Mbunge Saashisha Mafue adaiwa kuwalipa vijana walioajiriwa kazi ya muda ya Postkodi Tsh. 15,000 kwa siku mkataba wa siku 15

 
Siasa zimelemaza akili za waTanzania na kufifisha uwezo wa UBONGO kutafakari......

Watanzania imefikia hatua ya kubeba jambo linalotendwa na mpinzani wako kisiasa linaloonekana kubeba kisiasa pasi na kulichambua au kulipembua kiuyakinifu......

Wanasiasa wamevifanya vichwa vya waTanznia kuwa mabox ya kuhifadhia matamko, maneno na ajenda zao na sio chem chem ya tafakuri......
 
Aisee JF imevamiwa kwa kweli. Hata kama ni propaganda za kisiasa hizi ni za hovyo kabisa kwani zinaonekana zimebeba chuki binafsi kwa mbunge wa Hai kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa taifa na amani ya taifa hili. Nao hao vijana waliopewa kazi ya kuweka anwani za makazi wanapaswa watimuliwe mara moja kwa sababu kama tu hawamjui mwajiri wao sahihi ni halmashauri na sio mbunge wataweza vipi kuifanya hiyo kazi kwa usahihi? Mbunge na anwani za makazi wapi na wapi?

Huyu aliyeleta madai yao hapa ndio anaonekana mwelewa kuliko wenzake lakini ni kilaza kiasi hiki sasa hao waliopo huku "field" si ndio balaa kabisa. Watu wanajaribu kumwelewesha hapa mbunge hahusiki lakini wapi anakomaa mwanzo mwisho eti wao wameelezwa mwajiri wao ni mbunge. Halafu eti madai yao watapeleka kwa Mbowe siku akifika Hai. Kwa ninavyomjua Mbowe ni kuwa ameshavuka mbali sana siasa hizi za ovyo ovyo za kuchafuana na kujengeana chuki zisizo za msingi.

Mleta mada pamoja na wenzako pelekeni madai yanu kwa siri kwa mkurugenzi wa halmashauri wa wilaya ya Hai. Ikishindikana nendeni kwa Mkuu wa wilaya Hai, takukuru Hai, au takukuru mkoa wa Kilimanjaro kote huko utapokelewa vizuri na taarifa zako zitafanyiwa kazi kwa siri tena kwa haraka sana. Hapo inaonekana kuna watu wameshafanya yao halafu wanamtupia jumba bovu mbunge ambaye hahusiki kwa namna yote ile labda kwenye uhamasishaji tu.
 
Mleta mada pamoja na wenzako pelekeni madai yanu kwa siri kwa mkurugenzi wa halmashauri wa wilaya ya Hai.(Siri)
 
Tatizo ni jimbo lililotajwa,ametoka mahabusu anataka akabidhiwe jimbo Kwa msamaha wa Rais.
 
Kila halmashaur Ina Muundo wake so ni vile walivyokubaliana kufanya Kazi. Mf Kuna halmashaur imeona itangaze nafasi nyingi Kwa malipo kidogo Ili Kazi imalizike mapema... Pengine 10000 Kwa siku lakn wametoa Ajira Kwa watu 400. Wengine wametangaza nafasi chache ila watachukua siku nyingi zaidi pengine watu 150 ila watalipwa 30000.
 
Nilishakukataza kutoa taarifa za umbea humu, tangu lini Mbunge akahusika na malipo kwa wafanyakazi wenye ajira za Halmashauri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…