Pre GE2025 Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'

Pre GE2025 Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Samia inabidi aondelewe. Haoni thamani ya maisha na uhai wa Watanganyika. Ngorongoro, , Loliondo, Misitu, DP World, tozo zimetuonesha hivyo.

Ila kuchukua nchi kunahitajika kuishirikisha nchii nzima. Unahitaji kiongozi wa kitaifa asiye na chuki na kabila, jamii, watu fulani. Mbowe ni mzuri akiendelea kuwa mwenyekiti wa Chadema na Tundu Lissu kama Mwanaharakati. Mwakubusi anaweza kupewa au Warioba, Shivji.
 
Nyumbu ni mnyama Jamii ya mamalia yani hali kitu chenye damu.. Kwamba hategei damu ya kiumbe hai imwagike ndio yeye aishi.. Yeye ni vegan.. Damu kwake mwiko!
LAKINI kuna mahali pakifika nyumbu huwa hahofii tena makucha wala meno makali ya carnivora yeyote yule awaye yote. hupambana na kupambania uhai wake!

Kampeni ya SAMY MUST GO! Ni dalili za kuchoka kwa Nyumbu kwenye kuonewa, kunyanyaswa, kutekwa kupotezwa na hata kuuliwa

Samy lazima
aende (aondoke mazima) ni dalili za wazi kwamba nyumbu kachoka na sasa anata kujilipua


Mdharau mwiba guu huota tende kama si tetanus na hatima yake ni kifo ( cha kujitakia)

Goof night Tanganyika (SMG)
Samia must go
Huyu mama alianza vizuri na mbwembwe za 4R na malidhiano
Kadri Muna unavyoenda anazidi kunogewa madaraka na wapambe wanamjaza upepo

Vijana wapuuzi wa idara nyeti wanamdanganya eti Kuna watu wanataka kupindua

Sasa basi liwalo na liwe,

tusipokufa kwenye maandamano, tukufa kwa kutekwa na kuteswana wasiojulikana

Tunajitoa muhanga
 
Mbowe akiwa kwenye mkutano wa waandishi uliohudhuriwa na wanachama wa CHADEMA asema wataanza na kampeni ya Samia Must Go ikiwa hakutakuwa na uwajibikaji kwenye matukio ya utekaji.

Mbowe pia ametoa rai kwa viongozi wa CHADEMA siku 12 kuanzia sasa kuja Dar kwaajili ya kupeana mikakati muhimu kwa hatua zaidi.

Soma Pia:

=====

"Kisiasa, n ani vyema mkasikia bunge la Tanzania, mwaka jana (2023) katika mabadiliko ya sheria ya usalama wa taifa ilipeleka usimamizi ya idara ya usalama wa taifa moja kwa moja Ikulu kusimamiwa na Rais, na sheria ile ilitoa kwa mara ya kwanza haki ya watu wa usalama wa taifa kukamata watu, kuwaweka kizuizini, bila kueleza mahali popote wala bila kushtakiwa.

"Sheria hii ilivyopitishwa Rais aliipitisha na akajimilikisha mamlaka ya usalama wa taifa. Sasa mimi kwa niaba ya CHADEMA na vikao na vikao vyangu, tuna declare mtu wa kwanza kuwajibishwa katika masuala hay ani Rais Samia Suluhu Hassan.

"Na sisi tunasema tunaanza moja kwa moja kampeni inayoitwa ‘Samia Must Go’, hiyo ndiyo rai yetu. Sasa basi, kwasababu bado tuna msiba, tumekubaliana kwamba tuna msiba kwasababu kuna viongozi wetu hatujui wako wapi. Kwahiyo sisi kama chama hatujamaliza msiba. Tutaendelea na msiba wetu kitaifa na bender azote za chama zitapeperushwa nusu mlingoti hadi tujue watu wetu wako wapi, wako hai au mauti

"Lingine, kuanzia siku ya Jumatatu, tar 23/9/2024 mkumbuke nilitangaza tar 21 tunategemea tuone hatua za watu kuwajibika zimeanza. Kama hawatachukuliana hatua wenyewe kwa wenyewe, sisi kuanzia tarehe 23 jiji lote la Dar es Salaam, kila kata kila mtaa.. ndugu zangu tumekuwa tunafanya utani mara nyingi, lakini kwa wakati huu hatuna utani.

"Kuanzia jumatatu sisi tutaingia barabarani kudai tunachoona ni uhai wa watu wetu waliopotenzwa unless serikali imechukua hatua za haraka na za makusudi kuwarejesha, watu kujiuzulu na watu wote kuwajibika kwa mujibu wa tamko letu la leo." -
Amesema Mbowe katika mkutano kwenye ofisi za CHADEMA, Mikocheni leo 11/9/2024

 
Watanzania tunayo aina yetu ya maisha ya kutatua mambo yetu kwa mazungumzo. Kwa msingi huo, kwenda kinyume ni kutafuta jinai na katika vitu ninavyoviheshimu kwenye nchi hii; ni kutokuchezea mamlaka ya Rais, amani, Uhuru na Usalama wa Nchi. Tusiige demokrasia isiyoendana na historia yetu. 🙏🙏🙏
Huu ujinga ulioandika ndio wanaoutumia kuteka na kuua watu wakiamini watanzania watatulia tu. Usisubiri yakukute ndio ujie umuhimu wa kuchukua hatua kama hizi.
 
Back
Top Bottom