Naamini sasa Mbowe anatakiwa kuleta umoja ndani ya Chama chake. Kwanza, alete maridhiano kwa kuwasamehe wale Wabunge 19 ili waweze kufanya siasa za kibunge huko Bungeni. Ukiwaangalia wale wamama unawaona kabisa wana damu ya CHADEMA ila hawafanyi siasa za kibunge na kiharakati kwa kuwa hawana uhakika na Chama chao. CHADEMA ikiwasamehe na kuleta maridhiano naamini watafanya siasa zenye manufaa kwa chama chao. Hivi kweli kabisa Halima Mdee, Kaboyoka, Paresso, Ester Matiko, nk hawana u CHADEMA miilini mwao? CHADEMA wakicheza wakaacha kufanya siasa za kibunge watakuwa wamefanya kosa kubwa.
Pili, Mbowe ana nafasi sasa ya kuleta siasa za kistaarabu hapa nchini kwa kujenga hoja za kisera, kuleta sera mbadala badala ya mihemko na matusi.Nilisikia akilisema hilo mbele ya Mh Rais. Naamini amegundua jinsi vijana wa chama chake walivyo na mihemko manake nimesikia akilitamka hilo kwa kinywa chake leo. Wakiendekeza na kuendeleza matusi watakuwa wanajitia kamba shingoni.