Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
- Utaijengea CHADEMA heshima
- Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.
Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.
Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.