Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakuu
Mbunge wa Jimbo la Ushetu (CCM), Emmanuel Peter Cherehani, akiwa katika ziara yake Kata ya Chambo Oktoba 7, 2026, aliulizwa na mwananchi kuhusu lini mchakato wa kupata Katiba Mpya yenye demokrasia utaanza. Katika ziara hiyo, pia alizindua Zahanati ya Kijiji cha Nyawishi na kutembelea pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo.
Ni lini tutaanza kujadili mfumo wa Katiba Mpya yenye demokrasia na inayowaendeleza Watanzania wote?
Akijibu, alisema Katiba ni karatasi tu na haileti chakula au maendeleo bila mtu kufanya kazi na kujenga uchumi wake.
"Katiba itakuambia barabara ikikamilika itengeneze? Katiba itakufanya upate bidhaa nyumbani? Swala la Katiba ni karatasi! Lakini kikubwa kila mmoja atengeneze maisha na uchumi wake. Kuna nchi zimebadilisha Katiba mara elfu, lakini zinafanya nini?"
"Majirani zetu wengi wamebadilisha Katiba zao, lakini Katiba bila kwenda shambani utakula? Katiba bila kufungua mlango wa duka la dawa utakula? Mimi sitalajii kama Katiba inaweza kubadilisha maisha. Na Katiba iliyopo ni ile ile..."