Mbunge Mohammed Issa aliyesema yeye si Mtanzania, kwanini bado yupo Bungeni?

Hata samia ukimuuliza uraia wake atasema ni mzanzibari lakini kizimkazi imejengwa kwa hela watanzania
 
Acha ujinga unajitukuza kwa usukuma this is purely Primimitive mindset

ni kabili Gani nchii halisemwi negatively

wahaya wachaga na wanyakyusa wamesemwa Toka 1954

wakwere tume wachamba sana kipindi Cha jk

nyie kusemwa semwa kidogo tu kipindi Cha mwendazake ndo iwe nongwa

kwa taarifa yako mmejulikana juzi baada ya mwendazake kuwa raisi
mhijishaue
 
Kule Darfur Janjawidi Arab Millitia wale ndio wabaguzi na Wauwaji sasa na huwezi kuwasikia Wazazibari wakilaani.
 
Ndio maana nashangaa Huyo Speaker/Subwoofer wa mabunge duniani- PhD ya sheria, bado hajatolea Muongozo ile kauli ya yule Mzenj... sijui ni kwa nini wabunge wengi wanaona aibu kuipigania Tanganyika. Ajabu sana kwa kweli

ASILI YA WATU WA ZANZIBARI (ZENJ-WEUSI)​

Watu wa Zanzibar ni wa asili mbalimbali, hasa watu wa asili ya Afrika Bantu, yakiwemo makabila ya Wahamidu, Makonde, Mwera, Nyasa, Sukuma, Ha, Manyema, Digo, Matumbi, na Watumbatu; halafu Waasia, awali kutoka India na nchi za Kiarabu.

Idadi ya wakazi wa Zanzibar ilikuwa 1,303,569 mwaka 2012, tarehe ya sensa ya mwisho, iliyoonyesha ongezeko la 3.1% kwa mwaka.

Karibu theluthi mbili ya watu wanaishi katika kisiwa cha Zanzibar (Unguja).

Mkoa wa mjini magharibi ndio wenye idadi kubwa ya wakazi, kiasi cha watu 205,870.

Pemba ina jumla ya makazi sawa. Mji mkubwa ni Chake Chake, ukiwa na idadi ya 19,283, mengine ni Wete na Mkoani.

Dini​

Dini ya Uislamu ina kiasi cha 97% za wananchi wote.

Waliobaki ni hasa Wakristo. Wa kwanza walikuja wakati wa utawala wa Kireno, halafu wakati wa masultani kuwepo Zanzibar na wa ukoloni wa Uingereza.

Kulikuwa na Wahindu pia lakini wengi wao walikimbia nchi au kuuawa wakati wa mapinduzi ya mwaka 1964.

Kuna misikiti 51, ambayo waadhini wake hugongana wakati wa maombi, pamoja na mahekalu ya Uhindu sita na makanisa kadhaa, yakiwemo Kanisa Kuu Katoliki na Kanisa Kuu la Anglikana katika mji wa Zanzibar Stonetown.

Hasa hilo la mwisho ni maarufu kwa sababu lilijengwa mahali pa soko la watumwa lililofungwa, altari ikiwa imejengwa juu ya nafasi ya mti wa kuwafunga watumwa walioadhibiwa kwa viboko, na batizio kuwa mahali walipotupwa watoto watumwa ambao hawakuuzwa pamoja na mama zao.

Hata hivyo MAKANISA kadhaa yalichomwa moto katika miaka 2005-2015.
 
Huyu rais wa kurithishwa urithi ambao yeye hakuutegemea anatuletea maruweruwe sana kwenye Nchi yetu ya Tanganyika .
Raisi anahusika vipi hapo?? Ni kina Lukuvi ndio wanaihitaji Zanzibar sio wazanzibar.
 
Mzanzibari na Mzanzibara
Hata wakubwa wengine huwa wanasema wao ni wazanzibari na mimi pia nasema mimi ni Mtanga au mimi ni Muarusha !!
Kubalini iandikwe Katiba mpya bora yote haya yatakwisha !!
ccm ndio hawakubali, wengine tuliisha ingia kingi kitambo sana toka ile Rasimu ya warioba itangazwe
 
Umesema angerudishwa kwao Zenji !
That means hata wewe unakubali kwamba yeye huyo mbunge ni Mzenji 😅😂🙏🙏 !

So hakuwa amefanya kosa lolote lile !
Kama kasema kuwa yeye ni mzanzibari si ataitwa mzanzibari(mzenji kwa jina lingine)?..Ama sivyo mkuu, ulitaka niseme angerudishwa kwao wapi ili hali amesema kuwa yeye ni mzanzibari?
 
hakuna hata moja ninalolikataa katika mifano yote uliyoitoa hapa, lakini...

Ni nani aliyefanya maamuzi haya?
Ni mTanganyika gani (kiongozi) aliyehusika katika mipango yote hii ya kutafuta maudhi kwa waTanganyika, ili wakasirike zaidi, ili na wao waanze kelele za kuvunja muungano?

Samia anafanya kazi kwa vitendo, ya akina OMO na wenzake. Na jibu linabaki palepale, kwamba sasa waTanganyika hasira zimewapanda hadi utosini, kitu ambacho wanakitaka sana hao "wazanzibari wasiopenda muungano."

Tunazunguka mle mle tu, mkuu wangu 'Nguruvi3'.

Mi napendekeza, tusikubali kupoteza vichwa vyetu kwa hizi kelele za hawa watu wanaotulazimisha sasa tuwe kama wao. Badala yake, tukatae kusalimu amri. Kazi ya kwanza iwe ni kuwaondoa CCM, ndio walioruhusu hali hii. Pili, tuchukue hatua za kuurudisha muungano kwenye malengo yake ya mwanzo bila kujali kelele; iundwe serikali moja tu, basi. Uzanzibari ubaki tu kuwa kama usukuma ulivyo.

Na kama unadhani haya hayawezekani, basi, tuirudishe Tanganyika yetu kama ilivyokuwa mwanzo. Hakuna sababu tena ya kujidanganya kuwa na muungano kwa kuunda chombo kingine cha kutafutia maslahi tu kwa watu.
 
hili nimekwisha lisemea, pamoja na kwamba huenda silielezi vizuri lakaonekana bayana. Mfano wa Jumbe niliutumia kwa maksudi kuelezea tabia hii ya waZanzibari. Jumbe angeachiwa kutamba wakati ule, usingeona wazanzibari wakiruka kimamnga kumkana. Lakini ilipoonekana uongozi wa CCM kwa wakati ule usingeweza kuruhusu ujinga huo, mara haraka sana Jumbe wakamkana.
Hali ni hiyo hiyo hata leo. Sasa hivi hawa watu wa Kero wanatamba sana, kwa sababu ndio wanaoonekana wameiletea Zanzibar manufaa makubwa bila ya mtu wa kuwa-'chalenge', siyo toka Tanganyika wala CCM huko Zanzibar. Hii 'option' ya serikali ya tatu ya nini tena, si ni bora tukakutane tu huko kwenye Jumuia yetu ya Afika Mashariki? 'Option' hii ni ya kuendelea kuwapendelea Zanzibar kwa njia moja au nyingine. Wao wataendelea kuja hapa Tanganyika, wakiwa na nchi yao, huku wakidai wamo ndani ya muungano wa Tanganyika na nchi ya Zanzibar yenye mamlaka kamili, kuamua chochote watakacho kufanya bila kujali maslahi ya Tanganyika. Zanzibar itakuwa ni njia tu ya kuihujumu Tanganyika, kama inavyofanyika sasa hivi.
Hapana hakuna aibu! wala hatuhitaji usawa na Zanzibar kwasababu kwa kanuni za asili hakuna usawa
Tuna population mara 30 , ardhi kubwa, mipaka 8 na nchi ndogo kati ya hizo ina watu milioni 14.
Tunahitaji kupunguza kelele zisizo na maana.
Aibu niliyoitaja hapa ni kwa waTanganyika kufanya kazi wanayotaka akina OMO na kundi lao ifanywe.
Li-nchi lote hili tunakosa uongozi wa kushindana na hiki kikundi cha wahuni, badala yake tunaona ni bora tufanye kama wanavyotaka wao?
 
Mkuu 'mzeewaSHY', naona kama pengine hujanielewa nilicho andika. Litakuwa jambo la ajabu sana kwangu kutetea hayo unayosema hapo juu - "kuhusu watu kupewa fursa ya kuongea..." Nitahoji vipi kitu kama hicho?
Sasa ni muhimu utofautishe. Nani huyo "anayetoa hiyo fursa..." Huyo mtu katoa wapi mamlaka makubwa ya namna hiyo?
Samia hajatoa fursa, hili ni takwa ndani ya Katiba, hata hii mbovu. Na hizi hadaa za kujidai katoa fursa, halafu wakati huo huo anatoa masharti mbele yake, ya kutumia lugha anayotaka yeye itumike, huoni kwamba bado fura hiyo ni ya masharti?
Na zaidi ya hapo, hiyo fursa inayotolewa kwa lengo la kuhadaa watu, huku matendo yakibaki vilevile, kama haya mazingaombwe ya tume huru na mengineyo; bado wewe huoni kasoro yoyote?

Nani kazuia Katiba Mpya isiandkwe, unajuwa? Tunasubiri mafunzo ya miaka mitatu juu ya swala hilo pekee. Kama huoni ulaghai katika haya yote, sijui nikueleze kitu gani ndipo uelewe.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja !
Hako unakokaita kakikundi ka OMO kanatakiwa kajibiwe kwa hoja sio kwa kutafutwa wa kukaziba mdomo !!

Wenye kushindwa kwa hoja siku zote hukimbilia kutumia mabavu. !
Siyo swala la hoja hapa. Kero ni hoja zipi katika muungano iwapo zinatazamwa toka upande mmoja tu; na zikilenga kuudhoofisha muungano.

Sijasema kuwanyamazisha kwa nguvu, wasiseme; lakini kusema kwao kusewe ndiko kutulazimishe kuuvunja au kuudhoofisha muungano
Waseme watakavyo, lakini kusema kwao kusiwe ndio iwe hatma ya muungano. Ni kazi ya CCM kujibu hizo unazoita hoja; lakini badala ya kuzijibu kwa hoja, badala yake wanaona ni bora kuwahonga ili kuwanyamazisha. Hawawezi kunyamaza, siku zote watakuwa na kero za kuwasilisha kwa CCM ili waendelee kula uhondo.
 
Ni nani aliyefanya maamuzi haya?
Ni mTanganyika gani (kiongozi) aliyehusika katika mipango yote hii ya kutafuta maudhi kwa waTanganyika, ili wakasirike zaidi, ili na wao waanze kelele za kuvunja muungano?
Hakuna Tume au Kamati au genge lililoundwa kushughulikia mambo ya muungano bila kushauri Tanganyika irudi.
Je, Jaji Nyalali , Jaji Kisanga, Shelukindo, Jaji Warioba walikuwa 'wrong'? Kwamba walikuwa na hasira unazosema!
Tume ya Warioba ilikuja na 'utafiti wa kina wa kisayansi' ukihusisha wadau wote wakiwemo CCM. Jibu ni lile lile.
Tanganyika inahitajika kama kitendawili kitateguliwa kwa amani
Samia anafanya kazi kwa vitendo, ya akina OMO na wenzake. Na jibu linabaki palepale, kwamba sasa waTanganyika hasira zimewapanda hadi utosini, kitu ambacho wanakitaka sana hao "wazanzibari wasiopenda muungano."
Hasira za Watanganyika zipo kwa namna nyingi
1. Yanyofanywa sasa na SSH ni yale ya akina OMO , si kuvunja muungano lakini ku 'abuse' Tanganyika.
2. Watanganyika wamepata kitu kinaitwa ''care fatique' yaani wamechoshwa uangalizi wa Muungano wao wakitoa na kumenyeka wakati kaeneo ka wa tu milioni 1.8 sawa na Ilala kakikpewa kipaumbele bila kuwa na ''return'
3.Watanganyika wamechoshwa na kelele, hawana cha kupoteza kwasababu wanaouhitaji si wao ni Wazanzibar
4. Watanganyika wanataka resources zielekezwe kwenye tija na si kulinda muungano. Kwa mfano, pesa zinazokwenda SMZ kutoka Tanganyika zingeimarisha mawasiliano na nchi 8 zinazotuzunguka zenye population na trade kubwa.
Mi napendekeza, tusikubali kupoteza vichwa vyetu kwa hizi kelele za hawa watu wanaotulazimisha sasa tuwe kama wao.
Hapana wakati ndio unatulazimisha na hakuna namna bali kuwapa 'choice' . Wazanzibar ndio wanahitaji Muungano. Kama huamini waambie wale 1.5 wanaoishi Tanganyika warudi Zanzibar uone kitakachotokea.
Tanganyika has nothing to lose , sijui kama unaelewa nina maanisha nini
Yes nakubaliana nawe kwasababu CCM wameshindwa kutengeneza suluhu, wanaweka viraka kwa jina la kero.
Hakuna kero, kilichopo ni Wazanzibar kudai hata wasichostahili kwasababu kuna kero gani wakati Tanganyika inatoa 100% na Zanzibar 0%? Of course kwa elimu ya Wazanzibar wanataka formula ya kugawana kama alivyoshauri balozi Amina !
Na kama unadhani haya hayawezekani, basi, tuirudishe Tanganyika yetu kama ilivyokuwa mwanzo. Hakuna sababu tena ya kujidanganya kuwa na muungano kwa kuunda chombo kingine cha kutafutia maslahi tu kwa watu.
Nakubaliana nawe, tumechoka kudanganyana ! Tanganyika irudi halafu wao waombe kama wanataka.
Yes, Tanganyika haihitaji Zanzibar
 
Siwezi kupata jibu la haraka ku'counter' hii. Siwezi kusema haielezeki. Lakini tuliachie hapa hili kwa sasa hivi.
Labda niseme tu: nani aliyezuia utekelezaji wa matokeo ya hizi tume, na kwa maslahi gani?
Mimi nadhani jibu litapatikana huko; na litaturudisha huku tuliko anzia. Kwa hawa kuishi Tanganyika ni hatua dhahiri ya wao kuukubali muungano. Sasa nasi tunataka kuungana na akina OMO, kundi dogo kabisa kudidimiza ndoto za uTanzania wao. Tumeungana na CCM na kikundi hiki cha sultani kuukata muungano, badala ya kuwatia moyo kwa kuunda serikali moja chini ya nchi yao moja.

Sisi pia hatutakuwa tofauti na hawa CCM, na kundi la OMO na Jussa.

Ninajuwa na kuelewa vizuri juu ya "Tanganyika has nothing to lose"... nisichokubali ni hili la kulazimishwa na kakikundi ka watu tufanye wanachotaka wao. Labda turejee huko nyuma, sababu za muungano wetu zilikuwa hasa ni zipi, ingawaje huko pia ni zilezile zinazoegemea kwa Zanzibar zaidi kuliko kwa Tanganyika.
 
Kama wale wabunge wasio na chama (COVID-19) wapo bungeni na wanalamba asali na uongozi wa bunge unaoongozwa na mwanasheria mbobevu amelala usingizi wa pono huku kaziba masikio yake kwa viganja vyake, huyo mbunge ni nani Hadi asiwepo bungeni Tena kwa raha zake?
 
Wananchi wengi wa Zanzibar wengi wao asili yao kupitia mababu ni bara,Malawi,Kongo na Zambia.,Visiwa vya Comorro,etc

Ukisoma historia vema mengi yapo wazi..Wengi walipelekwa Zanzibar wakiwa watumwa ktk mashamba ya waarabu..Visiwa vya Unguja na Pemba..

Zanzibar kuna Wasukuma,Wakurya,Wandengereko,Wazaramo,Wanyamwezi,Wadigo,Wasambaa,Wamanyema,Wabemba,Wanyasa,…Hata majina ya koo zao .

Undugu wa Watanganyika na watu wa visiwa vya Unguja na Pemba una mapana na mizizi ya damu kabisa..
 
Nimekuelewa Mkuu Kalamu !
Ngoja tusubiri tuone hii movie !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…