ALL IS POSSIBLE. SIDHANI KAMA MBOWE ANA KISASI. ALISEMA WAKI KUWA NIKISHINDWA NAKWENDA KUTAFUTA MAPEKECHEE.
BUSARA INGELIKUWA KUMTAFUTA AKAE NA WAFUASI WAKE WAACHE KUKIGAWA CHAMA. HILO ANAWEA KUFANYA, MY WORRY NI LISU MAANA HAELEWEKI!
Mie naona kuwa Lissu ni mpole sana.
Hebu angalia vifungu hivi vya kikatiba na kikanuni:
Kanuni za Chadema:
10.1 Maadili ya Viongozi
(iii) Kila kiongozi anatakiwa kulinda siri zote za Chama.
(ix) Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa Chama au
wanachama wake.
(x) Kiongozi asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelezwa kwenye kanuni za Chama.
(xi) Kiongozi anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa na viongozi wa ngazi ya juu au vikao halali na kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kwa kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye kanuni.
(xii) Itakuwa marufuku kwa kiongozi wa CHADEMA kukashifu Chama, kiongozi au mwanachama yeyote wa Chama au vyama vingine, au viongozi wa kiserikali. Ni muhimu viongozi wa CHADEMA waelewe tofauti ya kashfa na ukosoaji wa kisiasa.
Katiba ya Chama:
6.3.6 (d) Bila kuathiri masharti ya vipengele (a) na (c) hapa juu, kiongozi yeyote anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao cha juu ya ngazi yake ya uongozi.
Halafu mwanachama anapanua mdomo wake na kusema kuwa Lissu ni "Kasongo yoyo" na bado anabaki kwenye chama?
My take:
Chadema inao uwezo wa kutumia kanuni ya "
kikao cha juu" ili kuleta nidhamu kwa mpigo mmoja tu ndani ya chama chote.
One word to a wise man is enough ("verbum sapienti sat est")!