"kwakuwa sijastaafu siasa na kwakuwa unafiki sio mzuri, natamka wazi kuwa nitaondoka chadema kipindi changu cha ubunge kitakapoisha na nitajiunga na NCCR Mageuzi, na nitagombea ubunge jimbo lolote isipokuwa jimbo la Moshi vijijini." Anthony Komu Mbunge wa Moshi Vijijini.
Kama hiyo nukuu ni maneno kutoka kwa Anthony Komu,basi kuna shida kubwa kichwani mwake. Ni kama vile anafanya hivyo ili kulipiza kisasi. Hata hivyo kafanya ujinga sana, ni kama anapelekwa na asijue mwisho wake ukoje. Maelezo ya Komu yanaonyesha kabisa bila kuwa CHADEMA kwa hii miezi michache, basi hata huo Ubunge wake utamponyoka.
Maelezo yake pia yanaonyesha nje ya CHADEMA, hana uwezo wa kushinda Uchaguzi ujao katika jimbo la Moshi Vijijini hata kama atahamia CCM, ndo sababu anasema atagombea ubunge lkn sio Jimbo la Moshi Vijijini.
Maelezo ya Komu yanaonyesha nia yake hasa kwa sasa ni kutengeneza mgogoro ndani ya CHADEMA, ni kama mtego kwa CHADEMA wa kuwafanya wawe busy na Komu na kuachana na masuala ya msingi.. Hilo tuwaachie CHADEMA.
Hata hivyo, style hii alokuja nayo Komu, ni kama inamwanika vibaya Mheshimiwa Mbatia, ni kama anaithibitishia dunia kwamba yupo kwenye utekelezaji wa jambo maalum..
Shida ninayoiona hapa ni matokeo ya anachokifanya kama kitakuwa na impact yoyote.
Ningekuwa Mimi ndiye Mbatia, ama Komu, ama yeyote mwenye plan kama hii, ningefanya tathmini kwanza kwa kutumia rejea ya Harambee ya Umma kuwatoa Viongozi wa CHADEMA Gerezani. Ile ilitosha kabisa kuwafanya watu wafahamu kwamba hii mision haina maana kabisa kwa Watanzania.
Bahati mbaya Wanasiasa huwa wana Imani zao za kufikirika.
#Nawa mikono kila wakati#
#COVID19 NI HATARI#
Sent using
Jamii Forums mobile app