Mbunge Jerry Silaa hajui kitu kuhusu ATCL, asijifanye mjuaji

Eti sisi ni familia tuliyoishi ktk mambo ya ndege! hahahaaaaaaaaaaaaa! kweli ushamba ukizidi ni hasara! baba kuwa rubani pekee ktk familia imekuwa nongwa!
 
Hizo ndege ziuzeni tuondokane na makelele,mbona tulishawaambia kwamba miradi yote aloanzisha Hayati Magufuli iliyokamilika ama iuzwe au ivunjwevunjwe na na ile ambayo haijakamilika iachwe isiendelezwe ili muanzishe miradi mipya ya kwenu yenye tija kwa taifa
 
Marekani wamejenga vingi vingine ndo wakaja kwenye hizo NASA za anasa unazozungumzia! Yaana Mtu hana kodi ya nyumba unamwambia anunue hummer, kisa NASA, NASA pori!
We mtu Shirika la Ndege si anasa, ni la lazima. Niambie nchi gani duniani haina shirika lake la ndege? Ukiona nchi inayumba kwenye vitu kama shirika la ndege kuna mawili, either ni failed state au si nchi huru.
 
Hiyo nisaidie kimoyo moyo! Kwakua mwenye misimamo uliyo kua unaamini ni dhabiti, amekua mwendazake na kwa kua taifa litaelekea kwingine, karibu tujenge nchi kwa positive criticism!
Kama huwezi thibitisha madai yako basi uwe unakaa kimya. Kuzusha ni dhambi.
 
Imeanza kubackfire? Records za JPM hamtazifuta kwa genge lenu uchwara kutoka msoga
 
Kama huwezi thibitisha madai yako basi uwe unakaa kimya. Kuzusha ni dhambi.
Sawa mkuu, lakini kutokua Mkweli kwa nafsi yako inaweza kua unafiki ambao nao ni dhambi pia! Ila pamoja kubadilika msimamo wako, kuna mambo yako ya zamani yalikujengea heshima kubwa kwangu, nimeshindwa kuacha heshima hiyo! Najua kuna utopolo ambao, penda usipende utapinga tu, Nyani!
 
Duh!

Hivi unaongelea nini wewe? Au umelewa?

Hueleweki!!!!
 
Bila shaka wewe utakuwa ni zuzu, zezeta na hujitambui!!
Yaani unataka kulinganisha NASA na ATCL? Shame in you! Hizi akili za kichatochato hizi hatutaki kuzusikia kabisa....!!!
Yaani unakaa miaka 6 hujaongezwa mshahara unaona fahari na unashangilia ati ni SACRIFICE? Nonsense. Hivi unajua maana ya ku- sacrifice au unaji ropokea tu?? Yaani Jiwe alikuwa anaumiza Watumishi kwa kununua ndege ZINAZO TENGEZA HASARA YA BILIONI 60 TSHS??? Nenda kapimwe Mirembe Mental Hospital kwanza ndipo urudi hapa!!!
Very likely you're not an employee of any government entity!! Are you?
 
We mtu Shirika la Ndege si anasa, ni la lazima. Niambie nchi gani duniani haina shirika lake la ndege? Ukiona nchi inayumba kwenye vitu kama shirika la ndege kuna mawili, either ni failed state au si nchi huru.
Sipingi shirika la ndege, lakini kazi ya uendeshaji wa mashirika siyo ya serikali! Shirika letu la ndege ni la kwetu tu, hata likendeshwa na sekta binafsi! Serikali yake kodi, alafu kusimamia usalama wa watu na mali zao!
 
muhusika wa yote kishatangulia mbele za haki.
😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳
 
Mimi nadhani kuwa na ndege jambo zuri ila kwa maoni yangu tungejikita na hizi ndege ndogo low budget airline kwa ajili ya safari za ndani tu kuchochea uchumi wa ndani, Hatukuwa na haja ya kwenda kununua Boeng au Airbus sababu kubwa ni kwamba, msafiri yoyote anapenda kuja na ndege ambayo ana uhakika na connection na kumrudisha anakotoka kwa wakati sasa ndege kama EK au Qat na zingine kama Ethiopia zinatosha kutuletea watalii wa kutosha na kama wamezidi hata wao watazidisha routes. Ndio maana unaona wanatua mpaka Kilimanjaro siku hizi Qatar, Ethiopia.... sisi network yetu sio kama ndogo tu ila hatuna kabisa kwenda China na India haileti tija au Comoro. Mtu akija kutoka Comoro labda anaenda France hawezi kuja Dar sababu connection hatuna labda akapande kina EK. Hawa Dubai au Ethiopia wanaenda kila sehemu wanakuleta kwao hapo unaunganishwa kwenda unakotaka sisi hatuna uwezo huo tulitakiwa kujikita na safari za ndani na ndio Airport zetu zinapokea ndege ndogo sio unapeleka Airbus Mwanza tunalipa Tsh haileti maana. Naunga mkono ndege lakini ndege za ndani kwa sasa na hakuna kutoka korosho wala maji panda ndege one hour umefika save money.
 
Miradi yeyote ya serikali yeyote Duniani huwa haina faida. Mfano Tanroads kwa mwaka huu imeingiza faida kiasi gani? Kwa km za bara bara zilizojengwa kwa kutumia mabilioni ya pesa umeshawahi kusikia wamepata faida? Kama hawapati faida, Tanroads ifungwe? Muhimbili tangu ianzishwe imeshawahi zalisha faida kiasi gani? Kama haizalishi faida ifungwe? Hii ni mifano michache.
Ndio maana hizi huduma na bidhaa zinaingia kwenye public goods. And gvt has to invest on market failures. Market failure ni pale huduma au bidhaa inayohitajika kwenye uchumi lakini bidhaa hiyo haiwezi kuzalishwa na nguvu ya soko.
Hii inatokana na either bidhaa hiyo kutokuwa na faida kibiashara au kuhitajika kwa mtaji mkubwa sana ili kuweza kuzalisha bidhaa hiyo. Kwa hiyo kwa kuwa hakuna private entity inayoweza kuzalisha public goods, gvt intervention ndio inakuwa suluhisho. Mf ujenzi wa reli ni gharama kubwa hivyo kusababisha market failure, huduma za ulinzi na usalama ni gharama kubwa kiasi kwamba huwezi kuwaambia KK security walinde nchi na wewe uwalipe ndio maana kuna market failure.
kuelewa zaidi public goods nawashauri msome welfare economics.
 
Ama kweli mtu yeyote ni mzuri HADI afungue kinywa chake.
 
Wewe tumia akili kuelewa kilichoandikwa udikurupuke kujibu tu. Kinachozungumzwa hapa ni aina ya shirika ambalo linalotia taifa hasara badala ya kua na mpango kazi wa kuliimarisha, pato lenyewe bado ni dogo inakimbilia kununua madege yanakutia hasara miaka 10 mfululizo na kiuchumi uko hoi, hivi hiyo ni akili?
Huyo akili hana zinamtoshea kuvukia barabara na kwenda chooni. Huyu hakua hata kazi inayofanywa na NASA, aliyemwambia NASA ni kampuni ya kibiashara ni nani? Basi kama ni hivyo Mamalake yetu ya hali ya hewa TMA nayo iwe inazalisha. Taifa hili tuna watu wapumbavu sijawahi kuona.

ATCL ni shirika lilisajiliwa kibiashara, linatakiwa kujiendeshe kwa faida. Eti linatoa huduma ndio maana linapata hasara, akaulize pale basi za Mwendokasi zinazotoa huduma kama UDART hawapati faida.
 
TANROADS wamesajiliwa BRELA kufanya biashara? Huwezi kufananisha TANROADS na ATCL
 

Ficha ujinga wako wew unaanzaje kufananisha uwekezaji wa kwene ndege kuwa ni sawa na kule wa barabara? eti ni public good kwaiyo ni sawa kupata hasara...huwez kuwa siriaz wew🤔kadanganye watoto wenzako huko.
 
Mbunge Jerry slaa kazia hapo hapo
 
Acha upuuzi wa kuongelea mashirika ya umma kama kampuni za wahindi.Shirika la ndege hata likiingiza hasara faida zake huonekana katika sekta nyinginezo kama utalii na madini pamoja na kutoa huduma kwa wananchi pamoja na safari za rais.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Jeri yupo sahihi. Wewe ndio mwehu. Muhimu ni kuwa na deni tunalolimudu. Ila kama unategemea ile kampuni isiwe na deni kabisa basi Wewe sahau.

Na ndege hatuziuzi . Mjipange kivingine kama hamuelewei.
Tubadilike,
Watz twatakiwa kujiruhusu kufanya mijadala yenye misingi ya kitaalamu itakayowezesha hoja za kitaalamu kutufikisha pazuri.
Tuepukane na waliorithishwa ubishi kama wa 'inzi' anaeng'ang'ania mzoga mpaka kuzikwa nao.
 
Usiniletee stress zako za kimaskini. Nimekupa mfano NASA ni shirika la taifa la Marekani na halizalishi faida yoyote lakini bado linaendelea kusupportiwa. Vivyo hivyo ATCL ni shirika la taifa la Tanzania, kama halijaanza kuzalisha faida yoyote siyo sababu ya kutoendelea kusupportiwa. Lengo la uwepo wa ATCL ni zaidi ya kuzalisha faida ya moja kwa moja.

Sijashangilia kutopandishiwa mishahara miaka sita, ila kuna matakataka wanaofikiri ni bora kupandisha mishahara ya wafanyakazi kuliko kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati. Mnailalamikia serikali kwamba inatoza kodi kwa mkono wa chuma, na kwamba inawanyonya wafanyabiashara kupitia kodi, halafu wakati huo huo unataka kodi hizo hizo zitumike kwenye kuongeza mishahara ya wafanyakazi. Kodi za wananchi lazima ziwafaidishe wananchi wote, si wafanyakazi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…