Pre GE2025 Mbowe iokoe CHADEMA kwa kuchukua maamuzi mazito ya kumuunga mkono Lissu, usisubiri kesho!

Pre GE2025 Mbowe iokoe CHADEMA kwa kuchukua maamuzi mazito ya kumuunga mkono Lissu, usisubiri kesho!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
  1. Utaijengea CHADEMA heshima
  2. Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.

Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.

Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Tuhuma dhidi ya Lisu zitakapodhibitika bado atakuwa amechafuka.Tuombe Mungu zisiwe za kweli
 
Wakapambane ktk sanduku la kura
Huko hakuaminiki, ma ccm yatatumia hata mabilioni kuhonga wajumbe wasimchague Lissu kwasabb moto wake wanaujua vzr...kwamba Kizimkazi atatawala kwa shida sana Lissu akiwa mwenyekiti so bora waweke hilo boya lao ambalo tayari walishamalizana nalo!!.
 
Tunahitaji kiongozi yeyote apatikane kwa kupigiwa kura.

Endapo mh mbowe akijiuru ama kutaka kutokugombea,basi tunahitaji wananchi na wanachama mda wa kumpata mgombea mwingine atakaeshindana na Mh TL katika kinyang'anyilo hicho.

Hatuhitaji Yale ya Ccm kupita bila kupingwa.

Wapo wengi,sio Mbowe Wala Lisu tu.🙏
 
Wakati mjadala wa vyama vingi unaendelea, Nyerere aliwahutubia UVCMM na kuwauliza kama wana imani na sera za CCM, wakamjbu "sana tu". Akawauliza kama wana imani na uimara na kukubalika kwa CCM, wakamjibu "100 %". Akawauliza kama wanakubali sera ya vyama vingi. Wakamjibu kwa sauti kubwa " hapana". Alicheka sana na kuwauliza " kama mna imani na chama chenu kwa nini mnaogopa ushindani?".

Swali kama hili linaweza kuulizwa kwa wafuasi wa Lissu, " kama mna imani na uwezo na sera za mgombea wenu kwa nini hamtaki Mbowe ashindane nae? Si atamgalagaza tu?" Hamuwezi kudai demokrasia halafu wakati huo mkataka washindani wanaowapendeza nyie tu.

Tofauti na nyie sisi tunasema washindane, wapimwe na wapiga kura, wapiga kura waamue na wao waheshimu matokeo, hata kama watashindwa. Tunachokiomba ( ingawa ni too late) ni kampeni ya kuchafuana zisiwepo maana hiyo itaacha kidonda kikubwa katika chama.

Mimi binafsi nimeanza kuwa "ignore" baadhi ya watu kwa sababu naona wanadhani kunitukana na kunikebehi ni sehemu ya mjadala. Katika umri wangu, uvumilivu wa kutukanwa sina.

Amandla...
Wewe una akili.hao wengine ni mihemko inawasumbua alafu unakuta hawana masaada wowote kwenye chama zaidi ya ushabiki.na wengi ni wafuasi wa lissu.kuna haja ya wajumbe kua na utulivu sana vinginevyo watajikuta wamesombwa na wimbi la mitandao wakasahau kupiga kura kwa utashi na busara.
 
Huko hakuaminiki, ma ccm yatatumia hata mabilioni kuhonga wajumbe wasimchague Lissu kwasabb moto wake wanaujua vzr...kwamba Kizimkazi atatawala kwa shida sana Lissu akiwa mwenyekiti so bora waweke hilo boya lao ambalo tayari walishamalizana nalo!!.
Acha kuamini maneno ya watu.huyo lissu anaweza kuja kua ndo mbovu kuliko mnavyodhani.Inawezekana umachachari wake nikwasababu hakua kwenye hiyo nafasi.Wako watu waliwahi kuaminiwa ila ikawa kinyume chake.tubakishe maneno.
 
Naamini unatania, tatizo ni wapiga kura!
Sasa mkuu wazo lako ni kuwa kusiwe na uchaguzi. Lissu apite bila kupingwa?

Katika jambo lililonikosesha raha sana ni kugundua kuwa CHADEMA nayo imejengwa kwenye misingi mibovu kabisa ya PATRONAGE na kuishi nayo miaka yote hii huku kikijinasibu ni chama cha kidemokrasia.

Yaani chaguzi zote za ndani za CHADEMA zilikuwa batili. Na hivyo lilikuwa KOSA KUBWA sana kuondoa ukomo wa kugombea kwa mwenyekiti (ambaye tayari kajijengea wapiga kura ambao tegemezi kwake!).

Leo hii wafuasi wa CHADEMA wanaogopa uchaguzi wa mwenyekiti wao. Hawataki uwepo bali kuwe na makabidhiano tu! Wanaogopa kivuli chao!

Halafu naiona HATARI KUBWA sana kwa chama kuweka tumaini lake lote kwa MTU MMOJA pekee (Tundu Lissu). I really wish wangekuwepo na wengine kwenye uchaguzi huo. Nilimfikiria mtu kama Heche lakini kwa kadiri siku zinavyosonga inadhihirika kuwa CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa mikingamo kibao (puzzling INTRIGUES).

Kinachoonekana sasa kazi namba moja, ikiwezekana, ni ya kuweka UONGOZI WA MUDA, ufanye REFORM kubwa ndani ya CHADEMA ili kukiwezesha chama kufanya uchaguzi huru na wa haki wa mwenyekiti na viongozi wake wote wa kitaifa na kuajiri watendaji makini wenye sifa (merit) pale makao makuu.

Short of that, sioni CHADEMA ikiendelea na hadhi iliyokuwa nayo miaka yote hii. Maybe this time kuna ma-genius huko serikalini wamefanikiwa kuivunja CHADEMA.
 
Je unawajua hao unaowaita wapiga kura? Oh judgement, thou art fled to brutish beasts and men have lost their reasons.

Kwa vyovyote watakavyopiga kura, uwepo wa Mbowe kwenye kinyang'anyiro hicho unafanya zoezi hilo kuwa na doa.

Sisi wenye mapenzi ya kweli kwa hiki chama tumemshauri tu Mh. Mbowe kutumia busara na hekima kumuunga mkono Mh. Lissu.


Sasa hivi? Kwani kwa miaka hiyo ishirini Mwenyekiti hakuwa sura na kiongozi Mkuu wa Chadema? Kusema kweli Fundi Mchundo, nimeshindwa kabisa kuelewa unachotetea.
Mimi nimeweka msimamo na mtizamo wangu kuhusu Lissu na Mbowe. Wewe weka wa kwako ili tuweze kujadiliana kama watu wazima. Kwa vile umesema hauelewi ninacho tetea, nitakufahamisha. Ninachotetea ni haki ya Mbowe kugombea ambayo nyinyi mnaojifanya mna mapenzi ya kweli na CDM mnataka kumnyima. Ninachotetea ni kuwa heshimuni haki yake ya kugombea. Ninachotetea ni yeye apewe heshima anayostahili hata kama unadhani ame over stay.

Kama hamumtaki fanyeni kampeni ( za kiungwana) ili ashindwe. Kama vile wewe unavyoona Mbowe hafai, mimi naona Lissu hafai. Hauwezi kunilazimisha nimkubali kama ambavyo siwezi kukulazimisha umkubali Mbowe. Mbowe anamjua Lissu kuliko wewe na mimi. Heshimu uamuzi wake wa kuamua kuwa hastahili kuongoza chama chao. Ni hekima na busara zake ndio zimemfikisha hapo. Kwetu sisi wengine, kila siku inavyoenda ndio Lissu anavyojidhihirisha kwetu kuwa Mbowe amemsoma vizuri. Wewe kama hulioni hilo endelea kumpigia kampeni Lissu mradi tu usilazimishe apite bila kupingwa. Ni kwa kupitia hizi kampeni ndio watu watamjua vizuri Lissu na Mbowe. Kwa nini unaogopa?

Mwisho, naomba tutumie lugha za staha tunapojadiliana. Kwa kweli vijembe havipendezi katika mjadala muhimu kama huu. Sana sana unanifanya nione kama hauna nia njema katika huu mjadala.

Amandla....
 
Mimi nadhani ni mateka kwa sasa. Huyu si Mbowe niliyemfahamu kabla.
Uchaguzi ni wa nini sasa? Kama Lisu anakubalika zaidi ya Mbowe acheni kura ziongee hiyo ndio Demokrasia.

Yani mtu anakubalika halafu mnataka aachiwe kama viti maalum? Jacob Zuma mbona alimshinda Thabo Mbeki kwenye Urais wa ANC? Kwa nini mnaogopa uchaguzi?
 
Kila wakati ni biashara ya kuanzisha vyama, naona kwetu haitaeleweka haraka, kwa majirani zetu naona ndiyo rahisi! 😃
Kwani maalim Seif ameanzisha ACT? Kwa nini wasiokubaliana na uongozi wa Mbowe waende Chauma? Au mnataka ready made?
 
Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
  1. Utaijengea CHADEMA heshima
  2. Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.

Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.

Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Mbowe linapokuja swala la pesa hawezi kukuelewa
 
Hii ni JF, where we dare. Please educate me ikiwezekana hata inbox.
Mkuu check hapa, chagua ya kweli ja uwongo uyaache hapa hapa....

Mengine tuwlnaweza discuss private, ila midahalo karibu yote kwanini TL na sio FAM is more rhetorical than a reality na imejengwa kwenye chuki zaidi kuliko hali halisi .
👇
VIONGOZI WA SAUTI YA WATANZANIA WANAOPAMBANA KUITEKA CHADEMA!

Anaandika Jogoo wa Shamba

Nawaletea majina ya viongozi wa kikundi kinachoitwa Sauti ya Watanzania (SYW) ambao wamekuwa mstari wa mbele kupambana na kuhakikisha kuwa wanachukua uongozi ndani ya Chadema!

Watu hawa wako makundi matatu na ambayo hawajuani sana kiundani kwani wamekutana mtandaoni na ndio wanaosuka mkakati wa kuhakikisha wanaiteka Chadema!

Kuna ambao walijikuta wanaunga mkono kila kitu bila kujua madhumuni ya kikundi hiki, wapo watu wa mfumo na wapo wana mikakati wa CCM !

Nitaweka orodha na wasifu mfupi sana kwa leo ili watanzania mfahamu hawa watu na malengo yao!

Orodha ya Viongozi wa SAUTI YA WATANZANIA!

1. Askofu Arthur Chilipwel - Mwenyekiti, muulizeni yeye na Kipilimba Wana uhusiano gani? Askofu huyu Kanisa lake na lile la Kipilimba yana uhusiano gani na yalianzishwa na nani? Kipilimba alikuwa Mkuu wa TISS (DGIS) wakati wa Magufuli,na ni Mchungaji Kanisa!
2. Albini Saragu - Katibu mzaliwa wa Manyara, ndugu yake Dr.Slaa, alikuwa mhadhiri msaidizi UDSM elimu, ila alipopata fursa ya kwenda kusoma Uingereza akaamua kupotelea huko huko! Anafanya kazi maalum akiwa huko na ndio Katibu anayeratibu Kila jambo! Alipofika huko alivuruga Diaspora base ya Chadema yote, ndio maana hakuna anayehangaika naye arejee kwani kazi anaweza sana ya kuvuruga!
3. Askofu Augustine Mpemba, huyu kafichama sana, atajitokeza mwenyewe baada ya kumtaja leo, ila aulizwe anasimamia Kanisa gani na pia anauhusiano gani na wenye mamlaka! Mtu hatari, anaogopwa sana kwenye mfumo kuliko Kipilimba!
4. Askofu Mwanamapinduzi, huyu ni lile kundi lililoingia bila kujua liko upande gani na linafanya nini. Yupo Kanisa la Askofu Gwajima, na anasimamia Kibaha, huyu ni mwandani wa Gwajima na anapeleka taarifa zote kwake, anatokea Itilima, alishindwa Uchaguzi Itilima akagombea Kanda ya Pwani nako akashindwa!
5. Dr. Wilbroad Slaa, - huyu mnamjua vyema, sihitaji kusema lolote ,ila jueni mission yake ni kuivuruga Chadema.
6. Joseph Chacha, - Kijana wa mfumo ambaye anazungushwa Balozi mbalimbali Duniani, huyu huwa Afisa Mwambata na mara nyingine Afisa Itifaki, ameishi huko Duniani na watu hawamjui sana! Kijana kutoka Mara , anatimiza wajibu wake wa kulinda Dola na mambo yake! Amejitahidi kujipenyeza karibu na Lissu na kuaminika!
7. Kaswahili Juma, - huyu Kijana wa Chadema, anatokea Magu, hajui kinachoendelea, ila ndio wale wako kwenye _MRADI WA KUUA CHADEMA bila kujua nani wanawafadhili! Aliomba kwenda USA na alisaidiwa sana na Chadema, huko SYW Wanamuita reporter!
8. Eliderick Kanyemela, - huyu ni reporter na hajui lolote! Anatumwa na Dr.Slaa kwani ni ndugu yake na Mushumbusi!
9. Liberatus Mwang'ombe, huyu anatokea Mbarali, Yuko USA, huyu anafanya kazi ya mhudumu wa afya, yaani NESI ndio amekuwa mstari wa mbele kushambulia Chadema, huyu ni msaidizi maalum wa Peter Msigwa, alitumika sana kusambaza Fedha za Diaspora wakati wa uchaguzi wa Njombe na Kanda ya Nyasa! Chadema walifanya kosa kubwa sana kumuamini na alikuwa ndio kiungo kati yao na Congress ya Marekani! Walipokata mrija huo ndio ikawa vita yake na Chadema, aliwahi kushiriki vikao vya IDU, mrija ulipokatwa vita ikaanza! Chunguza yeye ni nani na Kapilimba alihusika vipi kumpeleka huko USA! Huyo ndio analipa vijana kama kina Gwamaka na wengine kufanya huo wajibu! Mfumo unamwelewa sana!
10. Mpaluka Said aka Mdude - huyu mwanaharakati ambaye ameingizwa kwenye genge ambalo halijui! Alidhani yuko na wanaharakati, kumbe yuko na watu kazini waliotumwa na Mamlaka zinazomtesa kila siku ila alinufaika na kundi hili tangu wakati wa Maandamano na alikuwa analipwa gharama zote na kundi hili!
11. Wakili Mwabukusi, huyu na Mdude hawana tofauti! Yuko Sasa TLS ila ana kampeni ya "Mama Samia legal Aid" kashasahau habari za chapter four wala Mkataba wa Bandari na DP WORLD! Hasemi lolote kuhusu ahadi yake ya chapter four! Juzi kati kapokea new model Prado! Anasema hiyo ni project aliikuta! Haya arejeshe madaraka Kwa Sungusia! Huyu atakuwa TLS Kwa miaka 3! The longest serving president ever! Term limit ianze naye kwani wenzake wote walikuwa na kipindi cha mwaka mmoja!
12. Alfa Zulu - tafuteni wasifu wake
13. Namourita Fayyene - tafuteni wasifu wake!

Naishia hapo kwa Leo!

©Jogoo wa Shamba
 
Mkuu check hapa, chagua ya kweli ja uwongo uyaache hapa hapa....
Fortilo, Kama unaamini tuhuma kama hizo sawa, hiyo ni haki yako
Swali...je kwa nini huamini tuhuma zinapoelekezwa upande wa pili?
 
Kwanini Lissu asikae pembeni amuache Mbowe?
Kwanini wasishindane kwenye sanduku la kura?
hii tabia ya kuachiana ipo kwetu CUF il siyo CHADEMA.
Kwa nini Mbowe asikae pembeni amwachie Lissu?
Tatizo ni washika bendera na wachezaji kuwa timu moja.
Hiyo tabia ya uchafuzi ipo kwenu CCM na si Chadema.
 
Kwa nini Mbowe asikae pembeni amwachie Lissu?
Tatizo ni washika bendera na wachezaji kuwa timu moja.
Hiyo tabia ya uchafuzi ipo kwenu CCM na si Chadema.
Kwanini Lissu asikae pembeni amwachie Mbowe?
 
Fortilo, Kama unaamini tuhuma kama hizo sawa, hiyo ni haki yako
Swali...je kwa nini huamini tuhuma zinapoelekezwa upande wa pili?
Ahsante mkuu,
Kwanza hizi tuhuma za pande zote mbili mimi siziamini.

Hawa wanasiasa wawili ni marafiki sana, na hizi drama zao tumeanza kuzisikia sio muda mrefu, wamekuwa marafik kwa zaid y miaka 20 sasa .

Nini kimetokea?

Loyalty betrayal...

Mmoja kamsaliti rafik yake, na mwingine kasaliti Umma.

Wanasiasa hawana desturi ya kufikiria maslah ya Umma linapokuja suala la maslahi yao binafsi...

Tushukuru wamesalitiana maana tusingejua haya yote, lakini kwa manufaa ya nani?

Tunaweza shangilia haya, lakini kwa akili za kawaida ni kama "tukose wote" watanzania tutakosa wa kutusemes proper kwa miaka mingi mbele, ikiwa mambo haya yataharibika sana .

Muda utasema.
 
Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
  1. Utaijengea CHADEMA heshima
  2. Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.

Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.

Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Wapambane tu tujue nani anakubalika.

Bila kupambana tunaweza kukosa closure na resolution ya kujua nani anakubalika zaidi.

Pia, kumtaka Mbowe asigombee uenyekiti ni kumuingilia kwenye haki yake ya kikatiba ya CHADEMA ya kugombea uongozi.

Haitakiwi umwambie Mbowe ampishe Lissu kwa sababu wewe unampenda Lissu. Vipi kama wanachama wa CHADEMA wanampenda Mbowe zaidi ya Lissu, huoni kumtaka Mbowe ampishe Lissu kutawanyima chaguo lao?

Waache Mbowe na Lissu wagombee uenyekiti, anayekubalika zaidi ashinde.

CHADEMA ikiweza kushinda mtihani huu itakuwa imara zaidi.

Isipoweza kushinda mtihani huu tutajua kuwa haikustahili kuwa chama cha kitaifa chenye potential ya kuchukua uongozi wa nchi anyway.
 
Mimi binafsi nimeanza kuwa "ignore" baadhi ya watu kwa sababu naona wanadhani kunitukana na kunikebehi ni sehemu ya mjadala. Katika umri wangu, uvumilivu wa kutukanwa sina.
Kama kuna mtu katukanwa, tena matusi ya nguoni, ni Mh. Tundu Antiphas Lissu na hakuanza kutukanwa juzi wala jana.

Lissu alianza kutukanwa toka uchaguzi ndani ya Chadema uanze katika ngazi za chini kabisa na nyakati hizo hakuna aliyemgusa Mbowe.

Kama yupo aliyeonesha uvumilivu mkubwa ni Mh. Tundu Antiphas Lissu. Kampeni dhidi yake zilianza mapema tu lakini alikaa kimya.

Hadi alipotaka kutetea kiti chake cha makamu wa mwanyekiti wa chama. Wenzake kumbe walishapanga safu zao tokea awali.
 
Back
Top Bottom