Mbowe: Niruhusuni kunyamaza

Mbowe: Niruhusuni kunyamaza

Leak
Nianze kwa kukupongeza kwa kuwa na shauku kubwa kusikia kutoka kwa mfungwa wa kisiasa Bwn Mbowe.

Pili acha nikujibu hivi;

Inashauriwa sana kama kiongozi au mtu mwenye hekima usiongee ukiwa na mihemko na hisia kali kama vile;
Hasira
Furaha.

Kuna hatari ya kuongea mambo magumu ambayo yanaweza kuondoa heshima yako.

Hata mawakili walishauri hadharani kuwa Mbowe asiongee kwasasa.

Ref: Mazungumzo ya Kibatala na waandishi wa habari.
Mh Mbowe amesema anaomba watu wamruhusu kunyamaza kwanza kwa kipindi hiki atakapo kuwa tayari atazungumza na taifa na watanzania kwa ujumla!

My opinion

Mbowe hawatendei haki wafuasi wake na watanzania ambao walimuombea usiku na mchana leo hii anawataka wampe muda wa kunyamaza?

Mbowe alitakiwa kuongea na watanzania kabla hata ya kuongea na Rais kwani watanzania walio wengi walitamani kuona Mbowe anakuwa wa kwanza kuongea nao na sio kuwaomba muda wa kunyamaza!

Mbowe sidhani kama ana sababu za msingi za kutoongea kwa sasa na sidhani kama kuongea na watanzania kwa sasa kungepunguza chochote! Ikiwa aliweza kuongea na Rais kwanini asiongee na watanzania?View attachment 2141158
 
Mbowe anahitaji muda. Usidhani anajua kila kitu kilichokuwa kinaendelea uraiani ni mpaka asimuliwe na kuhadithiwa na kusoma ili apate kujua si vyote ila vingi asije akaongea upumbavu.
namwamini mbowe kamanda mkuu ana akili sana ya siasa na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana hapa nchini.
ataongea vyema zaidi kama sasa atanyamaza .usidhani mbowe ni mjinga akurupuke bila kuongea na wasaidizi wake na watu wake wa karibu.
na ikulu alialikwa huwezi kwenda ikulu bila miadi hvyo kama raia mwingne unapoalikwa ikulu huna budi kuitikia wito hasa wa maongezi na si wa kula,
lakini hayo maongezi ya ikulu kamwe hayawezi kubadilisha msimamo wa mbowe hata wangemwambia ukiongea kuhusu katiba tunakukata ulimi.
usikute mama amemuomba akoleze kuhusu katiba maana katiba mpya ni nzuri kwa zanzibar kuliko kwa ccm sasa mama akiambiwa achague zanzibar au ccm atachagua ccm? Hapo ni sawa na kuchagua maji ya kunawa badala ya pilau.

Wengi watashangaa sana atakachoongea mbowe.
Mkumbuke lissu yuko mbioni kurudi. Hapo nchi itanoga na kuchangamka.
 
Hapa ndipo sifa ya nyumbu inapokuja.
Sio nyie mliosema mwamba hawezi kufika Bei?
Kipo wapi?
Mbona kanyamaza ghafla?

Sijui hata unaongea utoto gani, kanyamaza ghafla na ndio katoka jela wala hana 48hrs nje!
 
Vipi tume huru ya uchaguzi?
Kuna nchi hazina uchaguzi kabisa na zinafanya vizuri kuliko sisi katika nyanja zote.

Binafsi sijali, kuwe au kusiwe na tume huru. Itasaidia nini kukunyayua wewe maisha yako binafsi?

Tatizo kubwa, mmejazwa na kusomeshwa sana ujinga na mzungu mpaka umewajaa ndi ndi ndi, hamjijui kuwa mnajitafutia wenyewe mnyororo upi mzuri wa kujifunga nao zaidi na mnaugombania.

Damned if you do, damned if you don't.
 
Katika viumbe wasio eleweka ni nyumbu. Hawajui leo wamesema Nini Jana walisema Nini.
 
Mh Mbowe amesema anaomba watu wamruhusu kunyamaza kwanza kwa kipindi hiki atakapo kuwa tayari atazungumza na taifa na watanzania kwa ujumla!

My opinion

Mbowe hawatendei haki wafuasi wake na watanzania ambao walimuombea usiku na mchana leo hii anawataka wampe muda wa kunyamaza?

Mbowe alitakiwa kuongea na watanzania kabla hata ya kuongea na Rais kwani watanzania walio wengi walitamani kuona Mbowe anakuwa wa kwanza kuongea nao na sio kuwaomba muda wa kunyamaza!

Mbowe sidhani kama ana sababu za msingi za kutoongea kwa sasa na sidhani kama kuongea na watanzania kwa sasa kungepunguza chochote! Ikiwa aliweza kuongea na Rais kwanini asiongee na watanzania?View attachment 2141158
Kusamehewa tu mbio kwa Samia, Sasa hakuna Cha kuchangia wakili Wala Nini, kafanyeni kazi.
 
Nilitegemea Mbowe aseme wazi kuwa nimeongea na Rais kuhusu hiki na hiki na nimemwambia hiki na hiki na kwa kirefu nitasema baadae lakini kwa ufupi nimemwambia hiki na hiki!
Zipo video clips kwa hayo uyatakayo, uwe unapitia na YouTube, au vifurushi vya data za video vinakupiga chenga?

Kishasema kaenda kumshukuru Rais. Unataka nini zaidi?
 
CDM kina watu wengi wanajihisi ni special...mtu anamuita Mkuu wa Nchi eti "samia" hapo hapo anataka apewe attention yeye kuliko Rais ....juzi nikasikia wanamshambulia vikali Msigwa kisa kasema Ngongoro Inharibika...Yaani Chadema watapinga chochote ili mradi waonekane wanapinga...

Hivi Walikua na Uwezo wa Kumtoa Mbowe bila serikali kuondoa kesi?? Wana matatizo sana hawa jamaa
 
Hili ndilo tatizo la watanzania wengi wanahitaji kila mtu akisaidiwa alipe hapohapo kama mnaamini Mbowe katoka kwa Maombi yenu mnataka awalipe hapohapo?

Na nyie ndio wale ambao kila mkisaidia mnawaza kulipwa Kwa chochote au nyie ndio wale mkitaka kusaidia watu mnaitisha umati wa waandishi wa habari mutoe mulichonacho ili mukimaliza tu pale munaowasaidia wenye mahitaji wawapongeze na maneno mengiiii.

Mbowe yupo sahihi hili swala lilikua Zito sana sio lakutoka Mahakamani na kwenda kwa Press inatakiwa u Digest vitu na sio kila kitu akiseme.

#Taifa hili lina wajinga wengi sana.
Sentensi ya mwisho ina uzito mkubwa sana !!
 
Watanzania wengi hatuna akili za kujifanyia maendeeleo, tunapoteza muda mwingi kubishana Yanga na Simba.

CCM na Chadema tushaigeuza Yanga na Simba, tubishane tu, hatuna akili za kijifanyia ya maana.

Digital world imetutoa kwenye kubishana vijiweni imetuingiza kwenye kubishana viganjani. Kazi Iendelee.
 
Back
Top Bottom