Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?

Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?

Angalau ameonyesha muhimu wa Kwa nini Zanzibar wana Bunge lao lisilo na Watanganyika huko Zanzibar, alafu Bunge la Muungano wa Tanzania ambalo na yeye yumo lipo, ila ajabu kabisa haoni Bunge la Watanganyika,na kweli halipo, na wakati Watanganyika wakienda huko Zanzibar wanapaswa kutambuliwa kama Watanganyika kwenye hizo passport anazoomba ziwepo, otherwise zikisoma Utanzania Bila Utanganyika itamlazimu akuhoji mbona na Mimi Ni Mtanzania!. Je Ni kweli Tanganyika inaona aibu kujitokeza kiutawala?

Wazee wengine Wa Tanganyika mlikuwepo Msizeeke na Akili zenu! Ajabu hata Documents, za Muungano zinazoonyesha Kuungana, Migogoro na Usuluhishi, Hatima na Uvunwjaji wa Muungano!
These are realm in real world, hazipaswi eti kutokuwepo kisa Muungano hautavunjika.
Kama hautavunjika, Vunjeni governance and borders za Uzanzibar.
Otherwise tuendelee kuongelea tofauti zetu.
 
Unadhani hayuko sahihi 😂😂
Wewe unaona ni sawa hoja za swahiba wako Mbowe zijibiwe bungeni wakati mko kwenye benchi la mbege hapo kilabuni?

Najiuliza bila YouTube kusikilizia hoja za wapinzani, vikao vya bunge vingekuwaje?
 
Wazanzibar hawataki na huyo anayeongea au wanaoongea wana 'Baraka'.

Hivi tangu Wazanzibar waanze kuporomosha mitusi mwaka huu umemsikia nani wa CCM Zanzibar, CCM Taifa, ACT Zanzibar akikemea. Hii maana yake wote wanakubali hoja kama za passport na upuuzi mwingine
Hapana. Tusihukumu kijumla namna hii.
Kukosa uongozi wa kutetea muungano haina maana hawapo wanaoutaka muungano huo.. Samia ni kundi la OMO na akina Jussa toka zamani. Huwezi kutegemea aseme lolote juu ya hili mbali na kufaidika na u-Rais ambao hakutegemea angeukwaa.

Turudi nyuma kwenye historia ya muungano huu. Sababu zilizozuia kuua u-Zanzibari moja kwa moja toka mwanzo, na matarajio ya baadae juu ya muungano.
Walipoingia akina Jumbe wakaanza kutikisa kiberiti, wakakuta kimejaa. Hata enzi za Ruksa, hapakuwa na kelele nyingi toka kwa hiki kikundi kilichokuwa hakitaki muungano toka awali. Kero zimekuwa nyingi sana alipoingia Kikwete, na kuanza kulegeza muungano na kuuelekeza tulikofikia sasa hivi. Kikundi cha akina OMO sasa ndicho kinachotawala; na hawaoni aibu tena kufaidi matunda ya muungano, huku wakitaka kuua muungano wenyewe.

Hao waTanzania toka Zanzibar tusiosikia sauti zao wapo wengi tu, lakini kwa vile hakuna kiongozi wanayeweza kumtegemea kuwasemea; akina OMO wanachukua jukwaa zima.
 
Sisi watanganyika wajinga Sana... Yaan kajamaa Kako Nchi mwetu afu kanajibu hoja kipuuzi watu wanacheka na kufurahia.... Just imagine hili bunge lingekuwa kifanyikia Zanzibar?.
 
Hawa Viongozi Hivi Vyeti Vya Elimu Walivipataje
Kucheka Mtacheka Ila Muungano Unavunjika Sasa
 
View attachment 2991526

Mbunge anasema na au anakana kwamba yeye si Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Mtanzania”.

Sasa Humo Bungeni anafanya nini?

Hatuna Nchi inayoitwa Zanzibar wala nchi ya Tanganyika. Tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “ Tanzania”

Sasa kama yeye ni Mzanzibar na hatuna nchi hiyo, humo ndani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya nini? Kiti cha Speaker kingefaa kimtoe nje pale pale kwa kauli yake mwenyewe kwamba hapokei taarifa ya yeye ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kiti cha Speaker mumepwaya sana maana, Hatuna dual nationality, tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtu anasema na anakana kwamba yeye sio Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Principle of legal estoppel), sasa kwa nini aendelee kuwemo humo Bungeni?
Hatuna dual nationality, hakuna raia wa Burundi, Rwanda au nchi ya “Zanzibar” anayeweza kuwemo Humo Bungeni.

Ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee anayeweza kukaa humo, vinginevyo ni magumashi tu, bila chenga chenga na mkosi ni Mkosi tu- Haijalishi unatokea wapi.

Povu ruksa bila Matusi.
Huyu mwakilishi kutoka Zanzibar hafai kuendelea kuwemo ndani ya bunge la Jamhuri wa Muungano ni bora abaki huko Zanzibar ajitanue kwa kulinga na uzanzibari wake.

Kuna siku mamlaka za serikali zote mbili watashangaa kujionea mwisho wa uvumilivu wa Watanganyika; it is just a fractional feather line to disintegrate the so-called 'Union Agreement' a few years to come.
 
Hapana. Tusihukumu kijumla namna hii.
Kukosa uongozi wa kutetea muungano haina maana hawapo wanaoutaka muungano huo.. Samia ni kundi la OMO na akina Jussa toka zamani. Huwezi kutegemea aseme lolote juu ya hili mbali na kufaidika na u-Rais ambao hakutegemea angeukwaa.
Na ni kwasababu hizo matatizo tunayoyasikia yanatokana na 'Ombwe'. Wako wapi wanaoutaka? Mbona hatuwasikii
Turudi nyuma kwenye historia ya muungano huu. Sababu zilizozuia kuua u-Zanzibari moja kwa moja toka mwanzo, na matarajio ya baadae juu ya muungano.
Nyerere alijua ''Utaifa' utaleta matatizo ikiwa Zanzibar itamezwa. Makosa ni kufuta Utaifa wa Tanganyika.
Huwezi kuwa na Tanzania halafu ikawepo Zanzibar, hapo lazima utaialika Tanganyika na ndicho kinachotokea

Matarajio ya Mwl ilikuwa kwamba baada ya muda watu wote watajisikia ni wamoja, na kwakweli alifanikiwa kwa kiasi. Wazanzibar wanaoishi Tanganyika ni wengi kuliko wanaoishi Zanzibar at any given time! Tatizo ni kuwafanya wao ni muhimu sana na kwamba Tanganyika inawahitaji na si kinyume chake! Bahati mbaya dude limeamka
Walipoingia akina Jumbe wakaanza kutikisa kiberiti, wakakuta kimejaa.
Jumbe alikuwa na point tatizo alisailitiwa !
Hata enzi za Ruksa, hapakuwa na kelele nyingi toka kwa hiki kikundi kilichokuwa hakitaki muungano toka awali. Kero zimekuwa nyingi sana alipoingia Kikwete, na kuanza kulegeza muungano na kuuelekeza tulikofikia sasa hivi. Kikundi cha akina OMO sasa ndicho kinachotawala; na hawaoni aibu tena kufaidi matunda ya muungano, huku wakitaka kuua muungano wenyewe.
Well, Muungano haujawah kutulia ! G55 ilikuwa wakati wa Mwinyi. In fact ndio muda ambao Muungano ulikuwa katika matatizo makubwa kwasababu Watanganyika walichoshwa na upendeleo na uchotaji rasilimali. Je historia inajiurudia?
Hao waTanzania toka Zanzibar tusiosikia sauti zao wapo wengi tu, lakini kwa vile hakuna kiongozi wanayeweza kumtegemea kuwasemea; akina OMO wanachukua jukwaa zima.
Hapana, nieleweshe kwanini Wabunge wa CCM hawakulaani kauli ya kibaguzi ya yule mpuuzi wa ACT kuhusu passport. Yes ni ya kipuuzi kwasababu nyingi! ni upuuzi tu.
Guess what? ACT Wazalendo wamekaa kimya kwa maana wanaunga mkono hoja ya passport
Viongozi wote wa JMT na SMZ wamekaa kimya, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono
Bunge limeshindwa kumkemea mpuuzi na mbaguzi yule anafaidi maziwa na asali ya Tanganyika.

Hakuna Mzanzibar mtaani anayelaani. Kwa maneno mengine wanakubali hoja ya kipuuzi
Tunasema hivi, warudishe passport hata kesho. Sisi tunahitaji Tanganyika tu deal na mambo yetu
 
View attachment 2991526

Mbunge anasema na au anakana kwamba yeye si Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Mtanzania”.

Sasa Humo Bungeni anafanya nini?

Hatuna Nchi inayoitwa Zanzibar wala nchi ya Tanganyika. Tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “ Tanzania”

Sasa kama yeye ni Mzanzibar na hatuna nchi hiyo, humo ndani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya nini? Kiti cha Speaker kingefaa kimtoe nje pale pale kwa kauli yake mwenyewe kwamba hapokei taarifa ya yeye ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kiti cha Speaker mumepwaya sana maana, Hatuna dual nationality, tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtu anasema na anakana kwamba yeye sio Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Principle of legal estoppel), sasa kwa nini aendelee kuwemo humo Bungeni?
Hatuna dual nationality, hakuna raia wa Burundi, Rwanda au nchi ya “Zanzibar” anayeweza kuwemo Humo Bungeni.

Ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee anayeweza kukaa humo, vinginevyo ni magumashi tu, bila chenga chenga na mkosi ni Mkosi tu- Haijalishi unatokea wapi.

Povu ruksa bila Matusi.
Mimi nafikiri hata yeye mwenyewe huyu mbunge bila shaka hata hajui anazungumza nini!
 
Hii mbegu wamaepianda Wazanzibar kwasababu ile ile aliyosema Nyerere '' Sisi ni Wazanzibar wao ni Watanganyika''
Ukishajitambulisha kwa Uzanzibar huwezi kukwepa Utanganyika. Ukishaondoa Zanzibar huwezi kuwa na Tanzania

Ni Wazanzibar hawa akina Jussa, Othman, Duni wanataja 'Tanganyika'' wanaosema Watanganyika ni Wapumbavu wamelala kama huyu Mbunge wa watu 3,338 wa ACT Wazalendo anayesema tutumie passport.

Ukisoma mandhari ndani ya Taasisi za nchi hata hapo Bungeni Watanganyika wakiwemo wa CCM wamechoka.
Tunahitaji Tanganyika tu kama watahitaji Muungano wataomba wao, Watanganyika hawana cha kupoteza!

JokaKuu Pascal Mayalla @
Mkuu kuna kitu kinaniambia kuwa hawa wenzetu wa visiwani (Zanzibar) hasa viongozi na elites wengine baada ya miaka mingi ya kuotesha mizizi ya kiuchumi na kiuongozi huku bara (Tanganyika) huku wakikingiwa kifua na chama tawala wanaona sasa wanaweza kutikisa kiberiti cha muungano wazi wazi. Tena sasa wakiwa na mtu wao pale juu ambaye anaimarishwa na katiba yenye imperial presidency juu ya vyombo vya dola na raia watiifu sana (extremely subservient citizenry), jeuri imeongezeka. Ni kama vile kibao kimegeuzwa.

Nionavyo, tatizo ni kuwa Tanganyika ilishapotezewa uhai na nguvu zake miaka mingi iliyopita tokea JKN akamilishe mradi wa kuisimika CCM kama state party. Ni mchakato uliofanywa taratibu na kwa uhakika kwa imani ya kujidanganya (false hope) kuwa hatimaye Zanzibar “itapotelea” yenyewe ndani ya “Tanganyika”. Hadi leo najiuliza sana kama JKN kweli alikuwa so naive. Kwamba hakuiona kabisa nguvu ya “uZanzibari” kwa uzito wake kuwa isingeruhusu kitu kama hicho kitokee. Au kwamba yeye asingekuwepo kushuhudia hilo na warithi wake wangekuwa na ajenda nyingine kabisa.

Leo Tanganyika haina uongozi wala utashi wa kuwepo kama taifa tena. Hakuna mwenye interest na Tanganyika miongoni mwa waTanganyika walio kwenye uongozi wa nchi. Ajenda ni maslahi binafsi na ya makundi. Elites wa CCM huku bara na Zanzibar wameshaungana kikamilifu kama kundi moja kimaslahi.

Haya yote yanaendelea wakati consciousness ya u-taifa wa Zanzibar ikizidi kuja juu, huku ya Tanganyika is long dead and buried. Sioni matumaini yoyote. No hope; no joy.
 
Halafu hakuna mtu wa kutaka mwongozo wa Spika..alipoapa Kuingia Bungeni aliapa kama na nani?
Yes ni swali muhim linalosumbua. Wazanzibar wanaukana Utanzania ndani ya Bunge la Tanzania 'with impunity'

Ni utamaduni, Mzanzibar anaweza kuongea lolote, neno lile lile akiongea Mtanganyika linakuwa kero au matusi.

Spika na Bunge hawawezi kuzungumzia 'Raia wa daraja la I, Wazanzibar)

Kuna ombwe la uongozi ! Wazanzibar wanaukana Utanzania na kudai passport! pengine kuna support !!!
 
Huyu mwakilishi kutoka Zanzibar hafai kuendelea kuwemo ndani ya bunge la Jamhuri wa Muungano ni bora abaki huko Zanzibar ajitanue kwa kulinga na uzanzibari wake.

Kuna siku mamlaka za serikali zote mbili watashangaa kujionea mwisho wa uvumilivu wa Watanganyika; it is just a fractional feather line to disintegrate the so-called 'Union Agreement' a few years to come.
Ndio maana nashangaa Huyo Speaker/Subwoofer wa mabunge duniani- PhD ya sheria, bado hajatolea Muongozo ile kauli ya yule Mzenj... sijui ni kwa nini wabunge wengi wanaona aibu kuipigania Tanganyika. Ajabu sana kwa kweli
 
View attachment 2991526

Mbunge anasema na au anakana kwamba yeye si Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Mtanzania”.

Sasa Humo Bungeni anafanya nini?

Hatuna Nchi inayoitwa Zanzibar wala nchi ya Tanganyika. Tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, “ Tanzania”

Sasa kama yeye ni Mzanzibar na hatuna nchi hiyo, humo ndani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anafanya nini? Kiti cha Speaker kingefaa kimtoe nje pale pale kwa kauli yake mwenyewe kwamba hapokei taarifa ya yeye ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kiti cha Speaker mumepwaya sana maana, Hatuna dual nationality, tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtu anasema na anakana kwamba yeye sio Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Principle of legal estoppel), sasa kwa nini aendelee kuwemo humo Bungeni?
Hatuna dual nationality, hakuna raia wa Burundi, Rwanda au nchi ya “Zanzibar” anayeweza kuwemo Humo Bungeni.

Ni Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee anayeweza kukaa humo, vinginevyo ni magumashi tu, bila chenga chenga na mkosi ni Mkosi tu- Haijalishi unatokea wapi.

Povu ruksa bila Matusi.
Mjinga tu na mbinafsi huyo mbunge wa zanzibar. Kwanza aweze kutofautisha kubaguliwa na kupingwa. Watu wanampinga rais kwa hoja mbalimbali kwa ujinga wake anasema anabaguliwa. Pia mjinga anadai ziwepo passport huku anajidai anaunga mkono uwepo wa muungano. Hajui kwamba ndani ya muungano hakuna taifa la zanzibar ila kuna taifa la tanzania. Kama walivyo vigogo wengi wa zanziba kunapokuja suala la muungano wanaonekana kama wajinga kutokana na ubinafsi na ubaguzi waliyonao. Yaani wanataka chetu chetu na chenu chetu.
 
Simple tu wapeni uhuru wao Zanzibar na muache kufagilia ukoloni kwa kigezo cha muungano.
 
Hakuna Mzanzibar mtaani anayelaani. Kwa maneno mengine wanakubali hoja ya kipuuzi
Tunasema hivi, warudishe passport hata kesho. Sisi tunahitaji Tanganyika tu deal na mambo yetu
Tunakubaliana sana sehemu kubwa, tofauti yetu ni sehemu ndogo lakini muhimu zaidi.

Hoja yangu ni kwamba, kuna watu wa kawaida sana huko mitaani, ukiwauliza maswala ya muungano, bila kuwawekea siasa mbele, watakwambia muungano wanautaka. Hawa watu hawana sauti na wanaogopa hili kundi lenye kelele nyingi sana.
Nani awasemee wasikike? Hakuna. Huko CCM, hasa ya huko visiwani, wabunge wote, mawaziri waliomo kwenye serikali zote mbili, wote ni bubu kwa kuogopa kundi hili la akina OMO; huku wakifaidi matunda ya muungano kupitia CCM ambayo ndiyo kinga yao dhidi ya hilo kundi lenye kelele.

Tunapopishana sasa, ni hapa pa kuvunja muungano kwa sababu ya kelele za watu wanaojulikana toka awali, hawakuupenda muungano. Kufanya hivi ni kuwapa ushindi hawa , ushindi wasioustahili kabisa.

Tudai Tanganyika, kwa shinikizo la hawa wapuuzi? Kufanya hivyo pia ni kusalimu amri kwao.
Dawa ni moja tu. Unda serikali moja, acha wapige kelele. Kelele zitakuwepo hata muungano ukivunjika, au ukiunda serikali tatu.
 
Kuna watu wa kawaida huko mitaani, ukiwauliza maswala ya muungano, bila kuwawekea siasa mbele, watakwambia muungano wanautaka.
Hawa watu ni Wazanzibar nadhani kwasababu Mtanganyika hafaidiki na chohote!
Hawa watu hawana sauti na wanaogopa hili kundi lenye kelele nyingi sana.
Ndio wanaojaza mikutano ya kina OMO. Ndio wapiga kura na bila wao akina OMO hawana nguvu
Nani awasemee wasikike?
They have to stand up! mwisho wa siku watakuwa victims of circumstances.
Hakuna. Huko CCM, hasa ya huko visiwani, wabunge wote, mawaziri waliomo kwenye serikali zote mbili, wote ni bubu kwa kuogopa kundi hili la akina OMO; huku wakifaidi matunda ya muungano kupitia CCM ambayo ndiyo kinga yao dhidi ya hilo kundi lenye kelele.
Ububu ni kubaliana na akina OMO at the same time wanaogopa masilahi yao.
Hakuna anayesimama kutetea masilahi na future ya Muungano! nao pia ipo siku watakuwa victims siku si nyingi
Tunapopishana sasa, ni hapa pa kuvunja muungano kwa sababu ya kelele za watu wanaojulikana toka awali, hawakuupenda muungano. Kufanya hivi ni kuwapa ushindi hawa , ushindi wasioustahili kabisa.
Hadi sasa wana ushindi. Resource za Tanganyika zinazoelekelezwa Zanzibar ni kubwa kuliko eneo lingine la nchi.
Eneo lisilo na mchango katika maendeleo ya Tanganyika ni Zanzibar , kwa namba za BoT

Lakini kubwa zaidi ni kuwafanya special na wenye authority. Fikiria hivi, watu wanatumia umeme na wake zao halafu bill wanaleta Tanganyika kwa muuza mchicha! na hili linafanyika kwasababu ya Uzanzibar

Kwamba wakope wao kama sehemu maalumu, halafu alipe Mtanganyika.
Jiulize nafasi za upendeleo katika masomo , ajira n.k. ni za nini ikiwa wao hawataki kabisa ''chao' kuguswa?
Wao ni washindi kwasababu wamedekezwa
Tudai Tanganyika, kwa shinikizo la hawa wapuuzi? Kufanya hivyo pia ni kusalimu amri kwao.
Hapana hatuwezi kuendelea na mizozo ya kila siku na watu milioni 2 nusu yao wakiishi Tanganyika
Hatuwezi kufanya lolote ni kelele za siku , we need to move on.

Tunahitaji Tanganyika . Ndio maana nimekuuliza, tushawishi tunahitaji muungano kwa masilahi au faida gani.
Dawa ni moja tu. Unda serikali moja, acha wapige kelele. Kelele zitakuwepo hata muungano ukivunjika, au ukiunda serikali tatu.
Haiwezekani! hao CCM Zanzibar hicho hawakubali, miaka 60 bado tunasikia upuuzi wa passport seuse hilo.

Tunahitaji kuelekeza resources zetu maeneo yenye tija yasiyo na kelele na tutakayotumia wote kwa faidia yetu kana nchi, ubaguzi wa Zanzibar hatuuhitaji . Tutakwenda na passport nao warudi kwao. Period
 
Back
Top Bottom