Mbuge Flatei Massay apiga sarakasi Bungeni kuonesha kulalamika kuhusu ahadi anazopewa kila mara bila kutekelezwa, afanya marejeo ya sauti za mawaziri

Mbuge Flatei Massay apiga sarakasi Bungeni kuonesha kulalamika kuhusu ahadi anazopewa kila mara bila kutekelezwa, afanya marejeo ya sauti za mawaziri

Mbuge wa Mbulu ameoneshwa kukerwa hadi kuamua kupiga sarakasi bungeni bila kujali uwepo wa spika

Ni sawa mmbuge kupiga sarakasi au mweleka kuonesha kukerwa na ahadi zizizo tekelezeka?

===

Kuruka sarakasi kwa mbunge Flatei ni jambo analotamani kulifanya mara nyingi, Mei 17, 2021 pia alipokuwa akilalamikia matatizo ya jimboni kwake aliomba kuruka sarakasi ili kuonesha kuwa ametumwa na wananchi wake kuwasemea.

Kabla ya kuruka sarakasi, Mbunge huyo wa Mbulu alifanya marejeo kwenye kishkwambi chake ya sauti zilizorekodiwa za waziri wa ujenzi na naibu wake wakitoa ahadi kwenye vikao vya Bunge vilivyopita za kukamilisha ujenzi wa barabara Mbulu jambo ambalo halijatimizwa hadi sasa.

Pia soma:Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay almanusura kupiga sarakasi Bungeni ili ajengewe barabara jimboni

images (4).jpg
 
Hahahahaha sijawahi kulifuatilia hili bunge ila leo nimesoma hii habari na nimecheka sana
Nalog off Z
 
Watu wengine bhana cjui mkoje, Ety mnasema hajielewi. Sasa mlitaka afanye jambo gani ili serikali imuelewe.? Mbona chadema walikuwa wanatoka nje huku kikao cha bunge kinaendelea, je tuseme nao hawana nidhamu mbele ya bunge.?
 
je wakiwa kama 50 wote wapige sarakasi bungeni?
 
Sarakasi zina uhusiano gani na hoja aliyotakakuwasilisha?
 
Back
Top Bottom