Akihutubia Maelfu ya Wananchi huko Nkasi kwenye ile Oparesheni Kabambe inayoitwa Oparesheni 255 okoa Bandari zetu, Mwenyekiti wa Chadema, Feeman Mbowe, amesema Rais Samia haaminiki na ili tuamini kile kilichosainiwa jana alichodai ni mkataba wa bandari na DP WORLD ya Dubai basi mkataba huo uwekwe hadharani. Hii ni kwa sababu tunaweza kuwa tumepigwa (zilongwa mbali zitendwa mbali).
Awali Wananchi walimtaka Mbowe aombe nakala ya mkataba huo ili wauone na kujiridhisha kama kilichosemwa ndicho kilichoandikwa .