Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?

Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?

Bunge la Tanzania halafu ndani ya Bunge hilo yupo mbunge ambaye anakana wazi wazi kuwa yeye siyo raia wa Tanzania. Na hii taarifa inaingia kwenye hansard. Na hao viongozi wa nchi wanamchekea tu huyu bwege. Hii ni hatari

Tunaelekea kwenye "state of anarchyc wallah
Asante ndugu yangu kwa kuliona hilo. Hawa viongozi wa Bunge kwa kweli wajipime
 
View attachment 2991526

Mbunge anasema na au anakana kwamba yeye si Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Mtanzania”.

Sasa Humo Bungeni anafanya nini?

Hatuna Nchi inayoitwa Zanzibar wala nchi ya Tanganyika. Tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “ Tanzania”

Sasa kama yeye ni Mzanzibar na hatuna nchi hiyo, humo ndani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya nini? Kiti cha Speaker kingefaa kimtoe nje pale pale kwa kauli yake mwenyewe kwamba hapokei taarifa ya yeye ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kiti cha Speaker mumepwaya sana maana, Hatuna dual nationality, tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtu anasema na anakana kwamba yeye sio Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Principle of legal estoppel), sasa kwa nini aendelee kuwemo humo Bungeni?
Hatuna dual nationality, hakuna raia wa Burundi, Rwanda au nchi ya “Zanzibar” anayeweza kuwemo Humo Bungeni.

Ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee anayeweza kukaa humo, vinginevyo ni magumashi tu, bila chenga chenga na mkosi ni Mkosi tu- Haijalishi unatokea wapi.

Povu ruksa bila Matusi.
Wote humo ndani ni raia wa Tanzania na wanaapa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wapate haki ya kukaa humo ukumbini.

Hayo mengine yote ni muendelezo tu na matakwa ya demokrasia kwa mapana yake.
 
Huyo mbunge naye kiazi kabisa.
Yaani anasema viongozi wa Tanzania wanaotokea Zanzibar wanabaguliwa, halafu hapo hapo anaambiwa yeye ajitambulishe kama mtanzania ili asibaguliwe anakataa kata kata, anang'ang'ania tu kuwa yeye ni Mzanzibar na sio mtanzania!!
 
Back
Top Bottom