Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Oleshangai: Wananchi wapatao 31 wamejeruhiwa vibaya sana. Wanatibiwa nchini Kenya

Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Oleshangai: Wananchi wapatao 31 wamejeruhiwa vibaya sana. Wanatibiwa nchini Kenya

 
Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Oleshangai Naomba kuthibitisha kuwa wananchi wapatao 31 wamejeruhiwa vibaya sana kwenye zoezi la uwekaji wa beacons kwenye ardhi ya vijiji, Ngorongoro...
 
Imekuwaje tena jamaa walisema hakuna kule mauaji ni wanapotoshwaa, waziri jiuzulu kwa aibu hii [emoji51][emoji51][emoji51]
 
Imekuwaje tena jamaa walisema hakuna kule mauaji ni wanapotoshwaa, waziri jiuzulu kwa aibu hii [emoji51][emoji51][emoji51]
 
Honestly, hata sijaelewa hoja yako specific ni nini..

Lakini, haijalishi. Labda nikuulize swali hili moja..

Kwani, wewe kwenu ambako ni asili yako na wazazi wako ni wapi kwani ndugu 1000 digits?

Hebu tuashumu, ni kule Peramiho kata ya Mtogo ambako wazazi wako na vizazi vyao vimekuwapo...

Sasa, hebu jaribu kujibu swali hili ukitumia dhamira safi ya nafsi na moyo wako pasipo kujidhulumu mwenyewe..

Kwamba, itokee sasa serikali inaamua kuja kunyang'anya ardhi wananchi wote wa kijiji chako na vya jirani eneo lenye ukubwa wa zaidi ya 16,000km² bila kuwashirikisha, bila kukubaliana nao eti tu kwa sababu iliyoamua ni serikali...

How would you feel..? Wananchi hao ndugu zako wangefanyeje unadhani?

Hiki ndicho kinachotokea huko Loliondo na Ngorongoro...!!

Nakushangaa tu unavyowalauumu hao Wamasai na kuwapa kila aina ya majina mabaya eti tu kwa sababu hawakaribishwi watu wengine kwenye ardhi yao..

Sasa, utawezaje kumpangia mtu namna ya kuishi ktk eneo lake binafsi? Hiyo ni ardhi yao, wamezaliwa hapo tangu vizazi na vizazi. Wanalinda mila, desturi na utamaduni wao ikiwemo kutouza ardhi kwa wageni...

Leo serikali eti inataka iwatoe wamasai ktk ardhi yao ya asili ili imuuzie mtu toka taifa jingine kwa jina la "mwekezaji". Hiyo ni ngumu, haikubaliki. Kama ni hilo dude uliitalo "serikali" kushikwa sharubu, sasa hakika litshikwa na lazima litulie kwa sababu nguvu ya umma ni kuu kuliko kikundi kidogo cha watu kinachoitwa "serikali"...!
Wamasai hawana ardhi maalumu ndio maana serikali inataka iwape ardhi. Wao wamezoea popote ni halali yao kufuga Hata kama ni Shamba la MTU lenye mazao. Isitishe Wamasai wanahamishwa Ili wapate mazingira Bora zaidi. Hivi serikali inawezaje kuleta maendeleo Kwa WATU wasio na makazi maalumu? Tuache kuangalia mambo Kwa hisia binafsi. Tuangalie Kwa manufaa ya Taifa. Mfumo huu Wa kifugaji UNAPASWA kubadilishwa Ili ulete tija Kwa familia. Hivi unadhani ukimchukua mtoto Wa kimasai mwenye miaka kumi na tatu ukampeleka Saint Francis kusoma atajisikiaje baada ya muda ukimwachisha masomo Ili arudi akachunge porini pasipo Hata na choo na maji safi na salama?

Sio sawa kabisa Serikali kuwaacha wanadamu kuishi kama wanyama Kwa faida ya wanaharakati uchwara.
 
Wamasai hawana ardhi maalumu ndio maana serikali inataka iwape ardhi.
Unajua unachowaza na kuandika kweli ndugu 1000 digits?

Unasema, wamasai hawana ardhi maalum ndiyo maana serikali inataka iwape. Kama ufikirivyo ndivyo hivyo, hapo walipo sasa hao wamasai ni ardhi ya nani? ya kwako wewe? Unasemaje hawana ardhi maalumu?

Na kwanini serikali iwatoe hapo halafu ikawape kwingine? Serikali iache kuchokoza wananchi. Na iwaache Wamasai ktk ardhi yao.

Kama serikali inahitaji kutwaa ardhi hiyo kwa matumizi mengine, basi ifuate utaratibu wa kisheria isitumie nguvu. Izungumze na watu wote. Itoe sababu za wazi kwanini inataka kutwaa ardhi hiyo ili kila mtu aelewe. Na ikikubalika, ihakikishe inatoa fidia stahiki kwa wote wanaotaka kuondoka kwa mujibu wa sheria..

Lakini hili kwa vyovyote vile, hili suala utekelezaji wake ni mgumu sana kwa sababu ni ngumu mno kutwaa ardhi na kuhamisha watu wengi karibu 300,000 ktk eneo kubwa la wilaya nzima bila kusababisha vurugu la maafa makubwa...!

Serikali lazima ifikiri mara mbili tatu tena kwa hekima na busara...!
Wao wamezoea popote ni halali yao kufuga Hata kama ni Shamba la MTU lenye mazao. Isitishe Wamasai wanahamishwa Ili wapate mazingira Bora zaidi. Hivi serikali inawezaje kuleta maendeleo Kwa WATU wasio na makazi maalumu?

Acha uongo. Hujui usemalo. Unazungumza kana kwamba wamasai wamezuka juzi na kutua hapo ngorongoro/Loliondo wakati wamekuwapo karne na karne na style yao ya maisha ndiyo hiyo hiyo - yaani ufugaji...

Kama unazungumzia maendeleo, basi huna unachoelewa. Mimi naishi Shinyanga. Jamii ya kisukuma nayo style yake ya maisha ya kiasili ni kama wamasai. Wengi ni ufugaji wa kuhamahama kutafuta malisho. Kuna vijiji huku maisha ni duni kabisa. Hakuna maendeleo. Hakuna huduma bora za kijamii kama tu ilivyo kwa wamasai. Kwa kigezo hiki, hoja yako haiwezi kusimama hata kidogo...!

Na kwa mantiki hii, serikali haiwezi kutumia kigezo hiki kutaka kuvuruga mfumo wa maisha ya asili ya watu kwa jina la "maendeleo"

Kama ni hivyo, kwanini sasa wasije kuwahamisha wananchi wote wa wilaya ya Meatu maana hawana tofauti na hao wa Ngorongoro?

JIBU NI RAHISI TU:

Meatu hakuna kitu wanachokitaka ila kipo Ngorongoro na baadhi ya viongozi wa serikali wameamua kuwa madalali wa mwarabu na wameteka ufahamu na akili zenu nyie "wajinga" wachache msioweza kuelewa kirahisi ili kupiga debe blindly ili kuwapa uhalali na kusaidia uporaji wao kwa urahisi lakini kwa gharama ya damu ya wananchi masikini, wamasai kwa kumuuzia mtu mgeni wa taifa jingine kwa jina la "investor...!" huku nyie mkidanga toka kuwa hayo ndiyo "maendeleo!!"l
 
Back
Top Bottom