Kuna vitu watu hukosea sana, na hii husababishwa na kurithi utamaduni, huku tukiendelea kuaminishwa lazima tuheshim tamaduni haijalishi uo utamaduni upoje.
Tuna shuhudia hata wenye elim kubwa tu, unakuta msichana anaelim yake kubwa lkn bado anajiona hana aman asipo olewa mapema. Na chazaidi anacho waza watu watamuonaje? wenzake wanaolewa yeye bado anachelewa na uoga wa umri kwenda.
Pamoja na kuwa na elim, lakini kukosa fursa ya kujichanganya na jamii tofauti, kukosa exposure na jamii tangu utotoni, kujifunza huru bado kunafanya vijana wasomi wengi kuishi ktk mfumo uleule unao fanana na ambao hawajasoma. Unashindwa kuona utofauti, cha zaidi labda utofauti utakuwa kwenye uchumi lkn kwenye social life hamna utofauti.
May be inachangiwa pia na kuzungukwa na Wajinga wengi kiasi kwamba unauzoea ujinga na kuwa sehem yao.
Lakini mimi naamini katika kuoa lzm uzingatie vifuatavyo
1. Kwanini unaoa? Je ni kwasababu watu wanaoa? Unataka tu upate watoto?
2. Upo tayari kuoa? (kukubali kubadilisha mfumo wa ubachela) upo tayari kukabiliana na changamoto za ndoa?
3. Unaweza mudu kuendesha familia? hali ya kiuchumi ipoje?
4. Umepata mtu sahihi? Umejihakikishia anakufaa? Umekubaliana na madhaifu yake na yako?
Kuishi kwa uoga ni hatari sana, yani utadhan una guarantee ya kuishi milelel hapa dunian.
Cha muhimu katika maisha ni kujitahidi kuitafuta furaha na aman, kuishi maisha unayoyataka.