gallow bird
JF-Expert Member
- Aug 10, 2024
- 14,889
- 18,593
Hakuna hoja ya kidini hapo,ila huyo yuda ndiyo anatumia sinagogi kwa ajili ya 2030,na huo ni ujumbe maalum toka jumba jeupeKwani nini shida..?
Watu wa system wakae nae asee, hoja za kidini sio njema hata kidogo
Umakamu wa rais hautolewi na rais wala chama,bali deep state,makamu wa rais ni rais in standbyJamaa hasemi Gwajima. Anamsema nchimbi wazi wazi kabisa. Nchimbi naye ngoja akome. Wewe ni katibu mkuu unakubalije kuruhusu MTU anatumia short cut kupata urahisi sababu tu amekuonga kuwa makamu wa rais.
Gwajima hayuko ndani ya serikali.Gwajima ni mpiga dili tu anatuzuga watanzania kama anavyo wazuga waumini wake.
Lakini kwanini Tanzania ina viongozi wa hovyo sana🤣🤣 kwanini hamjadili kuleta maisha bora kwa wananchi. Na mnaishia kujadili kiazi Gwajima🤣
porojoAnaaripoti Zungu Mgalilaya
View attachment 3600055
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu (Zanzibar), Ndg. Simai Mohammed Said, amezua taharuki bungeni leo baada ya kushusha makombora mazito ya kisiasa dhidi ya kiongozi mmoja ndani ya serikali ambaye hakumtaja jina moja kwa moja na akambatiza jina la "Yuda" kwa madai ya kumsaliti Rais Samia Suluhu Hassan, kuvuruga safari za kisiasa za watendaji, na kutumia jina la hayati Rais John Magufuli kujitafutia huruma ya umma.
Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, Simai amewasihi wabunge na serikali "kuamka" na kutoumia moyo na propaganda zinazoenezwa na kiongozi huyo kwenye nyumba za ibada. Simai amerejea kauli ya aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, aliyewahi kusema "binadamu ni wale wale," lakini akasema yeye ameamua mmoja wao kumbatiza jina la Yuda Iskariote kutokana na tabia yake
Link : https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/reel/885931224536362/
Je kiongozi huyo ni nani? How safe is the government kama tumefikia hatua hii?
Magufuli alitaka mwinyi na kikwete akasuma mpaka samia akapata. Deep state iko wapi hapo. Deep state yenyewe hiko wapi. Ngoja nchimbi apambane na Hali yakeUmakamu wa rais hautolewi na rais wala chama,bali deep state,makamu wa rais ni rais in standby
Too bad! Humo humo bungeni atasimama mtu ajibu vibaya iwe nongwa. Hawa watatoana damu hadi wafikie mwisho.
Nakuamini. Maelezo haya ni ya ndani kabisaBalozi Leo hata wakati namba Moja anaondoka Nchini hakuwepo kwenye Line up ya Kumuaga pale airport, Hii gesture inatuambia kuwa Huenda hata yeye sio in charge wa top seat,
Huyo itakuwa katumwa.Huyu Simai atasababisha mpasuko mbaya ndani ya chama. Huyu akichekewa ndo utakuwa mwanzo wa mpasuko chamani. WanaCCM wajue vyama vya upinzani vilivyopo haviwezi kuitoa CCM madarakani ila mpasuko ndani ya chama unaweza ukaleta shida kubwa kiasi cha kupoteza madaraka.
Mje na novichok au polonium kutoka urusi yuda apotee basi tumechokaa kelele zenuHakuna hoja ya kidini hapo,ila huyo yuda ndiyo anatumia sinagogi kwa ajili ya 2030,na huo ni ujumbe maalum toka jumba jeupe
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said, amesema mafanikio ya Serikali katika ukusanyaji wa mapato yanaonyesha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha Bungeni leo Juni 2, 2026, Simai alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha unaoelekea ukingoni, jambo alilosema linaakisi uimara wa usimamizi wa uchumi wa nchi.
Hata hivyo, alisema bado kuna baadhi ya watu wanaokwamisha juhudi za maendeleo kwa maslahi binafsi, akidai kuwa mmoja wao ni mtu aliyemtaja kwa jina la "Yuda" ndani ya Serikali.
"Kosa la Rais Samia ni lipi? Kumuamini mtu? Kumbe ni Yuda. Yuda huyu amewasaliti ndugu zake mwenyewe, hata familia iliyomlea kisiasa haitaki kumuona. Hata huko nyuma aliwahi kuitwa mzigo, lakini leo mzigo huo tunao ndani ya Serikali," alisema Simai.
Aidha, Simai alidai kuwa mtu huyo amekuwa chanzo cha maumivu kwa watu mbalimbali, akiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi wa umma na wafanyabiashara, huku akisema baadhi ya waliokuwa na mustakabali mzuri wa kisiasa walipoteza nafasi zao kutokana na ushawishi wake na wengine kuingia katika changamoto za kisaikolojia.
"Leo huyo huyo anapita katika nyumba za ibada na maeneo mbalimbali akitafuta huruma ya wananchi. Anajaribu kujijenga kama mwathirika wa mfumo, wakati wengi wanafahamu nafasi yake katika kuathiri maisha na safari za watu wengine," aliongeza.
Kwa upande mwingine, Simai alikosoa kile alichokiita matumizi ya jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa maslahi ya kisiasa, akisema si sahihi kwa mtu yeyote kujinasibisha na urithi wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa lengo la kujijengea uhalali mbele ya umma.
"Leo anataka kutuaminisha kuwa Hayati Magufuli alimpenda sana. Kama alimpenda, kwa nini alimuweka mbali? Waliompenda na waliopendwa na Rais Magufuli wanafahamika, na baadhi yao wapo hapa Bungeni hadi leo. Tumwache Hayati Magufuli apumzike kwa amani; alilitumikia taifa kwa kiwango kikubwa. Yuda aache kutafuta huruma za wananchi kwa kutumia majina ya watu waliotangulia mbele za haki," alisema Simai.
Anaweza asiingie ikulu,deep state huwa haitaki mtu wa hivyoMje na novichok au polonium kutoka urusi yuda apotee basi tumechokaa kelele zenu
Je anamlenga nani?Hayo maneno kutumwa na Samia
Yuda ashakuwa controlled , ndio maana bado yuko seriakilini.Huu mtanange umefikia patamu
Hakuna mtu,hajawahi toke wa ku-hand pick rais au makamu,elewa,hizo ni propaganda za kumpaka choo kikweteMagufuli alitaka mwinyi na kikwete akasuma mpaka samia akapata. Deep state iko wapi hapo. Deep state yenyewe hiko wapi. Ngoja nchimbi apambane na Hali yake
Unaposema deep state unamaanisha kikwete au nani aliye salia?Anaweza asiingie ikulu,deep state huwa haitaki mtu wa hivyo