Mbunge haoni umuhimu wa quadratic equation na periodic table

Mbunge haoni umuhimu wa quadratic equation na periodic table

Acha janja janja za ki-JF za ujuaji mwingi lakini uhalisia ni sifuri! Mjibu huyo "ng'ombe" wewe zimekusaidia nini!!
Kwa Sisi engineers we know zinapotusaidia wewe kama hazikusaidii jiunge na ng'ombe wenzio
 
Hivi huyo mbunge mpumbavu jina lake ni nani ?😁😁😁😁 suti na tai ajijamsitiri na upumbavu wake ni kama hijabu tu ....hijabu wanavaa na upumbavu wanao
Yuko sahihi sana.
Hayo mambo sisi tunajifunza kujariri tu lakini hatuna matumizi nayo kwenye maisha ya kawaida.
Kila kitu tunaagiza nje ya nchi hadi mifagio ya ndani inatoka China,quadratic equation ya nini?
Makandarasi wetu wakikujengea barabara,utadhani wote darasa la saba.
Wakemia,wafamasia na wanasayansi wetu hawawezi hata kutengeneza ethanol,ethanol yote inatoka China na ulaya wakati wao wakiweka sheria ya kudhibiti wanaotengeneza gongo ( ethanol) wakiwa hawajui lolote kuhusiana na periodic table.
Bado tuna ujinga mwingi sana tunahitajika kubadili namna ya kufikiri na kuona mambo
 
Sawa, wewe umesaidiwa nini na hiyo Quadratic Equation na Periodic Table? Si unauza genge wewe pale Kariakoo?
Wewe unadhani hata ingredients za maji safi ya chupa zinawekwaje bila kujua periodic table, ukafahamu molecular mass nk kwaajili ya kichanganya.
Unatumia maji safi, juice,madawa, ukiugua unatundikiwa maji, sabuni unatumia na Bado hauoni umuhimu wa kuifahamu periodic table??
 
Kwa Sisi engineers we know zinapotusaidia wewe kama hazikusaidii jiunge na ng'ombe wenzio
Kuandika "kwa sisi engineers we know zinapotusaidia..." ni kauli au tungo inayoweza kusemwa/kuandikwa na yeyote yule, hata mshona viatu ili mradi anaweza kuandika!
 
Yuko sahihi sana.
Hayo mambo sisi tunajifunza kujariri tu lakini hatuna matumizi nayo kwenye maisha ya kawaida.
Kila kitu tunaagiza nje ya nchi hadi mifagio ya ndani inatoka China,quadratic equation ya nini?
Makandarasi wetu wakikujengea barabara,utadhani wote darasa la saba.
Wakemia,wafamasia na wanasayansi wetu hawawezi hata kutengeneza ethanol,ethanol yote inatoka China na ulaya wakati wao wakiweka sheria ya kudhibiti wanaotengeneza gongo ( ethanol) wakiwa hawajui lolote kuhusiana na periodic table.
Bado tuna ujinga mwingi sana tunahitajika kubadili namna ya kufikiri na kuona mambo
Mkuu waza upya izo kazi mbovu unazosema ni kwasabu hatusomi ivi vitu vya kutosha kama kupunguza tungegusa kwenye lugha, history ,masomo ya dini ila sio physics, chemistry l,bios, geography na mathematics pamoja na civics huu ndo msingi wa maendeleo yetu
Ukibaki na mtazamo huo utasema digestion system imekusaidia nini kwenye maisha sasa
Huezi sema quadratic imekusaidia nini na kila cku unatumia magari ,yanapita kwny madaraja,unataka simu iko edged,kana kipato kinaruhusu unapanda ndege,kuna jeshi linakulinda wanasiraha za kulenga shabaha
 
Kuandika "kwa sisi engineers we know zinapotusaidia..." ni kauli au tungo inayoweza kusemwa/kuandikwa na yeyote yule, hata mshona viatu ili mradi anaweza kuandika!
Ukisoma engineering yoyote kuna semester nne unasoma advanced mathematics for engineers kwasabu lazima utazitumia
 
Kwahio alitaka watu wasome Chemistry na wafundishwe kushona na kusuka nywele kwenye Chemistry wakati kuna masomo yanayofundisha hicho kitu ?; Kwa ufupi tu faida ya Periodic Table wala uhitaji kujifunza bali kufahamu ilipo na kuangalia kama vile ilivyo kwa Multiplication Table

Periodic Table; is important for various applications. It helps scientists analyze reactivity, predict chemical reactions, and understand trends in element properties, such as electronegativity, ionization energy, and atomic radius.

Huwezi kujua hilo kwenye somo la PE (Physical Education); Kila kitu kina sehemu yake, na ubongo sio one dimensional hata ukijifunza kila kitu huwezi kuujaza...
 
Nimesikitika sana! Nimepitia posts karibu zote lakini ukitoa posts za Kiranga na Shotocan, wengine wote wamebaki kuponda tu na angalau wawili miongoni mwao wao wamefikia hadi kuingiza upumbavu wa udini lakini bado wameshindwa kutuambia akina sie tuliosoma arts umuhimu wa hao akina quadratic equations ingawaje binafsi naitumia tumia kidogo kwenye research! Inaonesha wengi tupo au mpo sawa na huyo mzee, yaani hamjui lakini kwavile JF kila mtu ni msomi na tajiri anaye-drive Range, ndo lazima tuponde ili tuonekane sisi tunajua!!

Acheni janja janja, tuambieni umuhimu wa quadratic questions na msifanye tu assumption kwamba yana umuhimu mkubwa vinginevyo yasingefundishwa bali kuweni real, na nyie mnaoponda hapa HAMJUI umuhimu wake! Hata huyo Mzee angetaka kujifanya ujuaji kama nyie wala asingesema hayo, tena kuwajaza tu angeweza hata kusema kwanini quadratic questions zisianze kufundishwa tangu darasa la kwanza!! Kwanza nikijiondoa kwenye kundi la wanafiki, nampongeza huyo mzee kwa sababu kuna baadhi ya post nimeona zikisema amewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi! Sasa mkizingatia hata nyie wenyewe hamjui, hivi hamuogopi kuona hata aliyewahi kuwa mtu mzito serikalini na mwenyewe hajui?! Na kwa kuzingatia majority hamjui hata tumizi moja (heri yangu mara moja moja naitumia kwenye research ingawaje hii ni more than quadratic equations- ukweli nimesahau zinaitwaje, manake nilifundishwa tu in a crash programme ili niweze kuzitumia lakini zinafanana na quadratic) hivi hapo tatizo ni huyo mzee aliyeweka wazi kwamba hajui au ni mfano halisi wa matatizo ya mfumo wetu wa elimu?!
Sasa hilo ndo tatizo wewe unatumia kwenye research yeye waziri kwamba alikua anakuta hesabu za kutoa na kujumlisha tu? Kwa mujibu wake izo mambo watu wakajifunze wenyewe badala ya serikali kuwekea mkazo Zaid watu wengi wajue unazani ni sawa hii?
Sipo kwenye kundi wasio jua faida zake lakini ata ningekua sijui nisengewaza mtu ashauli zitolewe yani apo katumia akili za kitoto za olevel kysema math ngumu ,log ngumu lakini angalia yeye anaongea wap yuko bungeni ambapo kama akiungwa mkono maana ake wanaeza ata kulifuta somo la math nchini unaxan ni sahihi?
Kuna ujinga unaendelea sana apa nchini watu wanakwambia veta kuna ujuzi kuliko chuo wanasahau veta ni course za engineering zs ngazi ya chini ndo izo level 2 level 3 fikilia civil ndo mafundi ujenzi, electronics ndo mafundi simu, electrical ndo mafundi umeme, mechanical ndo mafundi gerage na mitambo, interior design na architect ndo mafundi mapambo ya nyumba.
Nije kwa field yangu nnayo ijua electronics kuna tofauti kubwa ya fundi wa veta na mtu aliesoma electronics chuo kuanzia kwenye ubora wa kazi ad utibuji wa tatzo kama huamini nenda kwa fundi wa mtaani kisha nenda kkoo tafta fundi kasoma electronics au computer engineering ndo utajua
 
Kwahio alitaka watu wasome Chemistry na wafundishwe kushona na kusuka nywele kwenye Chemistry wakati kuna masomo yanayofundisha hicho kitu ?; Kwa ufupi tu faida ya Periodic Table wala uhitaji kujifunza bali kufahamu ulipo na kuangalia kama vile ilivyo kwa Multiplication Table

Periodic Table; is important for various applications. It helps scientists analyze reactivity, predict chemical reactions, and understand trends in element properties, such as electronegativity, ionization energy, and atomic radius.

Huwezi kujua hilo kwenye somo la PE (Physical Education); Kila kitu kina sehemu yake, na ubongo sio one dimensional hata ukijifunza kila kitu huwezi kuujaza...
Kweli kabisa
 
Habari wakuu,
Ni aibu kuwa na mbunge kama huyu haoni umuhimu wa periodic table kisha baadae utamkuta anasifia mama ameleta soko la madini kuna kila sababu ya kufanya reform kabla ya uchaguzi watu waache kupachikana kwenye nafasi tu

Hawa "wabunge" mambo mengine ni vyema wayadadisi kwanza kabla ya kuzungumza hadharani.
 
Siku huyu mzee wangu akijua kuwa kuna hesabu za calculus atapigana bungeni huyu

Sasa bila periodic table unaisomaje hiyo chemistry..??
Wacha wadhungu waendelee kutuonya manyani tuu...
 
jamani taratibu. Huyu ni Mtu mkubwa sana. Ni Mstaafu Waziri Kiongozi wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Huyu ni Mhe, Shamsi Vuai Nahodha. alishautaka na urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (a.k.a urais wa Tanganyika).
 
Back
Top Bottom