Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo ni maajabu ya Musa na Speaker/kaimu speaker akakaa kimya tu.Huyo mbunge naye kiazi kabisa.
Yaani anasema viongozi wa Tanzania wanaotokea Zanzibar wanabaguliwa, halafu hapo hapo anaambiwa yeye ajitambulishe kama mtanzania ili asibaguliwe anakataa kata kata, anang'ang'ania tu kuwa yeye ni Mzanzibar na sio mtanzania!!
Hisia tu za maongezi yake lakini wote humo ni watanzania.Mbona amekana na speaker akakaa kimya?
Anajua anachofanya Bosi angekuwa Magu angthubutu?!View attachment 2991526
Mbunge anasema na au anakana kwamba yeye si Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Mtanzania”.
Sasa Humo Bungeni anafanya nini?
Hatuna Nchi inayoitwa Zanzibar wala nchi ya Tanganyika. Tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “ Tanzania”
Sasa kama yeye ni Mzanzibar na hatuna nchi hiyo, humo ndani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya nini? Kiti cha Speaker kingefaa kimtoe nje pale pale kwa kauli yake mwenyewe kwamba hapokei taarifa ya yeye ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kiti cha Speaker mumepwaya sana maana, Hatuna dual nationality, tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtu anasema na anakana kwamba yeye sio Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Principle of legal estoppel), sasa kwa nini aendelee kuwemo humo Bungeni?
Hatuna dual nationality, hakuna raia wa Burundi, Rwanda au nchi ya “Zanzibar” anayeweza kuwemo Humo Bungeni.
Ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee anayeweza kukaa humo, vinginevyo ni magumashi tu, bila chenga chenga na mkosi ni Mkosi tu- Haijalishi unatokea wapi.
Povu ruksa bila Matusi.
Kwamba yeye siyo 'MTanzania'?Unadhani hayuko sahihi 😂😂
Yanachekesha ssan lo
Yeye ni Mzanzibari kwanza utanzania ni subset.Kwamba yeye siyo 'MTanzania'?
Wewe unadhani yupo sahihi?
Naanza kuwa tofauti na wewe kidogo.Hii mbegu wamaepianda Wazanzibar kwasababu ile ile aliyosema Nyerere '' Sisi ni Wazanzibar wao ni Watanganyika''
Ukishajitambulisha kwa Uzanzibar huwezi kukwepa Utanganyika. Ukishaondoa Zanzibar huwezi kuwa na Tanzania
Ni Wazanzibar hawa akina Jussa, Othman, Duni wanataja 'Tanganyika'' wanaosema Watanganyika ni Wapumbavu wamelala kama huyu Mbunge wa watu 3,338 wa ACT Wazalendo anayesema tutumie passport.
Ukisoma mandhari ndani ya Taasisi za nchi hata hapo Bungeni Watanganyika wakiwemo wa CCM wamechoka.
Tunahitaji Tanganyika tu kama watahitaji Muungano wataomba wao, Watanganyika hawana cha kupoteza!
JokaKuu Pascal Mayalla @
Tukienda kwenye hesabu, mimi nitakupeleka kwenye AI (Artificial Intelligence), sasa sijui kama hapo tutaelewana.Yeye ni Mzanzibari kwanza utanzania ni subset.
Kama umesoma hesabu za set utamuelewa.
Ndio maana tunasema huu Muungano una utata sana
Serikali moja ipi hiyo ambayo itabaki kati ya hizi za sasa mbili? Na lini hiyo serikali moja itauliwa na kubaki na hiyo moja?Naanza kuwa tofauti na wewe kidogo.
Hatuwezi kuvunja muungano kwa sababu ya kikundi hiki kidogo ambacho tunajua historia yake toka muungano uwepo. Huu utakuwa ni ujinga wa hali ya juu sana.
Muungano utaendelea. Serikali itabaki kuwa moja tu. Acha hiki kikundi kiendelee kupiga kelele huko huko kwenye serikali moja.
Hiki kikundi kimepewa fursa, kilipoanza kupenyeza mambo yake ya "KERO" zisizokuwa na mwisho; na kwa ujinga wa CCM wakadhani kitaishia hapo. Sasa wamejitokeza mbele kabisa kwa ujasiri wote, kudai wao ni Wazanzibari, na siyo waTanzania!
Unaweza kuwa Mtanzania lakini usiwe MzanzibarKwamba yeye siyo 'MTanzania'?
Wewe unadhani yupo sahihi?
Mbona unajichanganya mwenyewe?Unaweza kuwa Mtanzania lakini usiwe Mzanzibar
Ndio sababu yeye anajivunia Uzanzibar wake
Yupo sahihi kwa sababu hajawahi Kuomba uraia wa Tanzania amekutana nao kwa mujibu wa katiba 😀
Mbona ni suala ambalo lipo wazi.Tukienda kwenye hesabu, mimi nitakupeleka kwenye AI (Artificial Intelligence), sasa sijui kama hapo tutaelewana.
Hili ni jambo jepesi tu, achana na 'subsets' hizo ambazo hazimo katika uraia wa nchi yoyote. Just be straight, on point.
Ukitaka 'upupu na ujinga' kama unavyo sema utaupata sana hapa, kwani umejaa tele ukitaka hivyo.Serikali moja ipi hiyo ambayo itabaki kati ya hizi za sasa mbili? Na lini hiyo serikali moja itauliwa na kubaki na hiyo moja?
Unless otherwise umekoment upupu na ujinga ambao huuelewu
Huo ni upumbavu uliovumiliwa miaka mingi. Haina maana hauwezi kukomeshwa.Mbona ni suala ambalo lipo wazi.
Mzanzibar ni mzanzibari kwanza na mtanzania kama chaguo la pili.
Kule Zanzibar kuna kazi zinatangazwa ukiomba hizi kazi unatakiwa uambatishe kitambulisho cha ukaazi wa zanzibar hawahitaji cheti cha nida unafikiria ni kwa nini.
Ili kuwa Rais wa Zanzibar unatakiwa uwe mzanzibari ukiwa Mtanzania tu huna sifa za kugombea uraisi wa Zanzibar
Yupo sahihi yeye ni Mzanzibari ndio maana anaweza kumiliki ardhi zanzibar bila masharti yeyote kama ambayo anapewa Mtanzania asiyekuwa Mzanzibari.Kwamba yeye siyo 'MTanzania'?
Wewe unadhani yupo sahihi?
Yeye kazaliwa nchi ya ZanzibarMbona unajichanganya mwenyewe?
Analo gamba (Pasipoti) aliyoomba yeye mwenyewe. Ni lini kila raia huomba uraia wa nchi aliyozaliwa, aliyokuta wazazi wake ni raia wa nchi hiyo?
Huo ni upumbavu uliovumiliwa miaka mingi. Haina maana hauwezi kukomeshwa.
Ni jambo jema tunapata mitazamo tofauti. Na wala usihofu mkuu, kuwa critical na simamia hoja unayoiamini.Naanza kuwa tofauti na wewe kidogo.
Tatizo kikundi hicho kimepewa 'umuhimu sana' kama kwamba Wazanzibar ni Raia wa daraja la I.Hatuwezi kuvunja muungano kwa sababu ya kikundi hiki kidogo ambacho tunajua historia yake toka muungano uwepo. Huu utakuwa ni ujinga wa hali ya juu sana.
Wazanzibar hawataki na huyo anayeongea au wanaoongea wana 'Baraka'.Muungano utaendelea. Serikali itabaki kuwa moja tu. Acha hiki kikundi kiendelee kupiga kelele huko huko kwenye serikali moja.
Anayetoa fursa hiyo ndiye anayefumbia macho ! Unachoita kikundi kilimshawishi alete KERO ya bili ya umeme ya Bilioni 60 kwa Watanganyika. Yaani imefika mahali hata bili za umeme tunalipa!! ni kwa 'return gani' huo ni muungano gani. Tunaungana kwa 'give and take'' . Tushawishi kwa sasa tunapata nini.Hiki kikundi kimepewa fursa, kilipoanza kupenyeza mambo yake ya "KERO" zisizokuwa na mwisho; na kwa ujinga wa CCM wakadhani kitaishia hapo. Sasa wamejitokeza mbele kabisa kwa ujasiri wote, kudai wao ni Wazanzibari, na siyo waTanzania!