..Zanzibar wakati wa Karume waliwahi kuwa na mkuu wa polisi [ edington kissasi] ana asili ya Uchagani. Je, hiyo nayo utasema ni ukabila?
..Kukusaidia tu, Wachaga ni kati ya makabila ya kwanza kutoka ktk maeneo yao ya asili na kusambaa Tanzania nzima kutafuta fursa.
..Sijui kama unamkumbuka Waziri mmoja mwanamama akiitwa Shamsa Selengia Mwangunga. Yule mama asili yake ni Uchagani, wazazi wake walilowea Dodoma na siasa alikuwa akifanyia huko.
..Mtanzania kama huyo unaweza vipi kumbagua asishiriki siasa ktk eneo alilokulia? Na ukimbagua kwenye siasa utaishia hapo au utambagua ktk fursa nyingine?
..Mwisho, Wachaga hawachagui mahali pa kuishi. Wachaga hawajitengi. Pia ni wameoleana na jamii nyingi hapa nchini. Huo ndio UTANZANIA.