Nakumbuka mwaka 2011 nilikuwa Dodoma nikawa sijisikii vizuri kiafya. Nikaamua kwenda hospital moja binafsi maarufu kuchek afya yangu.Utaratibu gn ndugu saiv kariakoo hata barakoa watu hawavai wanajua corona imeisha lakini wakati huohuo katika mpk wa zambia na holili madereva wengi toka tanzania wanatest +ve huoni kuna kitu hakiko sawa ila kinafanywa kionekane ni normal
Baada ya kuonana na daktari akaniandikia vipimo nikaenda maabara
Majibu ya vipimo yalikuwa kama ifuatavyo
Nina malaria tatu
Mkojo mchafu na
Niliambiwa mapafu yangu yanaonekana yanashida "KUBWA"
Majibu mawili ya mwanzo wala hayakunishitua maana ni yakawaida na niliyategemea
Kilichonishitua ni ubovu wa mapafu! Nikamuuliza daktari, nimepimwa mkojo na damu tu majibu ya mapafu yamepimwa wapi?
Akaniambia wanapo test mkojo wana pima vitu vingi. Kwamba mkojo ulionekana una protini nyingi
Sikubishana nae, nikaweka kichwani. Nikaandikiwa dawa nyingi ambazo katika Maisha yangu sijawahi kuziona
Kwa vile nilikuwa natumai bima wala sikujali japo nilijua kabisa sitameza hata moja kwasababu nilishajenga mashaka
Baada ya pale nikaenda hospital ya mkoa. Nikajieleza vizuri kama nilivyojieleza kule mwanzo. Nikapimwa nikakutwa na Malaria tu.
Nikakaa kama wiki tatu nikaenda hospitali ya mkoa tena specifically kupima mapafu tu!
Nikajieleza kadiri nilivyoweza japo sikuhisi shida yoyote. Daktari akaanza kunidadisi. Ikabidi nimpe kisa cha wiki tatu nyuma ambacho ndicho kilichonijengea hofu
Akacheka kidogo Kisha akanipa shule na namna ya kushinda ushawishi katika private hospital hasa kipindi hicho ambapo kuna baadhi ya hospital madaktari walikuwa wanapewa target ya kuuza dawa.
Yaani daktari anayeuza dawa nyingi (kuandikia wagonjwa) alikuwa anapata bonus kwenye malipo
Kwanini hiki kisa nimekiweka kwenye comment yako?
Ni kwasababu umesema Madereva wetu wengi wakipimwa huko wana test positive positive wengi
Kumbuka Rais anamsimamo tofauti na karibu nchi zote zilizotuzunguka
Vikao vya kujadili corona tumewaachia. Mipango yao hatuijui na amesema hatuna haja ya kuijua
Kuna wakati tunatakiwa kuwaza tofauti kidogo
Sent using Jamii Forums mobile app