Mbunge Saashisha Mafue adaiwa kuwalipa vijana walioajiriwa kazi ya muda ya Postkodi Tsh. 15,000 kwa siku mkataba wa siku 15

Mbunge Saashisha Mafue adaiwa kuwalipa vijana walioajiriwa kazi ya muda ya Postkodi Tsh. 15,000 kwa siku mkataba wa siku 15

Heeee????
IMG-20220306-WA0010.jpg
 
Mbunge wa CCM Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Mh. Saashisha Mague ,amefanya maajabu kwenye serikali ya awamu ya sita kwa kuwalipa vijana walioajiriwa ajira ya muda ya Postikodi Tsh 15,000 kwa siku badala ya Tsh 30,000 kwa siku kama ilivyopangwa nss as Serikali ya mama Samia.

Kituko cha pili Mbunge huyo Amewaambia vijana hao kuwa ajira hiyo ni ya muda wa siku 15 badala ya siku 30 kama ilivyoainishwa na serikali ili zoezi lifanyike kwa Uangalifu na kwa umakini mkubwa.

Vijana hao wameamua kufanya kazi hiyo bila ufanisi kutokana na kulipwa malipo tofauti na mpango wa serikali, ila siku ya jumamosi tarehe 19.3.2022 wataandamana kumpokea mwenyekiti wa chadema Taifa ambaye atahutubia Jimbo la Hai mjini ikiwa ni mara ya kwanza tangu atoke gerezani na watafikisha kilio hicho mbele yake kwa mabango.

Mkuu wa Wilaya ya Hai alivyotafutwa kuzungimzia malipo hayo na siku za kufanya kazi hakutaka kusema chochote bali alisema hausiki na zoezi hilo na hakushirikishwa .

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, tulivyompigia simu ,kumuuliza kuhusu stahiki ya malipo kwa hao vijana wanaofsnys kazi kwa mkataba, kwa kila siku na muda wa kazi hadi kumalizika alisema yuko kwenye kikao.
Hiyo ni Kazi ya serikali sio mbunge.
 
Mbunge wa CCM Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Mh. Saashisha Mague ,amefanya maajabu kwenye serikali ya awamu ya sita kwa kuwalipa vijana walioajiriwa ajira ya muda ya Postikodi Tsh 15,000 kwa siku badala ya Tsh 30,000 kwa siku kama ilivyopangwa nss as Serikali ya mama Samia.

Kituko cha pili Mbunge huyo Amewaambia vijana hao kuwa ajira hiyo ni ya muda wa siku 15 badala ya siku 45 kama ilivyoainishwa na serikali ili zoezi lifanyike kwa Uangalifu na kwa umakini mkubwa.

Vijana hao wameamua kufanya kazi hiyo bila ufanisi kutokana na kulipwa malipo tofauti na mpango wa serikali, ila siku ya jumamosi tarehe 19.3.2022 wataandamana kumpokea mwenyekiti wa chadema Taifa ambaye atahutubia Jimbo la Hai mjini ikiwa ni mara ya kwanza tangu atoke gerezani na watafikisha kilio hicho mbele yake kwa mabango.

Mkuu wa Wilaya ya Hai alivyotafutwa kuzungimzia malipo hayo na siku za kufanya kazi hakutaka kusema chochote bali alisema hausiki na zoezi hilo na hakushirikishwa .

Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Hai , Dionis Myinga alivyotwafutwa ofisini kwake palikuwa pamefungwa .​

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, tulivyompigia simu ,kumuuliza kuhusu stahiki ya malipo kwa hao vijana wanaofanya kazi kwa mkataba, kwa kila siku na muda wa kazi hadi kumalizika alisema yuko kwenye kikao.

Vijana hao wanakiomba Chama cha mapinduzi ngazi ya wilaya ,mkoa,Taifa kuingilia kati hatima ya malipo yao na siku za kufanya kazi hiyo kama ilivyopangwa na serikali ya CCM. Vijana wamekata tamaa iliyosababishwa na mtu mmoja au kikundi cha watu.​

Wacheni kuandika taatifa za kusambaza chuki bana ni lini umewahi sikia mbunge anahusika na mambo za postkodi ?? Kweli wewe ni mpumbavu kabisa. Na taarifa zako za kipuuzi sana
 
CAA5EDF8-2E00-4ED8-BA22-847CCC932622.jpeg
Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe hongera sana kwa juhudi kubwa na nzr unazoendelea kuzifanya katika kuijenga Hai yetu. 🙏🏽
 
Hizi pesa huenda baadhi ya halmashauri zinaiba hizi pesa.

Kwanini kuwe na utofauti wa malipo wa hizi pesa?

Kwanini baadhi ya halmashauri ziweke wazi malipo yatakuwa ya sh. 30000 kwa siku huku zingine zishindwe kutangaza kiasi watakacholipa na idadi ya siku?

Taasisi za usalama wa Taifa zifuatilie hili na zipelekwe taarifa kwa amri jeshi mkuu kwa hatua zaidi kwa. halmashauri zote zinazotaka kukwamisha zoezi hili la postkodi
.

Ila mleta mada Mbunge hahusiki na kuajili au kuwalipa hao vijana.Mhusika mkuu ni mkurugenzi wa halmashauri.
 
Back
Top Bottom