Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Utaratibu gn ndugu saiv kariakoo hata barakoa watu hawavai wanajua corona imeisha lakini wakati huohuo katika mpk wa zambia na holili madereva wengi toka tanzania wanatest +ve huoni kuna kitu hakiko sawa ila kinafanywa kionekane ni normal
Nakumbuka mwaka 2011 nilikuwa Dodoma nikawa sijisikii vizuri kiafya. Nikaamua kwenda hospital moja binafsi maarufu kuchek afya yangu.

Baada ya kuonana na daktari akaniandikia vipimo nikaenda maabara

Majibu ya vipimo yalikuwa kama ifuatavyo

Nina malaria tatu
Mkojo mchafu na
Niliambiwa mapafu yangu yanaonekana yanashida "KUBWA"

Majibu mawili ya mwanzo wala hayakunishitua maana ni yakawaida na niliyategemea

Kilichonishitua ni ubovu wa mapafu! Nikamuuliza daktari, nimepimwa mkojo na damu tu majibu ya mapafu yamepimwa wapi?

Akaniambia wanapo test mkojo wana pima vitu vingi. Kwamba mkojo ulionekana una protini nyingi

Sikubishana nae, nikaweka kichwani. Nikaandikiwa dawa nyingi ambazo katika Maisha yangu sijawahi kuziona

Kwa vile nilikuwa natumai bima wala sikujali japo nilijua kabisa sitameza hata moja kwasababu nilishajenga mashaka

Baada ya pale nikaenda hospital ya mkoa. Nikajieleza vizuri kama nilivyojieleza kule mwanzo. Nikapimwa nikakutwa na Malaria tu.

Nikakaa kama wiki tatu nikaenda hospitali ya mkoa tena specifically kupima mapafu tu!

Nikajieleza kadiri nilivyoweza japo sikuhisi shida yoyote. Daktari akaanza kunidadisi. Ikabidi nimpe kisa cha wiki tatu nyuma ambacho ndicho kilichonijengea hofu

Akacheka kidogo Kisha akanipa shule na namna ya kushinda ushawishi katika private hospital hasa kipindi hicho ambapo kuna baadhi ya hospital madaktari walikuwa wanapewa target ya kuuza dawa.

Yaani daktari anayeuza dawa nyingi (kuandikia wagonjwa) alikuwa anapata bonus kwenye malipo

Kwanini hiki kisa nimekiweka kwenye comment yako?

Ni kwasababu umesema Madereva wetu wengi wakipimwa huko wana test positive positive wengi

Kumbuka Rais anamsimamo tofauti na karibu nchi zote zilizotuzunguka

Vikao vya kujadili corona tumewaachia. Mipango yao hatuijui na amesema hatuna haja ya kuijua

Kuna wakati tunatakiwa kuwaza tofauti kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna nyuzi zikianzishwa tu,
u GT unatupiliwa mbali.

Alafu vinafuata vijembe vikali vya CCM dhidi ya CHADEMA and vice versa.

Ila nakiri kuwa navyo ni burudani ya aina yake.
 
Ndugu yangu mimi nimesoma ud nimemaliza 2006 lecture theatre hua tunajaa kuliko darsa la form one. Nakumbuka wakati mwengine ukichelewa ht kuingia huez.

Pili katika hostel zero distancing is equal to zero. Jamani tuwe na utu na tufikirie wengine pia
Sasa kama mtu yupo chuo kikuu na atashindwa kwendana na dharura ya Dunia atakufa kama wengine wanakufa. Watabaki ambao wapo makini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hilo la Covid 19 mheshimiwa Mbowe angekubali tu matokeo kwamba kazidiwa.Upamoja wa wananchi na raisi Magufuli katika hili ni ushahidi tosha kwamba Raia wapo pamoja na raisi wao.


Maadamu yeye mheshimiwa Mbowe alishalizungumza basi na aliache na hata km madhara yatakuwepo huko mbele atakuwa shujaa kwa sababu historia itamlinda.


Kwa yeye kuendelea kulisemea mara kwa mara italeta picha km analibeba hilo kama agenda ya kisiasa.
 
Tatizo ni uhaba wa taarifa, na tatizo kubwa zaidi ni dhana tunazo zijenga kutokana na taarifa haba.
Na hapa ndio kuna tatizo. Viongozi wanatuambia hali ni shwari na wagonjwa wamepungua huko mahospitalini. Hii ni habari nzuri lakini shida inakuja hamna takwimu rasmi ya idadi ya waliopona, waliofariki na rate ya maambukizi imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani.
 
Utaratibu gn ndugu saiv kariakoo hata barakoa watu hawavai wanajua corona imeisha lakini wakati huohuo katika mpk wa zambia na holili madereva wengi toka tanzania wanatest +ve huoni kuna kitu hakiko sawa ila kinafanywa kionekane ni normal
Hata wewe ukipimwa utatest positive, Ila hautaumwa.
Na hii itakuwa kwa wengi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hawaruhusu kama unavyofikiria wewe kuna utaratibu maalum utakao zingatiwa wa kitaalam utakaofatwa.
corona haishi leo wala kesho ni lazima maisha yaendelee huku kukiwa na tahadhari kubwa.

magufuli anaanzisha ila hamini nakwambia kuna nchi nyingi tu zita fuata,


Sent using Jamii Forums mobile app
lakini kauliza maswali ya msingi: Je ni kweli kuwa vipimo vyetu ni feki?????
 
Kwa mujibu wa Raisi kacorona kanaenda kwisha wiki ijayo
Hivyo vifo mnavyovisikia ni matatizo ya Hofu tu
Shule zifunguliwe na Michezo irejee ili Watanzania waburudike
 
Nimejaribu kujizuia nimeshindwa.

Tanzania inaenda kuangamia kwa kukosa maarifa.

nilikuwa nasubiri nipewe ripoti ya mashine za kupimia ambapo kila takwimu zilizokuwa zinatoka ugonjwa ulikuwa unaongezeka maradufu.

tujiulize km wagonjwa wamepungua je tulipima wangapi na kwa mashine zipi?

Tunaomba viongozi watuambie sisi wananchi je ripoti ya ukaguzi ya mashine imetoka?

na wakaanza kupima tena lini?

najiuliza sipati majib pale mashabiki watakapojazana viwanjani, wanafunzi maskulini na wageni kuingia bila karantini hii ni jambo la kustia mno.


salaam.
Chief

Samahani sana

Tunaomba usemee kwako,Tz si yako wala si ya Familia yako

Tz ni ya wa Tz wote



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hapa ndio kuna tatizo. Viongozi wanatuambia hali ni shwari na wagonjwa wamepungua huko mahospitalini. Hii ni habari nzuri lakini shida inakuja hamna takwimu rasmi ya idadi ya waliopona, waliofariki na rate ya maambukizi imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani.
anzia kwenye ukoo wako kupata hizo takwimu au na ukoo wako mnafichana ? vipi kwenye ukoo wenu mna takwimu rasmi ya idadi ya waliopona, waliofariki na rate ya maambukizi imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani.?
hebu zimwage hapa hizo hazihitaji serikali tupe wewe
 


Akizungumza na taifa Leo hii, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na kiongozi wa upinzani bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe amemfafanua vizuri Spika wa Bunge kuwa ni MTU wa aina gani.
Akizungumza kwa upole mkubwa, unyenyekevu na weledi wa hali ya juu ameeleza vituko na udhalilishaji ufanywao na Ndugai kama vile gubu la ukewenza.
Hakika Mbowe utulivu usio na chuki umewashangaza wengi kwani utadhani hakuna jambo baya hata moja kesha wahi kutendewa yeye na chama chake.
Tupende tukatae, Mbowe ni kiongozi. Tena kiongozi adimu kupata kutokea katika zama hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Za Kuambiwa Changanya na Za Kwako!
 
hawaruhusu kama unavyofikiria wewe kuna utaratibu maalum utakao zingatiwa wa kitaalam utakaofatwa.
corona haishi leo wala kesho ni lazima maisha yaendelee huku kukiwa na tahadhari kubwa.

magufuli anaanzisha ila hamini nakwambia kuna nchi nyingi tu zita fuata,


Sent using Jamii Forums mobile app
hana lolote kasikia mabeberu wanaongelea kufungua na yeye anataka kufungua wakati hata mashine mbovu inayopima mapapai positive hajaibadirisha intubators hana na hata mpango mkakati w kitaifa wa kupambana na janga hana
 
Trend imetokea wapi?? Usiulize..trend ipi wakati VIPIMIO VYA VIPIMO VINAPIMWA??

Nilichogundua ukiwa Mr Politishiani, unakuwa pathological liar...

Everyday is Saturday........................ 😎
 
anzia kwenye ukoo wako kupata hizo takwimu au na ukoo wako mnafichana ? vipi kwenye ukoo wenu mna takwimu rasmi ya idadi ya waliopona, waliofariki na rate ya maambukizi imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani.?
hebu zimwage hapa hizo hazihitaji serikali tupe wewe
ukishaona watu wenye vichwa vya samaki ndio kama nyie kwenye ukoo wake atashindwa kupata takwimu tunaongelea uzembe wa kiongozi anayefurahia majanga alianza kwenye watu wa mafuriko kahama akaenda wale tetemeko Kagera akaja waliozama na vifusi kahama wale wamaporomoko upareni kote huko yeye anaona ndio makafara yake hata kwa corona ajabu ya kweli anaichororesha nchi hii watu wanadhani sote tunatoka kuzimu
 
tapeli wa taifa, muongo muongo na mnafiki. Inaonekana jinsi alivyoshindwa kumudu uenyekiti wake. Dkt Magufuli si wa kumpinga, ukimpinga tegemea kupata kipigo toka kwa Mungu.
Mungu yupi??acha utani
 
Back
Top Bottom