Mkuu 'Nguruvi3, ngoja nikwambie USHINDI mkubwa kabisa walioupata hawa kundi OMO. Ni kuwafanya waTanganyika ambao tayari walishaukubali u-Tanzania wao kuanza kudai Tanganyika. Hakuna ushindi zaidi ya hapo.Hadi sasa wana ushindi. Resource za Tanganyika zinazoelekelezwa Zanzibar ni kubwa kuliko eneo lingine la nchi.
Eneo lisilo na mchango katika maendeleo ya Tanganyika ni Zanzibar , kwa namba za BoT
Ngoja nikurudishe kwa mkasa wa Jumbe.Ukiutazama mkasa ule kwa umakini zaidi, utaona kwamba uongozi wa juu wa wakati ule ungekuwa ni legelege, tusingefika hadi huku tulikofika sasa hivi.
Tabia na tamaduni za watu hawa wa visiwani ni tofauti sana na tabia za huku Tanganyika na maeneo mengine mengi. Jumbe walimsulubu, baada ya kuona viongozi wa juu hawamchekei nyani. Walipoona vile mara moja wakamgeuka Jumbe na kumvisha jiwe shingoni; hao hao wenzake waliokuwa wakimsukuma atoke mbele.
Tumeona jinsi Samia anavyofanya kazi. Akiwa chini ya Magufuli, hukusikia akiinua kidole hata kuonyesha tu alama kwamba yeye hayamhusu. Baada ya Magufuli kutoka kwenye picha tumeona sarakasi nyingi alizo/anazofanya hadi hapa tulipofikia.
Nusra amzamishe maskini Mbowe, kwa njia zilezile za kupuliza sana pasitokee maumivu anapong'ata.
Kwa hiyo, kuwalaumu waZanzibari (wote) kukataa muungano, siyo kweli. Sasa hivi utawaona wakijaza mikutano ya akina Jussa, kwa vile wakati huu ndio wanaotamba. Hakuna sauti nyingine wanayoweza kuisikiliza kuwatahadharisha juu ya janga hili la kuvunja muungano.
Ili tusiwe tunazungukia humu humu kwenye mambo ambayo tayari tumeyajadili tayari, niseme tu kuwa kwa upande wangu mkazo nauwekea kwa kundi hili ambalo toka mwanzo halikuukubali muungano, kundi ambalo lilikuwa limedhibitiwa vizuri sana toka awali wa kuanzisha muungano. Taratibu, kundi hili likaanza kujipenyeza na kutunga na kupenyeza maswala ya KERO; maswala ambayo viongozi dhaifu wa CCM hawakuweza kuyakabili ; badala yake wakadhani kuyatumia kama rushwa ili kuwapunguza ukali kundi hili, kumbe ndiyo wanawachochea moto.
Hoja yangu muhimu zaidi, na ambayo ningekuomba uitilie fikra zaidi, ni hili swala la Tanganyika. Kuidai Tanganyika sasa hivi, kwa vile akina OMO wametuhimiza iwe hivyo itakuwa ni swala la aibu. Kwa sababu tutakuwa tunashiriki ujinga waliokuwa nao hawa watu toka mwanzo.
Lakini naomba unielewe vyema, kama hakuna uongozi wa kutufanya tusimame kulikabiri hili kundi, sina tatizo kabisa kuuvunja muungano na kurudisha Tanganyika yetu.
Swala la kuwa na Tanganyika, ili mradi tuwe sawa na hao wenye u-Zanzibar wao, hili sioni mantiki yake hata kidogo. Kwa hiyo swala la serikali tatu ni kupotezeana muda tu, na kufuja mali. Ni bora tukakutana na waZanzibari huko kwenye Umoja wa Afrika Mashariki.
Haya yote ni marudio ya yale ambayo tayari nilisha yawasilisha, lakini nimeona ni muhimu niyarudie, pengine nitaeleweka vizuri zaidi safari hii.
Muungano ni serikali moja tu. Acha akina OMO wafanye kazi waliyo zoea kuifanya,-kupiga kelele.