbale chake kwenye maisha yake Kama haki yake ya msingi na lazima kueshim, mfano mziki,siasa,mpira, n.k ,hivyo Kuna wengine ukizuia mikutano ya vyama vya siasa umegusa maisha yao, au ukazuia mpira tiyari unakua umewaumiza,

Hizi kauli za kuita watu kwamba ni wa kawaida, izi ni kauri za kikaburu ,na kibaguzi ndo maana viongozi wakishakua madarakani wanajiona Vip, Yani alikupeleka madarakani amekua mtu wa kawaida, katiba MPYA lazima
 
Back
Top Bottom