Pre GE2025 Mbowe: Nimetoka mbali na Lissu, nilikuwa namlipia tiketi za ndege kwenda Tarime kuwatetea wachimbaji madini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hiyo zilikuwa rushwa?
Mbowe angesoma tu alama za nyakati.
Awamu zote tulimuunga mkono lakini kwa sasa hapana,atuachie chama chetu au akomae kife abaki peke yake
 
Mbowe achia Uongozi acha mambo ya Prof Lipumba hayo kutaka kuongoza wewe tu miaka yote mambo unayoongea hayahusiani na kugombea Uongozi..
 
hata lisu kafanya mengi sana kwa mbowe, sema tu wewe ni limwinyi fulani huamini kama wenzio wana mchango kwako. halafu, haya yote yanayotokea ni kwa ajili ya kulinda uenyekiti tu? hutako kung'oka? ondoka mzee kabla haujaumbuka.
 
Hizi akili ni utumwa!! Hivi kweli hamuwezi kuonesha ukomavu wenu hadi mualike wageni?? Yaani ushujaa na ukomavu wako kwa mkeo uthibitishwe na majirani? Serious? Huku ndo kujitawala??
Wasimamizi wa uchaguzi hawaaminiki
 
“Nimetoka mbali na Lissu. Nilikuwa ninamlipia Lissu tiketi za ndege ninamgharamia safari zake kwenda Tarime kuwatetea wachimbaji Wadogo. Wakati huo hakua hata Mwanachama wa CHADEMA na nilikuwa nina mfadhili kwa mfuko wangu”.

Kwa hiyo mtu aliyefadhiliwa na Mbowe ndio anabanwa na katiba ya Chadema kutaka uongozi wa juu wa chama?
 
Kwa hivyo hizo zilikuwa fadhila za rushwa, tit for that, Lissu alihongwa ili asiwe huru kusema anachotaka?

Ajabu ni kwamba kuna watu hayo matamshi ya Mbowe wameona yanafaa kuwa uzi JF...
 
Nje ya mada, Kikeke kwenye hii interview na Mbowe, amepoa sana, no followup questions. Yeye ndio anamwelekeza Mbowe nini cha kujibu na kuelezea.
 
Alitaka Lissu amuogope na kumyenyekea...😱😱 hilo sahau Mangi Lissu sio Yericko kanjanja lako.

Na ukimfanyia Lissu ZENGWE chama kinakufia.
 
Hizi akili ni utumwa!! Hivi kweli hamuwezi kuonesha ukomavu wenu hadi mualike wageni?? Yaani ushujaa na ukomavu wako kwa mkeo uthibitishwe na majirani? Serious? Huku ndo kujitawala??

..huo ni uwazi, uadilifu, na kujiamini.

..Ni kuionyesha dunia kuwa uchaguzi wa Chadema ni huru, wa haki, na kuaminika.

..ningependekeza hata vyama vingine vya siasa viruhusiwe kuwa waangalizi wa uchaguzi wa Chadema.
 
Kuongea haya nikutaka kuonekana km hustahili kuachia kiti kisa umemsaidia mtu. Hili nalo ni tatzo mkubwa. Vyema ungeacha kusema haya kwa maana jamii na watu wako wa chadema wanaona kama hutaki kupata challenge kwenye umwenyekiti wako.
Ila namna njema ungesikiliza na kutafakari kundi kubwa la viongozi wemzako kimawazo nk ndipo ungeamua na sio kusema tu bado nahutajika bado kuna watu wananichukulia fomu hzo n mbinu za kuitwa nkurunziza aka kagame au mugabe, sultan au mfalme au ayatollah
 
Duuh ndo maana CCM hawakubali kuacha nchi
Kwa hizi mbanga zinavyopigwa unaweza kuona kuna kitu masisiemu yanakijua ndio maana hayataki kuachia nchi maana wapinzani wenyewe wako na pigo za kilanguzi wakikabidhiwa nchi itakuaje apo
 
Weka sauti tusikie, kama ni maneno Yako ni uzushi.
 
Aisee kumbe FAM ni mweupe jamani,yaani kumlipia mtu tiketi za ndege unataka asigombee au asiwe na haki ya kuchaguliwa
 
At least amekijenga(wamekijenga) kikawa bora zaidi ya vyama vingine vyote vya opposition otherwise kisingekuwa topic na battle ya mwenyekiti na makamu wake(iwe ni ya kweli au mbinu tu ya kuwa muda wote kwenye headlines) isingefuatiliwa kwa kiwango tunachokishuhudia.
Give credit where credit is due.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…