Pre GE2025 Mbowe: Nimetoka mbali na Lissu, nilikuwa namlipia tiketi za ndege kwenda Tarime kuwatetea wachimbaji madini

Pre GE2025 Mbowe: Nimetoka mbali na Lissu, nilikuwa namlipia tiketi za ndege kwenda Tarime kuwatetea wachimbaji madini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

View: https://www.youtube.com/watch?v=O6OAQjXmaXQ

Wapi hapa Mbowe kasema Lissu atachukuliwa hatua baada ya uchaguzi? Alichosema ni kuwa tatizo kubwa ndani ya Chadema ni ukosefu wa nidhamu. Ndio maana akasema uongozi utakaoingia itabidi uchukue hatua za kudhibiti hii hali bila kujali nafasi ya mhusika. Amesema hata kama yeye atashinda, Kamati Kuu mpya itakuwa na mamlaka ya kumchulia hatua kama itaona kuwa amehusika katika huo utovu wa nidhamu. Alipoulizwa kama atamchukulia hatua Lissu, alijibu kuwa huo utakuwa ni uamuzi wa Kamati Kuu na sio wa kwake. Hakusema mahali popote kuwa Lissu atachukuliwa hatua kwa sababu amemtukana. Huo ni uongo mtupu.

Amandla...

Umfahamu Mbowe wewe Lissu, ndiyo basi tena Chadema hata akishinda hawezi kupewa chama.
 
Back
Top Bottom