Mbowe: Kukosa pesa za MCC Inachafua jina la nchi ktk medani za kimataifa

Mheshimiwa Mbowe, are you serious kumtaka Rais amwamuru DPP afute kesi zilizoko Mahakamani. Mimi nimekuwa naelezwa kuwa DPP yuko huru na hatakiwi kuingiliwa na yeyote yule, au sheria zetu zimebadilishwa kinyemela?
 
Ninyi Lumumba bajeti yetu ni sh ngapi kwa mwaka? Trillion 1.3 kwa mwezi zidisha mara miezi 12 utapata bei gani? Na je, hiyo bei uliopata ni asilimia ngapi ya bajeti yetu? Bila misaada hatuwezi kuenda. Tunaihitaji.
 
Politics is difficult than physics. Albert Einstein
 
Hii inaonyesha Tanzania hakuna democracia maana kama unakamata watu wasiokuwa na Bhatia na kuwabambikia kesi na kukaa na vifaa vyao mpaka sasa huo ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu hivyo mcc hawawezi kukupa msaada kwani haki za binadamu na democracia ni kiongozi mwa masharti yao hivyo Tanzania haijakidhi.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAULI YA MWENYEKITI FREEMAN MBOWE

KUHUSU

UAMUZI WA BODI YA MCC KUZUIA MSAADA WAKE KWA SERIKALI YA TANZANIA

Muda mfupi baada ya Bodi ya MCC kutoa taarifa inayoonesha Tanzania haitapata msaada kutoka shirika hilo kama ilivyotarajiwa kwa ajili ya mwaka 2016, Mwenyekiti wa Chama (T), Freema Mbowe ametoa kauli nzito juu ya suala hilo akisema kuwa kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC.

MCC imeahirisha msada huo wa USD Mil. 472.8 ambazo ni takriban trilioni moja kwa fedha za Tanzania zilizolengwa kusaidia sekta ya nishati ya umeme hususan ule wa vijijini, katika kuunganisha wateja wapya, mabadiliko ya kimuundo ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ili lifanye kazi na kutoa huduma kwa ufanisi katika sehemu za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji.

Fedha hizo pia zilikusudiwa kusaidia kuanza kwa mpango mkubwa wa kuboresha sekta ya umeme nchini.2014-2024.

Mbowe amemtaka Rais John Magufuli kuchukua hatua za haraka za kiuongozi kumaliza mtanziko wa kisiasa Zanzibar kwa mshindi wa nafasi ya urais kutangazwa kutokana na uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu.

Aidha amesema kuwa Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ambayo ni mojawapo ya sababu zilizotumiwa na MCC kuahirisha msaada huo kwa Tanzania hadi itakapokuwa imefanyiwa kazi, ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano na kuzuia upashanaji wa habari miongoni mwa jamii ambayo ililenga kuweka makosa ya kijinai ili kudhibiti wapinzani wa CCM katika uchaguzi mkuu na kukipatia mazingira ya ushindi chama hicho.

"Sasa imethibitika kuwa Bodi ya MCC iliyokaa tarehe 16 Dec 2015 imeahirisha rasmi kuidhinisha msaada wa Millenium Challenge uliokuwa umekusudiwa kwa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2016. Sababu kuu mbili zilizosababisha uamuzi huo ni:

1. Mkwamo wa Uchaguzi wa Rais na Wawakilishi Zanzibar na
2.Matumizi mabaya ya she ria ya makosa ya mtandao hususan kuhusiana na uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa 2015."

"Ubabe wa baadhi ya viongozi wa CCM ni janga la Taifa. Kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC," amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza;

"Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano. Aidha, kwa makusudi kabisa inafifisha uhuru wa kupashana habari na ni dhahiri ilitungwa kwa nia mbaya ya kuthibiti kijinai uchaguzi mkuu."

"Tuliipinga sheria hii Bungeni na ikapitishwa usiku wa manane kwa ubabe wa wabunge wa CCM na hata tulipomtaka rais Kikwete asiisaini aliisaini kibabe akijua anaandaa mazingira gani ya "kihalifu", " amesema Mwenyekiti Mbowe.

Ameongeza kusema kuwa sheria hiyo ilitumika kuvamia vituo vya CHADEMA vilivyokuwa vikitumika kukusanya matokeo ya kura za rais na wabunge na hadi leo vijana zaidi ya 161, wakiwemo wanafunzi, wana kesi za "kubumba" mahakamani.

Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa Sheria hiyo hiyo ilitumika kuficha dhana ovu iliyotumika kuhalalisha kuvamia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilichokuwa kikiratibu watazamaji wa uchaguzi wa ndani kwa kibali cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

"Vile vile Sheria hii imetumika kuwakamata na kuwaweka ndani na hata kuwanyima dhamana vijana wetu ambao walituunga mkono katika uchaguzi mkuu."

"Namtaka rais Magufuli achukue hatua za kiuongozi na kiutawala kwa kufanya yafuatayo:"

"Kwanza aumalize mgogoro wa kisiasa Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa mshindi halali anatangazwa.

"Pili achukue hatua ya kuifanyia marekebisho makubwa Sheria ya makosa ya mtandao katika bunge lijalo. Aidha wale wote waliobambikiwa kesi amuamuru DPP kuzifuta kesi hizo mara moja," amesema.

Mwenyekiti Mbowe amesisitiza kuwa Rais Magufuli hana budi kuchukua hatua hizo za haraka ili kulinusuru taifa na hasara ya kupoteza mabilioni hayo ya MCC na zaidi kuepusha kuporomoka zaidi kwa biashara ya utalii nchini Zanzibar.

Amesema katika taifa ambalo sekta ya umeme inakabiliwa na matatizo makubwa katika uzalishaji, usambazaji na usafirishaji huku wananchi wa kipato cha chini wakibebeshwa mzigo mkubwa wa kumudu nishati hiyo na wengine wakilazimika kutumia nishati mbadala kama mkaa unaotokana na miti hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira, serikali inayojua wajibu wake yenye viongozi wanaothamini uwajibikaji, haikupaswa kushindwa kuchukua hatua stahiki kutimiza vigezo vya msaada huo ambao umeshaisaidia Tanzania katika miradi mingine kadhaa.

Imetolewa leo Ijumaa, Desemba 18, 2015 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Huyu mbowe ana AKILI NDOGO ZAIDI SANA, ndo maana alimwalika PAPA FISADI Kuimalisha chama,

Pole mbowe, naanza kuwa na wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri..

Ile kauli ya mchungaji msigwa ya kupimwa akili inakufaa sana..
 
Mkuu, mbona la kufanya mmeambiwa lkn hamtaki kusikia : uchaguzi zanzibar urudiwe. Kama hamtaki keep quiet.
 
Hivi nyie hamjachoka tu na kuwa omba omba ukizingatia utajiri tulionao???? Let's be positive and supportive to our president together we can. Just ask yourself how does mcc relate to internal matters? It's just another form of neo colonialism which we have to fight against. Obama alikuja bongo akacheza mpira pale ubungo na kelele zake za power Africa umeona chochote hadi leo?
hatutaweza hata tulikusanya 2tr kwa mwez.... hawa jamaa wana nguvu sana.... tulitakiwa tujipange kuondokana nao......
 
Habari za Mbowe tumeshazichoka umu, hatuna time na fisadi na muuza chama. Mods unganisha hii.

hiko cheo cha kuwasemea wengine nani amekupa?

jitetee nafsi yako na si kujidai unajua kila mtu anawaza nini.
 
Huyu mbowe ana AKILI NDOGO ZAIDI SANA, ndo maana alimwalika PAPA FISADI Kuimalisha chama,

Pole mbowe, naanza kuwa na wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri..

Ile kauli ya mchungaji msigwa ya kupimwa akili inakufaa sana..
Wa kwako ni mtindio wa ubongo kwa ajili ya bangi za Lumumba
 
Kwa hiyo comment nzima umeona kitu ambacho sio sahihi ni neno mkopo? Kwanini uchukie kutopewa fedha ambayo hujaivujia jasho fanyeni kaz hii ya kusubiria wahisani watoe ufurahie achana nayo mkuu karne sio hii
 
Akili za mbowe ni kama za muuza utumbo anabakia kupepea nzi badala ya kufuta mavi

Huwezi kutangaza mshindi kama kuna mgombea aliyevunja sheria ya uchaguzi na kujitangaza kuwa mshindi. Ni lazima uchaguzi urudiwe kwani umeharibika vibaya sana. Wamevunja sheria bado wanalaumu tu. Do the right thing at the right time. Go to polls.
 
Sasa imethibitika kuwa Bodi ya MCC iliyokaa tarehe 16 Dec 2015 imehairisha rasmi kuidhinisha msaada wa Millenium Challenge uliokuwa umekusudiwa kwa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2016.

Sababu kuu mbili zilizosababisha uamuzi huo ni:

1. Mkwamo wa Uchaguzi wa Rais na Wawakilishi Zanzibar na
2. Matumizi mabaya ya sheria ya makosa ya mtandao hususan kuhusiana na uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa 2015.

Kauli yangu juu ya jambo hili ni hii;

1. Ubabe wa baadhi ya viongozi wa CCM ni janga la Taifa. Kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC.

2. Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano. Aidha, kwa makisudi kabisa inafifisha uhuru wa kupashana habari na ni dhahiri ilitungwa kwa nia mbaya ya kuthibiti kijinai uchaguzi mkuu.

Tuliipinga sheria hii Bungeni na ikapitishwa usiku wa manane kwa ubabe wa wabunge wa CCM na hata tulipomtaka rais Kikwete asiisaini aliisaini kibabe akijua anaandaa mazingira gani ya "kihalifu".

Sheria hii ilitumika kuvamia vituo vyetu vya kukusanya matokeo ya kura za rais na wabunge na mpaka Leo vijana wetu zaidi ya 161 wana kesi za "kubumba" mahakamani.

Aidha Sheria hii ilitumika kuficha dhana ovu kuvamia kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC) waliokuwa wakikusanya matokeo ya kura za Rais .

Vile vile Sheria hii imetumika kuwakamata na kuwaweka ndani na hata kuwanyima dhamana vijana wetu ambao walituunga mkono katika uchaguzi mkuu.

Namtaka rais Magufuli achukue hatua za kiuongozi na kiutawala kwa kufanya yafuatayo:

1. Aumalize mgogoro wa kisiasa Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa mshindi halali anatangazwa .

2. Achukue hatua ya kuifanyia marekebisho makubwa Sheria ya makosa ya mtandao katika bunge lijalo. Aidha wale wote waliobambikiwa kesi amuamuru DPP kuzifuta kesi hizo Mara moja.

Hatua hizo zitalinusuru taifa na hasara ya kupoteza mabilioni hayo ya MCC na zaidi kuepusha kuporomoka zaidi kwa biashara ya Utalii nchini Zanzibar.

Huyu atuelezee fedha alizotorosha nje ya nchi huko China na Hong Kong asituletee porojo
 
Hata hivyo tumechoka na misaada yenye masharti wakae nao tu we can make on our own with 1.3 trillion Month. Kwa pamoja tukatae kushobokea weupe
Hiyo jeuli kwa sasa sahau hii ni nchi ya kimatonya daima
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, mbona la kufanya mmeambiwa lkn hamtaki kusikia : uchaguzi zanzibar urudiwe. Kama hamtaki keep quiet.

Urudiwe kwa sababu zipi ?! Kwamba unaamka asubuhi na kuamua uchaguzi urudiwe(that's a joke) . Kuwafurahisha CCM
 
Back
Top Bottom