Mbunge haoni umuhimu wa quadratic equation na periodic table

Kumbe ni muislamu basi ni sawasawa kumiliki akili kama hizo.....mtu awezi kuwa muislamu na akawa na akili
Wewe ulisoma wapi!
Asad alikuwa dini gani?
Magufuli alikuwa dini gani?
 
Sasa hilo ndo tatizo wewe unatumia kwenye research yeye waziri kwamba alikua anakuta hesabu za kutoa na kujumlisha tu? Kwa mujibu wake izo mambo watu wakajifunze wenyewe badala ya serikali kuwekea mkazo Zaid watu wengi wajue unazani ni sawa hii?
Yeye amezungumzia ngazi za chini, na ukweli mchungu ndo huo ngazi za chini elimu yetu ni kama kokoro; ni mwendo wa kuzoa zoa tu kana kwamba tunafanya majaribio ya kujua nani atafahamu nini kati ya haya tutakayowafundishwa! Lakini pamoja na hayo, hoja yangu ya msingi sio hiyo ni jinsi watu wanavyoponda hapa lakini ukweli ni kwamba hata hao wanaoponda wala hawajui hizo quadratic equations zinatumika kwenye nini kwa sababu na wenyewa walisombwa sombwa tu na mfumo wa ovyo wa elimu!
Sidhani kama kuna anayesema VETA kuna ujuzi kuliko chuo lakini ukweli ni kwamba, huku mtaani ni Wahitimu wa VETA ndio wanatumika sana kuliko hao ma-engineer! Bila shala ukifanya survey unaweza kukuta katika kila nyumba 10 unazopita basi angalau moja ina changamoto inayomhitaji fundi lakini fundi huyu sio Engineer bali yule wa levels za VETA! Mimi mwenyewe hapa feni yangu mbovu! Do I need an engineer? Hapana, bali Mwamba wa VETA au "Fundi Maiko"!
Chifu, hakuna mwenye akili timamu anayeweza ku-ignore Wataalamu wa Jambo Fulani lakini tatizo watu tunapenda sana kuchukulia mambo out of context! Issue ni kwamba, sio kila tatizo ni la kupeleka kwa mtu mwenye digrii! Hata wewe ukijisikia homa hapo hauendi Muhimbili waliko specialties bali utaenda kizahanani cha jirani ambacho unajua kabisa huenda waliopo hapo hata diploma hawana!! Hivi leo hii nyumba yangu ina shot ndo nitafute Electrical Engineer?! Wapo walio kwenye huo mfumo lakini majority wanafanya maamuzi kutokana na ukubwa pamoja na unyeti wa tatizo!
 
Hebu mtuambie hizo hata mimi nimezisoma na sijawahi kuzitumia na wala kuona zikitumika....
zaidi ya kujibia mitihani....
 
Siku huyu mzee wangu akijua kuwa kuna hesabu za calculus atapigana bungeni huyu

Sasa bila periodic table unaisomaje hiyo chemistry..??
hizo ulitumia kujibia mtihani tu
wapi hapa bongo zinatumika kazini...
 
wewe mlugaluga hebu acha kelele...
vyote ulivyotaja havijawahi kutumika na wala havitumiki huku bongonyoso,
 
Ni huyu tu mtanzania mmoja ambae anaweza kusema zimemsaidia...na ni mmoja kati ya millioni 60 na haishi bongo....
Wengine muende VETA, hizo table na equation mnalazimisha na kuishia kuwa wanasayansi uchwara wa kugombania mwendokasi na wadangaji......

 
Yupo sahihi lakini CCM kawaida ina wabunge uchwara ila kwa hili hajakosea. Hata wewe jiulize, hiyo Quadric Equation na Periodic Table imekusaidia nini maishani.
Daktari akikuandikia dawa na kusema hakuna side effects, huku inserts zikionesha kuna heavy metals,. Kama unajua periodic table, na kuelewa reactivity series na atomic masses za hizo elements unaweza mwambia daktari anywe mwenyewe. Ila kama hujui utabugia tuu, matokeo yake baadae unapata autoimmune disease bila kujua ugonjwa umetoka wapi.
 
Chukulia una eneo la mita za mraba 48 unataka kuligawa kwa urefu wa mita mbili zaidi ya upana. Kwa kutumia quadratic equations unaweza kupata suluhisho la urefu wa mita sita kwa mita nane.
 
Mpaka hapo Jimbo lake lishakula hasara maana lazima halina umeme, Wala maji
 
Kheee...!! Hajui au haoni umuhimu wa periodic table...!!!
Nimpe kitu kimoja tu kwenye gas production.
1. Anajua maana ya sacrificial anode kwenye cathodic protection???
2. Anajua kwamba metals gani zikikaa karibu au kugusana na metal ipi, nyingine inapata corrosion??
3. Anajuaje inert gases zinazotumika kuondoa gas kama methane wakati pipe inayobeba methane gas inapotaka kufanyiwa matengenezo?
 
He is just surviving in this world
 
Aisee, moja ya kigezo cha kuwa Mbunge ni kujua kusoma na kuandika.
Lakini pia tunaambiwa Bunge ni chombo cha kutunga Sheria yaani watu wanaojua kusoma na kuandika tu wanaweza kukaa chini na kutungia Sheria Watanzania milioni 60 na zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…