Mbunge Simai: Kuna Yuda Msaliti ndani ya Serikali hili anatafuta huruma kanisani

Tokea jana alielekea Dubai huku nyuma akiacha mjadala wenye tuhuma ndaniye

Hoja, kwa nini huyo ndugu Mamlaka zilimruhusu asafiri kuelekea Dubai na siyo awasilishe hoja ya Yuda kwa Mamlaka za ki uchunguzi?!

Kwa nini amefikia kwenye nyumba ya mmoja ya watoto wa wenye Mamlaka kuu hapa nchini?!

Mda ni Mwalimu.
 
Screenshot_20260604-133242~2.png
 
Huyu Simai atasababisha mpasuko mbaya ndani ya chama. Huyu akichekewa ndo utakuwa mwanzo wa mpasuko chamani. WanaCCM wajue vyama vya upinzani vilivyopo haviwezi kuitoa CCM madarakani ila mpasuko ndani ya chama unaweza ukaleta shida kubwa kiasi cha kupoteza madaraka.

Ilishapasuka zamani mpaka yakatokea yalio tokea, Cha kushangaza ni kama hawajifunzi.
 
Maneno kama siwezi kuharibu future yako yalivyotua masikioni mwa waharibu future za watu kisa tu kutofautiana kwa mtizamo ama kuwaza/mawazo, yamewatesa sana watu wetu. Hata uteuzi wa Ummy Mwalimu kama mshauri wa Rais, unaweza kuwa umechangiwa sana na hiyo statement. Na hata huo ushauri anaweza kumaliza miaka iliyobakia pasipo kuutoa.
 
Hii nchi ingekua na Deepstate, kizimkazi asingegombea 2025.

Kuna genge la Wahuni tu.
Aliyetakiwa Ʊi amina salum Ali,sasa yeye akawa team lowasa kindakindaki,ndipo mama akalamba dodo,na alikua hataki akalazimishwa kama ambavyo magu hakutaka 'akasukumizwa'..so deep state iliamua makamu awe mwanamke
 
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said, amesema mafanikio ya Serikali katika ukusanyaji wa mapato yanaonyesha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha Bungeni leo Juni 2, 2026, Simai alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha unaoelekea ukingoni, jambo alilosema linaakisi uimara wa usimamizi wa uchumi wa nchi.

Hata hivyo, alisema bado kuna baadhi ya watu wanaokwamisha juhudi za maendeleo kwa maslahi binafsi, akidai kuwa mmoja wao ni mtu aliyemtaja kwa jina la "Yuda" ndani ya Serikali.

"Kosa la Rais Samia ni lipi? Kumuamini mtu? Kumbe ni Yuda. Yuda huyu amewasaliti ndugu zake mwenyewe, hata familia iliyomlea kisiasa haitaki kumuona. Hata huko nyuma aliwahi kuitwa mzigo, lakini leo mzigo huo tunao ndani ya Serikali," alisema Simai.

Aidha, Simai alidai kuwa mtu huyo amekuwa chanzo cha maumivu kwa watu mbalimbali, akiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi wa umma na wafanyabiashara, huku akisema baadhi ya waliokuwa na mustakabali mzuri wa kisiasa walipoteza nafasi zao kutokana na ushawishi wake na wengine kuingia katika changamoto za kisaikolojia.

"Leo huyo huyo anapita katika nyumba za ibada na maeneo mbalimbali akitafuta huruma ya wananchi. Anajaribu kujijenga kama mwathirika wa mfumo, wakati wengi wanafahamu nafasi yake katika kuathiri maisha na safari za watu wengine," aliongeza.

Kwa upande mwingine, Simai alikosoa kile alichokiita matumizi ya jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa maslahi ya kisiasa, akisema si sahihi kwa mtu yeyote kujinasibisha na urithi wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa lengo la kujijengea uhalali mbele ya umma.

"Leo anataka kutuaminisha kuwa Hayati Magufuli alimpenda sana. Kama alimpenda, kwa nini alimuweka mbali? Waliompenda na waliopendwa na Rais Magufuli wanafahamika, na baadhi yao wapo hapa Bungeni hadi leo. Tumwache Hayati Magufuli apumzike kwa amani; alilitumikia taifa kwa kiwango kikubwa. Yuda aache kutafuta huruma za wananchi kwa kutumia majina ya watu waliotangulia mbele za haki," alisema Simai.
Kauli kama hii Kwa Kiongozi wake wa juu, na sio kwenye Kikao ambayo mtuhumiwa hawezi kujitetea, ni dharau Kwa "Yuda" na aliye juu ya "Yuda" isipokuwa kama ametumwa na Aliye juu ya Yuda
 
Kwa bamna makamu anavo mpambania mama, kuitwa yuda ni kumkosea.
 
Yuda aache kutafuta huruma za wananchi kwa kutumia majina ya watu waliotangulia mbele za haki
Hii sio sawa huyu Muhuni kakosea kinoma yaan bila kujua hata anachofanya, hata km mtu una bifu nae hukutakiwa kufanya wewe boya unajichafua mwenye.. creation ya neno Yuda ni sisi wewe unadandia mtumbwi kwa mbele halafu unaropoka kinyesi mwanetu tubu hata km umekunywa bia tubu dhambi zako, wewe mboni unatumia jina la Yuda kumpakaza kinyesi mwenzio Yuda yupo mbele yako au yupo mbele ya haki matako yako
 
Nadhani hapa kuna harufu ya Uzanzibar vs Utanganyika!
Drivers Licence ya Tanzania haikubaliki na polisi Zanzibar!

Uzanzibari na Utanganyika upo ndio!

Sio harufu. Ni uhalisia.

Hivi kwa nn sisi Watanganyika ni wapumbavu kiasi hiki kwenye kutetea maslahi yetuuuu??
 
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said, amesema mafanikio ya Serikali katika ukusanyaji wa mapato yanaonyesha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha Bungeni leo Juni 2, 2026, Simai alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha unaoelekea ukingoni, jambo alilosema linaakisi uimara wa usimamizi wa uchumi wa nchi.

Hata hivyo, alisema bado kuna baadhi ya watu wanaokwamisha juhudi za maendeleo kwa maslahi binafsi, akidai kuwa mmoja wao ni mtu aliyemtaja kwa jina la "Yuda" ndani ya Serikali.

"Kosa la Rais Samia ni lipi? Kumuamini mtu? Kumbe ni Yuda. Yuda huyu amewasaliti ndugu zake mwenyewe, hata familia iliyomlea kisiasa haitaki kumuona. Hata huko nyuma aliwahi kuitwa mzigo, lakini leo mzigo huo tunao ndani ya Serikali," alisema Simai.

Aidha, Simai alidai kuwa mtu huyo amekuwa chanzo cha maumivu kwa watu mbalimbali, akiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi wa umma na wafanyabiashara, huku akisema baadhi ya waliokuwa na mustakabali mzuri wa kisiasa walipoteza nafasi zao kutokana na ushawishi wake na wengine kuingia katika changamoto za kisaikolojia.

"Leo huyo huyo anapita katika nyumba za ibada na maeneo mbalimbali akitafuta huruma ya wananchi. Anajaribu kujijenga kama mwathirika wa mfumo, wakati wengi wanafahamu nafasi yake katika kuathiri maisha na safari za watu wengine," aliongeza.

Kwa upande mwingine, Simai alikosoa kile alichokiita matumizi ya jina la Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa maslahi ya kisiasa, akisema si sahihi kwa mtu yeyote kujinasibisha na urithi wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa lengo la kujijengea uhalali mbele ya umma.

"Leo anataka kutuaminisha kuwa Hayati Magufuli alimpenda sana. Kama alimpenda, kwa nini alimuweka mbali? Waliompenda na waliopendwa na Rais Magufuli wanafahamika, na baadhi yao wapo hapa Bungeni hadi leo. Tumwache Hayati Magufuli apumzike kwa amani; alilitumikia taifa kwa kiwango kikubwa. Yuda aache kutafuta huruma za wananchi kwa kutumia majina ya watu waliotangulia mbele za haki," alisema Simai.
Makamu wa rais ameuzuliwa na Wazanzibari! Nyerere alikuwa anafikiria nini kuunda muungano wa namna hii? Aidha uwe muungano wa kweli wa nchi Moja, au mipaka izingatiwe. Haiwezekani mambo kiholela holela tu. Mtanganyika hawezi kumwuzulu hata Sheha Zanzibar!
 
Back
Top Bottom