Mbunge Jerry Silaa hajui kitu kuhusu ATCL, asijifanye mjuaji

Baba ake Jerry anamiliki ndege iliyomuua Filikunjombe

Jerry anajua sana maswala ya ndege!
NDEGE ILIYOMUUA BABA YAKE JERRY NA FILIKUNJOMBE ILIKUWA NI HELICOPTER!!! SASA JERRY ANAJUA MASWALA YA NDEGE ZIPI?

MAMBO YA UENDESHAJI WA BIASHARA YA NDEGE NI MTAMBUKA , YANAHUSU TARANSPORT ECONOMICS, MARKETING, ENGNEERING, ACCOUNTING, HUMAN ADMINISTRATION KWAHIYO NI BIASHARA INAYOHITAJI WELEDI WA HALI YA JUU NA SIO KUIENDESHA KAMA BIASHARA YA DALA DALA!!
 
Jerry Slaa ni puppet
Yuko nyuma ya watu..
Akiongea Bashe ujue Rostam kaongea
Kuna wabunge huwa wanaongea Kwa niaba ya wengine...
Watu wakubwa kama kina Kinana.Lowasa.
Kikwete na wengine Wana wabunge wao
Wanazungumza kwa niaba yao..
Haya ni maneno mazito ya ukweli.
 
 
Umemsema Jerry Slaa hajui kitu kuhusu ATCL wakati wewe mwenyewe umeonesha ndio MAAMUMA kabisa!
 
Prof Abbas alieleza vizuri kabisa hata Sisi ambao siyo wachumi tumemuelewa. Tatizo watu wana pick maneno kwenye paragraph na Kuya twist.

According to Abbas, Kilichotakiwa kufanyika ni kuliquidate ATCL, then pesa inayopatikana inawaliipa creditors then unakuwa ni mwisho wa deni. Baada ya kufanya hivyo unaanzisha kampeni nyingine ambayo itakuwa free na madeni. South Africa kwa Sasa wako kwenye hiyo process...!!
 
Nilitaka kujua iwapo ana ABC za airlines, sio darasa la kwanza afu anabwabwaja.
 
Baba yake alikuwa Rubani basi anajiona tayari yeye ni Mtaalam wa kila kitu kwny ndege kuanzia Engine, Kapeti za ndege hadi mfumo mzima wa baishara

Watoto wa 'Fundi Garage' hujifanya wanajua kila kitu kwny Magari
Kukaa karibu na mahakama siyo kujua sheria... Kasahau hii
 
Jinsi ulivyoanza na mbwembwe za kumkosoa Slaa nilitegemea nikute nondo za uhakika za kutetea hoja yako. Nimeishia njiani baada ya kuona blah blah,bora hata Jerry Slaa maelezo yake yana logic.
Anzia na hili... COVID19 imekuja mwaka 2019, lakini ndege zimepiga hasara kwa miaka mitano mfululizo... YAANI HATA KABLA YA COVID19...
 
Sasa mkupishana mawazo na wenzenu mnakashfu, mnataka mfanane mawazo? Activist wa JF mna chekesha
 
Ndege zinunuliwe fullstop.
 
Lakini hawa wakaguzi wetu wawe wanatujulisha pia hiyo Loss inavyokuwa calculated. siku zote financial statements usipojua kuzifafanua huwezi elewa.Kuna wakati statements zinaonyesha shirika linapata faida na bado linafirisika.

Wewe hujiulizi kwa nini mashirika yote makubwa duniani ya ndege yana declare loss lakini bado yapo sokoni na ndege zao zinaendelea kuruka wala hujasikia hata siku moja wameshindwa kulipa mishahara ya uendeshaji.

Finacial statements ni "fictious" zinatumia standards ambazo zimejaa estimates na judgements.

Unajua pia,kuna kitu kinaitwa uchakvu,nazo huwa ni gharama ,ijapo hakuna cashoutflow

Nadhani mijadala kama hii inahitaji watalaamu wa mambo ya uhasibu,siyo kuwaachia wanasiasa.tukiwaachia wanasiasa watatupotosha kwa maslahi yao binafsi.

Kwa upande wangu siwezi ku-hemka kwa taarifa kama hiyo iliyo ya upande mmoja.mpaka nipate taarifa zote mhimu,1) faida na hasara 2)mizania 3)mtiririko wa fedha taslimu,4)taarifa ya madiliko ya mtaji. Uhai wa shirika unaangaliwa kwa vigezo zaid ya faida tuu. pia sera za shirika katika katika uhasibu na utoaji taarifa za fedha.

Huwezi kuanza biashara kubwa kama hiyo ukapata faida ndani ya muda mfupi
 
Mbona wewe ndiyo mpitoshaji usiyejitambua. Slaa hujulinganishi naye kaa kimya
 
Wala hujui jinga wewe labda unajua biashara ya bar ndio ujuzi wako. Mijitu kama lissu ni ya ovyo mtu huwezi kubishana nayo maana ni confident fools. Jerry slaa ametoa maelezo utadhani mtaalamu wa biashara ya usafiri wa wanga halafu jitu linabisha tu kwa unyumbu...aaaaaagh yaani hii minyumbu ni balaa.
 
Niliona Ndugu gai na genge lake wakimshangilia...
 
We nae ni chakubanga tu huna lolote,sasa hapo wewe unajua nini? Acha kujidai kumbe ni debe tupu!
 
Baba yake alikuwa Rubani basi anajiona tayari yeye ni Mtaalam wa kila kitu kwny ndege kuanzia Engine, Kapeti za ndege hadi mfumo mzima wa baishara

Watoto wa 'Fundi Garage' hujifanya wanajua kila kitu kwny Magari
Acha wivu na majungu!
 
Jerry Slaa ni puppet
Yuko nyuma ya watu..
Akiongea Bashe ujue Rostam kaongea
Kuna wabunge huwa wanaongea Kwa niaba ya wengine...
Watu wakubwa kama kina Kinana.Lowasa.
Kikwete na wengine Wana wabunge wao
Wanazungumza kwa niaba yao..
Hebu tupe list ya wabunge wa Rostam, Kikwete na Lowasa tuanzie hapa kwanza,usilete umbea na majungu hapa,kama huna ushahidi basi hustahili hata kulike chochote humu maana utakuwa umedhihirisha ufinyu wako wa akili!
 
Mimi kinachonishangaza bungeni,ni kama wanaipinga Ripoti ya CAG waziwazi kwa kisingizio cha hotuba ya Mbowe ambayo inaonekana kuwavuruga!
 
Hebu tutajie hizo spin off effects ambazo tunapata kutoka ATCL? Hao NASA wenyewe wanatumia rockets za Space X kupeleka Astronauts wake angani.

Kinachogomba hapa kwetu ni hiyo haja ya kuwa na midege yetu wenyewe ambayo inatutoza nauli kubwa wakati yalikuwepo mashirika yakitoa huduma hiyo hiyo kwa bei nafuu. Hao watalii walioongezeka waliletwa na mashirika ya ndege ya kimataifa bila sisi kuingia gharama yeyote isipokuwa kuvuta ada wanazotulipa kutumia anga na facilities zetu. Na kama tunadhani hao watalii watakimbilia ATCL na kuacha KLM, Emirates, Turkish Airlines n.k. tunajidanganya.
Wamarekani pamoja na mihela yao hawana shirika la taifa la ndege. British Airways inamilikiwa na IAG, kampuni ambayo imekuwa registered Spain na inamiliki Iberia na Aer Lingus.

Sisi tungewaachia wenye uzoefu watoe hiyo huduma ya usafiri wa anga na hivyo vihela vyetu tungevitumia kuboresha maisha ya wananchi wetu. Usafirishaji wowote ni biashara, sio huduma.

Amandla....
 
Halafu hawa watetezi wanayumba sana, hawana kauri moja: wengine wanasema ATCL inafanya BIASHARA na hasara mwanzo wa biashara ni kawaida baadae tutapata faida.
, wengine wanasema inafanya kutoa HUDUMA tu hivyo tusiihesabie hasara kwani mashirika yote ya ndege duniani yanaendeshwa kwa hasara lakini yanahudumia sector zingine zipate faida.

Je, ni:
BIASHARA?
HUDUMA?

Najua wataendelea kuyumbisha mpira anga hizi huku wakiendelea kuropoka.
[emoji3][emoji3]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…