Mbunge Anne Kilango: Serikali ina Pesa, Madiwani waongezewe Posho

Mbunge Anne Kilango: Serikali ina Pesa, Madiwani waongezewe Posho

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mbunge wa Jimbo la Same mashariki, Anne Kilango Malecela akichangia Bajetia Kuu ya Serikali 2026/2027 Bungeni leo Juni 2026, ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuboresha maslahi na posho za madiwani nchini.

"Nimwombe Rais Samia kwa unyenyekevu, kwa hali ilivyo sasa, ni vyema serikali ikawaangalia waheshimiwa madiwani. Kwa sababu bajeti imeboreka sana, serikali ina pesa. Waheshimiwa madiwani, mheshimiwa Rais namwomba, serikali naiomba, ni vyema ikawaangalia waheshimiwa madiwani sasa.

Mheshimiwa mwenyekiti, mimi ni mbunge wa jimbo. Ukweli niseme ukweli waheshimiwa wabunge, nashindwa kufanya kazi mwenyewe jimboni kwangu, nafanya kazi na madiwani. Sina uwezo wa kuingia kata zote, wenzangu wako kwenye zile kata zao. Lakini mwenyekiti mkisema ukweli, waheshimiwa madiwani posho zao ni ndogo mno."

"
 
Back
Top Bottom