Tetesi: Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na Meya wasakwa na Jeshi la Polisi


Shida hapo ugomvi wao hawa wawili unachochewa na mkulu na ndio tatizo kubwa ktk mkoa huo

Inasikitisha kuona Rais mzima kukosa busara ya kuingilia kati mgogoro huu wa kipuuzi unaosababishwa na Mteule wake Gambo!
Mimi kwa kumheshimu Rais JPM napenda kumpa ushauri wa bure na sihitaji hata ukuu wa Wilaya au Mkoa! Kwamba: KWA HALI INAYOENDELEA ARUSHA KATI YA MBUNGE LEMA(Chaguo la Wananchi)na RC GAMBO(Chaguo la Rais) LAZIMA RAIS AIDHA AMUHAMISHE MTEULE WAKE GAMBO AU AMFUKUZE KAZI! Rais Magu asitegemee chembe ya maendeleo jijini Arusha kwa hali hii!Kwa vile Lema ni Mbunge wa kuchaguliwa na Wananchi Rais hana mamlaka ya kumwondosha ila kwa Gambo anaweza!
Kama Rais JPM hawezi kuchukua ushauri huu wa bure basi kuna hatari ya kuanza kuwatengeneza kina Mwamwindi wa Arusha na huyu Gambo ni mwanadamu kama wengine na huenda yaka mtokea kama yaliyomtokea Dr.Kleruu(RIP) enzi za uhai wake! It' s just a matter of time!
 
Mkuu hayo ni matokeo ya elimu pasipo elimu. Sifa ya uteuzi ikiwa ni kujivika ujinga ili mradi chama dola mbele kwa mbele ndiyo matokeo yake. Bado miaka minne tutaisona namba
 
Mbona kejeli za rais hazikukeri? Usisahau sheria ya maisha kuwa kila mtenda hutendwa
 
Lema akamatwe na afunguliwe mashitaka kwa kauli inayoashiria kutaka kumuua rais kwa kisingizio cha Mungu kumbe wao chadema ndiyo wanapanga na wanajiumbua kwa kauli zao tatanishi
 
Mm nashauri itafutwe njia ya wawili hao Lema na Gambo wakae na kuzika tofauti zao na kila kiongozi afanye majukumu yake bila kuingilia majum ya mwingine tunataka arusha isonge mbele kimaendeleo bila malumbano ya viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa
Haiwezekani kwa mamlaka zao za kazi zao zinasimamiwa kitofauti.

Mimi naamini Lema analegezea kamba huyu mgambo, ila cha moto kinampata mgambo.
 
Ubaya ni kwamba labda wabadilishe sheria mbunge awe miaka kumi tuu, la sivyo lema is there to stay miaka Mia 8, Gambo hawezi kukaa hapo hata miaka mitano
 
Lema akamatwe na afunguliwe mashitaka kwa kauli inayoashiria kutaka kumuua rais kwa kisingizio cha Mungu kumbe wao chadema ndiyo wanapanga na wanajiumbua kwa kauli zao tatanishi
Hamjiamini? Fungueni mashtaka maana hamna aibu ya kushindwa.
 
nimeanza kupata idea
 
Kwahiyo wewe unadhani Lema kafanya nini hadi atafutwe hivyo? Au ndo amehisiwa kusambaza ile barua ya Mkurugenzi wa Jiji, Kihamia. Mimi na wewe hatujui tutulie. Vinginevyo basi wewe ni Gambo na unajua Lema amekutenda vipi ndo maana unamtafuta.
 
jifunzeni ngeli kwanza[emoji23] !! wafkiri watalii wanahamishwa kizembe ivoo ata mkivijenga kumii kama mnaishi kishamba don't expect tourists wafikie uko samahani lakini
 
Ka gamba bwana! Leo nimekasikia kakiwaambia Masai kule longido kuwa serikali haiwezi saidia wenye njaa .
 
Gambo ana haingaika bure Lema hamuwezi,Lema ni wananchi wa Arusha,kupambana na Lema ni kupambana na wananchi wa Arusha,Lema siyo size yake kwa chuki alizo nazo kwa Lema,Lema angekuwa mtumishi wa umma angekuwa ameshamtumbua.
 
Ntibenda aliondolewa Arusha kwa bifu za UVCCM kwa sababu alikuwa anashirikiana vizuri na Viongozi wa upinzani ndo huyu Gambo akiwa DC akapandishwe cheo kuwa Rc baada ya kutofautina na Lema kwenye kikao mbele ya Naibu Waziri Jafo akiwa kwenye ziara jijini Arusha.
Gambo anatakiwa kutumia zaidi busara kama ana bifu zake na Lema anatakiwa kuziweka pembeni kwa sasa.
 
Huyu hafai kuwa Mwenyekiti wa mtaa anafanya kazi bila kufuata utaratibu anapenda sana kuingilia mambo ambayo hayamuhusu sijui hata JPM alimleta Arusha kufanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…