Mbunge wa Muheza, Mwana FA alipataje Master's Degree bila kuwa na Bachelor degree?

Mbunge wa Muheza, Mwana FA alipataje Master's Degree bila kuwa na Bachelor degree?

Ni Advanved Diploma naona kuna error kwa aliyeandika hii CV ,miaka ya nyuma IFM walikuwa wanatoa Advanced Diploma ambayo ni Equivalent na Degree ya sasa ambao nao kwa sasa IFM wanatoa degree wameachana na Advanced diploma
Kwahiyo ukimaliza certificate unaenda Advanced diploma/ bachelor degree moja kwa moja na sio unasoma ordinary diploma?
 
Daah wabongo bhana huyo dogo alikua anaimba huku anasoma na alikua busy sana na masomo miaka ya nyuma TIA,CBE na IFM pamoja na vyuo vingi vya ufundi walikua wanatoa Advance Diploma wakisema ni Equivalent to Degree kama mtu anapata point nzuri anaweza kujiunga Masters bila kusoma Postgraduate diploma ambayo vyuo hivyo pia walikua wanatoa...kwa jinsi nilivyomuona alivyokua anathamini Elimu toka enzi hizo na yupo fomu kwenye Muziki nilimpa Big Up sana..
 
Kwahiyo ukimaliza certificate unaenda Advanced diploma/ bachelor degree moja kwa moja na sio unasoma ordinary diploma?
Kuna watu SAUTI Mwanza walisoma certificate mwaka 1 na kuunga degree au hujui hilo?ili mradi uwe umesoma form 6 na kupata results au cheti cha form 6 fuatilia kwa waliosoma SAUTI wengi wao wamefanya hvyo
 
Unazungumzia vyuo vya biashara hivyo.
 
2004 -2005, 2005-2006 na 2006 - 2007 kuna diploma ya miaka mitatu kweli? Nadhani ni Advanced diploma ambayo ilikuwa inamuezesha kusoma Post Graduate Diploma. MENGINE atakuja kujibu mwenyewe.
Diploma ya miaka mitatu imekuwepo kwa mda mrefu mkuu!

Diploma za miaka mitatu ziliwahusu zaidi wahitimu wa kidato cha nne..

NB; diploma hizi hazikuhusisha kada ya ualimu!!!
 
Ukisoma Advanced diploma unapaswa usome Postgraduate Diploma ili ukwolifai kusoma Masters
mimi nimesoma ADA IAA Tena Kwa kulipiwa na wizara ya fedha na masters nimesoma UD , usiongee usiyoyajua
 
Back
Top Bottom