Viongozi wa kiroho muwe kweli Manabii (wa kweli), Wafalme (wa kweli) na Makuhani wa kweli wakati wote na kwa kondoo wote wa BABA hata nyakati ngumu. Msielemee upande moja. HAKI ndicho kitu cha kwanza, AMANI itafuata palipo na haki. Mungu Baba ndiye aliyetuleta Tannzania (Tanganyika) sisi wote.
Hakuna binadamu mwenye jukumu hilo. Sisi sote tuna haki sawa ndani ya nchi hii. Hivi mnadhani vurugu ndani ya nchi zinaletwa na wananchi? La hasha, bali viongozi waliosahau kutekeleza wajibu wao, wakaanza kutekeleza matakwa ya Ibilisi Lusifa na vibaraka wake.
Kiongozi bila haya unafurahia aibu wanayotenda kina Sabaya kwa Watanzania wenye mtizamo tofauti nawe. Viongozi wa kiroho mmekaa kimya. Leo hii neno "Mwendazake" limewatoa karamuni mnakokula vinono na watesi tena kwa gharama zetu.
Mungu daima atabaki YULE Mwenye uwezo ulio MKUU unaodhibitiwa na Destruri yake iliyo bora (UPENDO, HURUMA, UPOLE, UVUMILIVU, UKARIMU hata kwa hao watesi wetu, WEMA, MKWELI, DAIMA MWAMINIFU). Mara zote tusimame kwenye kweli na haki, unafiki tuachane nao. Amin