Pre GE2025 Mbowe iokoe CHADEMA kwa kuchukua maamuzi mazito ya kumuunga mkono Lissu, usisubiri kesho!

Pre GE2025 Mbowe iokoe CHADEMA kwa kuchukua maamuzi mazito ya kumuunga mkono Lissu, usisubiri kesho!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ninatofautiana na wewe. Lissu alipotangaza tu kugombea wafuasi wake wakaanza kumbeza Mbowe na kutaka asigombee ( hapo hata hajaonyesha nia) ya kugombea. Dharau na vijembe vya Lissu vilianza zamani sana. Kuna wakati alimtumia surrogate wake Msigwa kumshambulia Mbowe). Hapakuwa na haja ya kumshambulia Lissu wakati ule kwa sababu hamna aliyepinga uamuzi wake wa kugombea urais.
Yericko alimshambulia baada ya kutoa tuhuma za uongo dhidi ya Wenje na viongozi wengine (ingawa hakumtaja ilikuwa wazi alimlenga Mbowe). Alipobanwa kutoa ushahidi akasema aliyempa amefariki! Tuhuma nyingine za Yericko mpaka leo hazijajibiwa. Kuwa alikuwa hahudumii nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa CDM mpaka ikabidi apewe Kibatala. Kuwa alikuwa hahudhurii wala kuitisha vikao.

Ni baada ya haya maneno ndio Ntobi akamshambulia kwa maneno yasiyofaa lakini alibanwa akaomba msamaha. Hamna hata mmoja aliyemuomba msamaha Mbowe kwa kumuita kibaraka, king'ang'anizi n.k. Na wakati wote huu wa mashambulizi ya Lissu, Mbowe hajasema neno.

Mimi naamini hapo ulipo ni kuwa hautaki kusikia lolote baya dhidi ya Lissu. Hiyo ni haki yako kama vile ilivyokuwa haki yangu kukupinga. Lakini kwa vile nimetambua kuwa ni futile exercise, sitakujibu tena kwenye suala lolote linalohusu uchaguzi wa CHADEMA. Nitangojea matokeo na nitamkubali yeyeto atakaeshinda.

Amandla....

Ninyi ndiyo mnaomdanganya mwamba.

Kuelekea dakika ya tisini: "Maoni ya wanachama yasiposikilizwa, CHADEMA njiani kulia na kusaga meno!"

Na mnachokitafuta mtakipata.
 
Mbona Kenya wanachama wa ODM hawajawahi taka Raila Odinga aachie madaraka ODM pamoja na kuunga mkono Serikali ya Uhuru Kenyata na sasa Ruto pia
Ndio maana miaka yote anashindwa, wenzie wanaanzisha vyama vipya fasta tu wanafanikiwa. Je wanachama wa chadema wanataka miaka yote washindwe??
 
Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
  1. Utaijengea CHADEMA heshima
  2. Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.

Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.

Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Retired Quinine Lusungo
 
Wakati mjadala wa vyama vingi unaendelea, Nyerere aliwahutubia UVCMM na kuwauliza kama wana imani na sera za CCM, wakamjbu "sana tu". Akawauliza kama wana imani na uimara na kukubalika kwa CCM, wakamjibu "100 %". Akawauliza kama wanakubali sera ya vyama vingi. Wakamjibu kwa sauti kubwa " hapana". Alicheka sana na kuwauliza " kama mna imani na chama chenu kwa nini mnaogopa ushindani?".

Swali kama hili linaweza kuulizwa kwa wafuasi wa Lissu, " kama mna imani na uwezo na sera za mgombea wenu kwa nini hamtaki Mbowe ashindane nae? Si atamgalagaza tu?" Hamuwezi kudai demokrasia halafu wakati huo mkataka washindani wanaowapendeza nyie tu.

Tofauti na nyie sisi tunasema washindane, wapimwe na wapiga kura, wapiga kura waamue na wao waheshimu matokeo, hata kama watashindwa. Tunachokiomba ( ingawa ni too late) ni kampeni ya kuchafuana zisiwepo maana hiyo itaacha kidonda kikubwa katika chama.

Mimi binafsi nimeanza kuwa "ignore" baadhi ya watu kwa sababu naona wanadhani kunitukana na kunikebehi ni sehemu ya mjadala. Katika umri wangu, uvumilivu wa kutukanwa sina.

Amandla...
Uchaguzi ungekuwa unashirikisha wanachama wote kusingekuwa na shida,.
Tatizo ni hawa wajumbe na namna walivyopatikana kwenye baadhi ya maeneo.
 
Mtahangaika sana, bado hadi muaibike katika BOX la kura na tumeshasema anayeshindwa hamna visingizio na lazima abakie kukijenga chama pamoja.
Hao wanaharakati wa mitandaoni wao ni kuvamia vyama, hawajui CDM imepitia yapi hadi hapa ilipo.

Mbowe - mwendo mdundo - mtoto kau...
Mbowe hawezi kushindana na muda akashinda. Muda ukuta,
awamu zote aliungwa mkono na kutetewa na wanachama wa CDM, lakini kwa sasa amepoteza mvuto na ushawishi.
Cdm inapoelekea chini ya Mbowe itakuwa kama ilivyo CUF, UDP na TLP.
 
Uchaguzi ungekuwa unashirikisha wanachama wote kusingekuwa na shida,.
Tatizo ni hawa wajumbe na namna walivyopatikana kwenye baadhi ya maeneo.
Hilo mtu kama Fundi Mchundo hawezi kulielewa si kwa sababu hana uwezo wa kuelewa ila mahaba yamefunga kabisa hiyo njia na kuweka kufuli kubwa.

Mathalani tuseme Mbowe anapata asilimia 100% ya kura za wajumbe, bado sisi wengine tutahoji uhalali wa hizo kura...si husemwa ukiona vyaelea vimeundwa!

Sanasana atakuwa amevunja hata ile rekodi iliyowekwa na CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Je na huo mliuita uchaguzi au uchafuzi?
 
Then stand up and be firm in that resolve. You seem to be standing on wobbly legs while expressing your desires!
Yes, wobbly legs indeed, at the same time deliberately skipping important details.

Can you by name of God say with confidence who is indriving these agenda?

As to why FAM is portrayed as so bad and corrupt now but not 3 years ago?

And TL is so clean, saint from heaven who will distribute 107M to all over 1200 CDM leaders?

Turbidity politics revolving around the intention is what scares me a lot.
 
Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
  1. Utaijengea CHADEMA heshima
  2. Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.

Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.

Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Na hili ndilo mimi nilitegemea, na bado hajachelewa!
 
Ni busara kwa Mh. Mbowe kuachia nafasi ya uenyekiti wa chadema kwa wanachama wengine waingie kwenye kinyang'anyiro hicho. Hii italeta afya kwa chama na demokrasia kwa ujumla. Mi binafsi namshauri abaki kuwa mshauri wa chama kutokana na muda aliokaa madarakani. Kung'ang'ania uenyekiti kwa muda mrefu namna hii kunaleta mashaka makubwa kuwa chama hakina watu wanaoweza kuongoza zaidi yake hivyo ni chama kisichofaa kupewa dola. Pili kunanini ndani ya uenyekiti mpaka ang'ang'anie namna hii?. Kung'atuka ni jambo jema kwake na kuachia fikra na mawazo mapya yaje.
 
Chama cha PRI cha Mexico kilizaliwa mwaka 1929 na kilitawala hadi 2000, miaka 71 baadae. Vyama vya upinzani havikukata tamaa muda wote huo. Chama cha ANC kilizaliwa 1912 na uchaguzi wa kwanza uliowahusisha watu weusi ulifanyw 1994, miaka 83 baadae. Muda wote huo hawakukata tamaa. Hauwezi kumlaumu Mbowe bila kuangalia mazingira ya kisiasa yaliyokuwepo wakati wa uongozi. Hata Chadema kuweza kufika hapa ilipo ni maajabu na ni testament ya umahiri wake. Huyo anaetaka kumrithi anatumia maneno yale yale ( Mbowe ni fisadi, Mbowe amekaa mno, Mbowe ni corrupt n.k.)ambayo wapinzani wake wamekuwa wakiyatumia siku zote katika juhudi zao za kutaka watu wakose imani nae na chama. Bila shaka Mbowe anatambua kuwa uhai wa chama chake uko mashakani kwa sababu kwa mara ya kwanza mashambulizi haya yanaongozwa na mtu ambae sehemu kubwa ya jamii ina imani nae.

Mbowe hajibu hizi shutma kwa sababu anajua akifanya hivyo atakibomoa zaidi chama chake. Ila sitashangaa kama Mbowe ana kitu anachokijua kuhusu mpinzani wake ambacho akikiweka mbele ya wapiga kura kitawafanya watambue kuwa yeye sio yule mtu wa kwenye majukwaa. Hataweki hadharani kwa kujua kuwa itakuwa kuongeza majeraha katika chama chake.

Tusubiri tu hali itakavyokuwa tukikaribia uchaguzi.

Amandla...
 
Hilo mtu kama Fundi Mchundo hawezi kulielewa si kwa sababu hana uwezo wa kuelewa ila mahaba yamefunga kabisa hiyo njia na kuweka kufuli kubwa.

Mathalani tuseme Mbowe anapata asilimia 100% ya kura za wajumbe, bado sisi wengine tutahoji uhalali wa hizo kura...si husemwa ukiona vyaelea vimeundwa!

Sanasana atakuwa amevunja hata ile rekodi iliyowekwa na CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Je na huo mliuita uchaguzi au uchafuzi?
Atapataje kura 100% wakati kuna wajumbe wameishajitokeza kuwa hawatampigia kura? Kabla ya kunisema mimi unatakiwa ujiangalie mwenyewe kioo. Unajifanya kuwa ni mpenda demokrasia lakini unaweka sharti kuwa ni lazima mtu wako ashinde ndio utakuwa wa haki!

Hauwezi kuamini kuwa hawa wanaopiga kura wanawajua hawa wagombea kuliko ambavyo sisi mashabiki wa online tunavyoweza kuwajua.

Tuwaache wafanye kazi ambayo katiba imewapa bila vitisho vyovyote. Na tukubali matokeo hata kama hatuyapendi kwa mustakabali wa upinzani katika nchi yetu.

Amandla....
 
Kwa vile Mag3 amenishutumu mimi binafsi inabidi nimfahamishe kwa nini Lissu hafai kuwa Mwenyekiti wa Chadema.
Awali ye yote ni lazima nikiri kuwa nilikuwa naamini kuwa timu ya Lissu na Mbowe ingekuwa formidable ingewasumbua sana CCM. Ndio maana Lissu alipotangaza kutaka kugombea haikunipa shida sana kwa sababu nilifikiri pengine kuna makubaliano ya Lissu awe Mwenyekiti huku Mbowe akimuunga mkono. Kilichonistusha ni mashambulizi ya shari ( mengine kwa kusema kweli yalikuwa ya kumvunjia heshima mbele ya sio tu wanachama wenzake bali taifa zima) yaliyoanza kuelekezwa dhidi ya Mbowe bila ya Lissu kusema lolote. Badala yake akaleta shutuma zisizo na mbele na nyuma kumhusu Wenje na Abduli. Mimi nilijua kuwa Wenje anatumika kama fig leaf maana ni Mbowe peke yake ndie angeweza kumkingia kifua mbele ya shutuma kutoka kwa Makamu Mwenyekiti. Yericko alipomtetea Wenje nikaona utetezi wake una mashiko. Wenje ndio akapiga msumari wa mwisho ambapo Lissu akabaki kujitetea kuwa conveniently aliyempa ushahidi amefariki dunia. Hapa pia, akaacha mlango wazi ili watu wafikiri kuwa mhusika alikuwa Marehemu Ali Kibao na Mbowe alihusika katika kifo chake. How low can one get?

Lissu pia aka insinuate kuwa Mbowe alikuwa hachangii pesa Chadema kiasi ambacho jamii inaamini. Naona nafsi imemsuta ( pengine baada ya kutambua kuwa kuna risiti na yeye ataulizwa ni kiasi gani amechangia) ndio amekiri kuwa Mbowe alikuwa anakikopesha CDM pesa nyingi.

Lissu pia amekiri kuwa Msigwa ni rafiki yake. Lissu pia ameshindwa kumsema Msigwa ambae hafichi kuwa lengo lake kubwa ni kuibomoa Chadema kwa niaba ya CCM. Alichofanya Lissu ni kudai tu kuwa hoja za Msigwa zijibiwe. Sasa kwa nini Mbowe asiamini kuwa Lissu alikuwa anashirikiana na Msigwa kumkashif Mbowe hata kabla ya uchaguzi wa kanda ya Nyasa.

Lissu akatoka hadharani na akasema kuwa kuna watu wanataka kumuua na kumsingizia Mbowe. Kwa juu juu utadhani kuwa amemlinda Mbowe lakini alikuwa amepanda mbegu ya watu kuamini kuwa Mbowe kweli anaweza kuhusika. Na kesho yake akatinga katika ofisi za Chadema huku amevaa bullet proof vest.

Kabla ya hata uchaguzi kufanyika ameanza kusema kuwa kuna mbinu za kuuhujumu. Kama kweli anajua hilo kwa nini asikae na sekretariat ya Chadema pamoja na wagombea wenzake ili watafute njia ya kuzuia usihujumiwe? Kwangu mimi nikuwa amepofushwa na personal ambition kiasi ya kutojali hatma ya chama anachodai anakipenda. Nitaendelea.

Amandla...
 
Can you by name of God say with confidence who is indriving these agenda?
I can state with confidence, with no contradictions whatsoever; that, Tundu Lissu is what Tanzania needs most at this time.

As to "who drives the agenda"? Why should anyone waste their time worrying about driving any agenda when we know the only important agenda is one driven by Tanzanians for the wellbeing of their nation?
Tundu Lissu is the only candidate fighting for this agenda at the moment. If you have doubts about that, then you need to carefully examine your conscious.
 
I can state with confidence, with no contradictions whatsoever; that, Tundu Lissu is what Tanzania needs most at this time.

As to "who drives the agenda"? Why should anyone waste their time worrying about driving any agenda when we know the only important agenda is one driven by Tanzanians for the wellbeing of their nation?
Tundu Lissu is the only candidate fighting for this agenda at the moment. If you have doubts about that, then you need to carefully examine your conscious.
Its getting emotional after the power struggle failure...

I can see the motion drivers loosing hope and starting to trust God to whom they initially thought they can without him .

TL is super good, most consequential politician of our time and highly required candidate now than ever to move us where we have stuck, but he started with the wrong foot, joining the opposing gang .

You cant fight your master and win....

Whether Tanzanians needs him or not, he should submit to his master who was feeding him for the past 20 years ..

Whether CDM will stand and be trusted after this cause is the question for another day ....
 
As to why FAM is portrayed as so bad and corrupt now but not 3 years ago?

And TL is so clean, saint from heaven who will distribute 107M to all over 1200 CDM leaders?
There's a stuck difference between the two' you can't even begin mistaking one for another!

Mbowe's dirty tricks are finally laid bare for everyone to see! Evidence is abundant and unmistakable; evidence that is finally laid clear on issues that were not easily explained in the past. Lowassa's candidacy, COVID- 19; hard to explain expenditures in the party. But his adventures with Samia, into the so called "Maridhiano", this has been the tipping point of his downfall from grace.
Look at this shameful misadventure in a final nail into his coffin as a respected political figure! Why would one want to play into a pond full of dirt and expect to come out clean!
 
Back
Top Bottom