Mbunge awachana bungeni wanaodai hajaolewa

Sasa hapo wajinga ni hao wahuni au wajinga ni wananchi ?
Kwa Umoja wetu wengi wetu ni wajinga..... Mtu anaona kabisa hiki sio sawa ...lakini Kwa kulinda tumbo na kusubiri teuzi anajivalisha mawani ya mbao...... Wengine mpaka maofisini tumeshapewa majina mabaya na pande tumechaguliwa .... Nchi ya hovyo sana.... Uchawa, unafiki, undumilakuwili ndio umetamalaki....
 
Tufanye nini ili kuondokana na ujinga?
 
bunge la shujaa wako alilowaachia?
Nyerere aliwaachia UJAMAA/KUJITEGEMEA na AZIMIO la Arusha wakaua vyote.

Iweje washindwe kuua bunge la mtu aliyekufa ?

Acha kujitoa ufahamu bwashee, hilo ni bunge pendwa la mama Abdul lipo kwa maslahi ya wezi na mafisadi na sio kwa maslahi ya wananchi.
 
Simkubali Mama Abdul , ila kwenye huu upuuzi mtamuonea kabisa engineers wa ule upuuzi wa October 28 , 2020 ni Jiwe , wakurugenzi na vyombo vya ulinzi na usalama vyote na mitandao ya simu.

Waliokuwepo Tanzania walikiri hata jumuiya za kimataifa na waangalizi wa uchaguzi walikiri irregularities kubwa kuwahi tokea tangu chaguzi za vyama vingi .

Unaitaje uchaguzi watu wanaingia vituo vya kupigia kura na mabegi yaliyojaa kura zilizopigwa tayari na mawakala wa vyama vya upinzani wakikamatwa siku moja kabla na wengine siku yenyewe ya tukio.

Hii iko documented Magufuli hasafishiki kwa hilo tukio la October 28, 2020.
 
Aliolewa akaachika . Kwahiyo ni divorced
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…