Mbunge Simai: Kuna Yuda Msaliti ndani ya Serikali hili anatafuta huruma kanisani

1995 kikwete hakuwa deep state,leo ni deep state,deep state ni marais wastaafu,wakuu wa majeshi wastaafu na waliopo,wakurugenzi TISS wastaafu na waliopo,vigogo vya usalama vistaafu na vilivyopo ambavyo huvijui
Kwa Sasa SI kakikundi ka watafuna nchi na wasio taka mirija yao ikatwe ndio wanajiita deep state?
 
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said, amesema mafanikio ya Serikali katika ukusanyaji wa mapato yanaonyesha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha Bungeni leo Juni 2, 2026, Simai alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha unaoelekea ukingoni, jambo alilosema linaakisi uimara wa usimamizi wa uchumi wa nchi.

Hata hivyo, alisema bado kuna baadhi ya watu wanaokwamisha juhudi za maendeleo kwa maslahi binafsi, akidai kuwa mmoja wao ni mtu aliyemtaja kwa jina la "Yuda" ndani ya Serikali.

"Kosa la Rais Samia ni lipi? Kumuamini mtu? Kumbe ni Yuda. Yuda huyu amewasaliti ndugu zake mwenyewe, hata familia iliyomlea kisiasa haitaki kumuona. Hata huko nyuma aliwahi kuitwa mzigo, lakini leo mzigo huo tunao ndani ya Serikali," alisema Simai.

Aidha, Simai alidai kuwa mtu huyo amekuwa chanzo cha maumivu kwa watu mbalimbali, akiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi wa umma na wafanyabiashara, huku akisema baadhi ya waliokuwa na mustakabali mzuri wa kisiasa walipoteza nafasi zao kutokana na ushawishi wake na wengine kuingia katika changamoto za kisaikolojia.

"Leo huyo huyo anapita katika nyumba za ibada na maeneo mbalimbali akitafuta huruma ya wananchi. Anajaribu kujijenga kama mwathirika wa mfumo, wakati wengi wanafahamu nafasi yake katika kuathiri maisha na safari za watu wengine," aliongeza.

Kwa upande mwingine, Simai alikosoa kile alichokiita matumizi ya jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa maslahi ya kisiasa, akisema si sahihi kwa mtu yeyote kujinasibisha na urithi wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa lengo la kujijengea uhalali mbele ya umma.

"Leo anataka kutuaminisha kuwa Hayati Magufuli alimpenda sana. Kama alimpenda, kwa nini alimuweka mbali? Waliompenda na waliopendwa na Rais Magufuli wanafahamika, na baadhi yao wapo hapa Bungeni hadi leo. Tumwache Hayati Magufuli apumzike kwa amani; alilitumikia taifa kwa kiwango kikubwa. Yuda aache kutafuta huruma za wananchi kwa kutumia majina ya watu waliotangulia mbele za haki," alisema Simai.

Anamjua vizuri Balozi lakini? Vita yake ni noma amuulize JK
 
Kwa hali ilivyo sasa ya chama cha ccm kupoteza imani ya wa Tanganyika.... ilidhani mwana ccm mwenye akili timamu angempongeza Dr Emanuel Nchimbi kwa kazi nzuri ya kurudisha umoja wa kitaifa anayoifanya ... lakini cha ajabu analipwa ubaya ...... hivi kwa nini serikali hii mtu anaehubiri Haki, Uwajibikaji ; Umoja na mshikamano anaonekana mbaya ?? Nyie mazezeta , ma chawa na msiojielewa ( mizanzibar ) msitufanye sisi wa Tanganyika wajinga tunajua kila kutu . Sasa hivi tunakaribia kupata Uhuru .
 
Huyu Simai atasababisha mpasuko mbaya ndani ya chama. Huyu akichekewa ndo utakuwa mwanzo wa mpasuko chamani. WanaCCM wajue vyama vya upinzani vilivyopo haviwezi kuitoa CCM madarakani ila mpasuko ndani ya chama unaweza ukaleta shida kubwa kiasi cha kupoteza madaraka.
Mpasuko upo Sana tu.
Ni suala la Muda yote yataonekana hadharani.

Yale mauaji na jinsi walivyoyahandle yalishaleta mpasuko.

Viburi kwa wazanzibar viko juu mno.
 
Hivi tulilaaniwa au?
Upendo haupo kwetu sisi ndio tatizo lilipo,angalia Zanziber linapokuja suala la uzanziber hamna Kafu sisim au act woote lao moja. Salum Mwalim Jusa Omo unawasikia hii leo? Nchimbi jeshi la mtu mmoja hamna Kabudi wala nani, damu ya kiarabu upendo wao kwa wao. Njoo huku kwetu sasa utamkuta Lukasi Mshamba Kabudi Nape na wengine wengi.
 
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said, amesema mafanikio ya Serikali katika ukusanyaji wa mapato yanaonyesha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha Bungeni leo Juni 2, 2026, Simai alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha unaoelekea ukingoni, jambo alilosema linaakisi uimara wa usimamizi wa uchumi wa nchi.

Hata hivyo, alisema bado kuna baadhi ya watu wanaokwamisha juhudi za maendeleo kwa maslahi binafsi, akidai kuwa mmoja wao ni mtu aliyemtaja kwa jina la "Yuda" ndani ya Serikali.

"Kosa la Rais Samia ni lipi? Kumuamini mtu? Kumbe ni Yuda. Yuda huyu amewasaliti ndugu zake mwenyewe, hata familia iliyomlea kisiasa haitaki kumuona. Hata huko nyuma aliwahi kuitwa mzigo, lakini leo mzigo huo tunao ndani ya Serikali," alisema Simai.

Aidha, Simai alidai kuwa mtu huyo amekuwa chanzo cha maumivu kwa watu mbalimbali, akiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi wa umma na wafanyabiashara, huku akisema baadhi ya waliokuwa na mustakabali mzuri wa kisiasa walipoteza nafasi zao kutokana na ushawishi wake na wengine kuingia katika changamoto za kisaikolojia.

"Leo huyo huyo anapita katika nyumba za ibada na maeneo mbalimbali akitafuta huruma ya wananchi. Anajaribu kujijenga kama mwathirika wa mfumo, wakati wengi wanafahamu nafasi yake katika kuathiri maisha na safari za watu wengine," aliongeza.

Kwa upande mwingine, Simai alikosoa kile alichokiita matumizi ya jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa maslahi ya kisiasa, akisema si sahihi kwa mtu yeyote kujinasibisha na urithi wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa lengo la kujijengea uhalali mbele ya umma.

"Leo anataka kutuaminisha kuwa Hayati Magufuli alimpenda sana. Kama alimpenda, kwa nini alimuweka mbali? Waliompenda na waliopendwa na Rais Magufuli wanafahamika, na baadhi yao wapo hapa Bungeni hadi leo. Tumwache Hayati Magufuli apumzike kwa amani; alilitumikia taifa kwa kiwango kikubwa. Yuda aache kutafuta huruma za wananchi kwa kutumia majina ya watu waliotangulia mbele za haki," alisema Simai.
Mbn hajamtaja Nchimbi, acheni fitina na uchonganishi. Hata hivyo Nchimbi ni mtu hatari, tangia apate umakamu wa Rais amebadilika sana, ukaribu na Rais umepungua amekuwa karibu sana na maaskofu wa RC, Pasaka alienda kuhiji Vatican, ni mdini. Halafu aache hotuba zenye utata, amekosa busara na hekima, mbn Dr. Mpango was very smart na ni mkatoliki mzuri sana. Nchimbi hajatulia halafu hata kuongea kwenyewe hawezi
 
Kivipi hakufukuti huko jikoni? Ila Nchimbi hamtamuweza sio Membe huyo, wacha tuone waganga wa vitabu toka Tanga na Tunguli labda machozi ya wajane na yatima yanaenda futika,hujaenda Russia??
Agenda ya taifa letu kwa mwaka,2030-2040 ni Dr Emmanuel John Nchimbi. Full stop. 🐒
 
Mbn hajamtaja Nchimbi, acheni fitina na uchonganishi. Hata hivyo Nchimbi ni mtu hatari, tangia apate umakamu wa Rais amebadilika sana, ukaribu na Rais umepungua amekuwa karibu sana na maaskofu wa RC, Pasaka alienda kuhiji Vatican, ni mdini. Halafu aache hotuba zenye utata, amekosa busara na hekima, mbn Dr. Mpango was very smart na ni mkatoliki mzuri sana. Nchimbi hajatulia halafu hata kuongea kwenyewe hawezi
Wew ndo huyo mbunge nini?
Haipendezi Mwanaume kuwa na maneno kama yale.
Men are straight forward
 
Back
Top Bottom