Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Tanzania imefika hapa kwasababu kura ya mwananchi haina thamani tena.Watawala wana uwezo wa kuiba kura jinsi watakavyo.
Baada ya kugundua kuwa tumeibiwa kura, je, tumechukua hatua gani? Tumebaki kulialia na kulalamika kwenye mitandao na kuwalaumu viongozi wa siasa.

Wengi humu ni majasiri tukiwa nyuma ya keyboards basi. Zaidi ya hapo hakuna kitu.
 
Tanzania imefika hapa kwasababu kura ya mwananchi haina thamani tena.Watawala wana uwezo wa kuiba kura jinsi watakavyo.

Ww ndio umesema kila kitu, iwapo kura haiheshimiwi tusitegemee chochote toka wahuni wanaoingia madarakani watakavyo. Kila siku nasema bila machafuko tusitegemee lolote la maana.
 
Wakiandamana wakapigwa virungu risasi na kuuawa huwa mnawatukana na kuwaita vibaraka WA mabeberu ,
Umbwa nyie Acha myooshwe Tu ,Mbowe akae atulie ,waTanzania ni umbwa Koko
Kila mtu apambane na Hali yake
Mbona mtusi mkuu! Ukumbuke haya ni mawazo tu
 
Wewe ndiye mwenye maono sahihi. Mbowe Hana jeshi .la kumsaidia zaidi ya support toka kwetu wananchi lkn tupo tu kama mazuzu. Mbowe wa watu anafika mahali anachoka
Kuwasaidia wabongo ni kazi sana,mtu anajitolea lakini anaowasaidia wala hawana habari na ndio waimba pambio, za kusifu na kuabudu huku wanateketea
 
Kuwasaidia wabongo ni kazi sana,mtu anajitolea lakini anaowasaidia wala hawana habari na ndio waimba pambio, za kusifu na kuabudu huku wanateketea
Amejitoleaje wakati ndio kazi yake aliyoichagua
 
Ni kweli kuwa wananchi ni waoga ila siamini kama Chadema inaweza fanya jambo lolote la maana katika Taifa letu kwa sasa.

Chadema imeshindwa kufanya lolote ilipokuwa ya moto kwa sasa viongozi wake wakuu wamejichokea na kukata tamaa.

Haya ndio matamanio ya kila mwanaccm kuwa CDM ichoke. Cha ajabu CDM wakiongea vyombo vya dola ambavyo kimsingi ndio CCM vinajitokeza kuilinda ccm!
 
Ni ununuzi wa magari, matengenezo na mafuta Kwa pamoja..

Aliyekwambia kwamba hizo pesa zote hutumika kununua magari na Kwa muktadha huu V8 ni nani?

Huu ni uzushi wa kina Mbowe sawa tuu na waliosema sensa imetunika bil.600 wakati ni bil.400 sawa na sh.6200 kwa kila mtu..

..inaelekea una taarifa sahihi za ndani.

..gharama za kununua ma-V8 kila mwaka ni kiasi gani?
 
Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
 
Is why tuko hapa. Kutoka hamuwezi sababu mmetishiwa virungu, na hili wameshalijua kwahiyo wanajua hamna namna zaid ya social media.
Tusifanye maandamano kuwa ndio hitaji letu tukumbuke kuwa maandamano ni moja tu ya njia ya kuonesha hisia zetu hivyo mimi naamini zipo njia zengine pia za kuonesha hisia zetu tusijifunge na maandamano tu.
 
Ndiyo na kandambili iliyokatika kipande kwa kuchanwa na gwambara. Kavaa tshirt na kofia yenye picha ya mwanamme/mwanamke mwenzake
Unadhani kama upinzani siku wakiamua nao kugawa kofia wapiga kura wa upinzani wataongezeka?
 
Sisi tupo bize na mpira hasa Simba na Yanga. Mambo ya nchi tumewaachia CCM na Mboye.

Japo inasemwa Mboye kalambishwa asali, lakini angalau anaonekana kuwaaamsha Watanzania ambao miaka nenda rudi tumelala usingizi mzito.

Nawashauri CCM wakitaka kuwazubaisha zaidi Watanzania wafanye hivi, wajenge viwanja vya mpira vya kisasa kila mkoa, halafu Simba na Yanga wawe wanachezea kwenye hivi viwanja kwa mzunguko, na serikali itoe kodi kwenye viingilio viwe bei chini kabisa, hakika wananchi watafurahi hata kama hawana wanalala na njaa!
 
Back
Top Bottom