Pre GE2025 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Pre GE2025 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Magufuli si hayupo? Nini tena bajameni?

Tikubaliana kabisa kwamba sasa Amani imetamalaki! Vipi teana huko?
 
Inasemekana kuwa mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Simanjiro.

Amekimbizwa hospitali katika juhudi za kupambania maisha yake.
Taarifa zaidi zitakujia baadae.
Hakuna alie salama..!!

---

Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuliahambulia gari lake kwa risasi mapema leo jioni hii.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wameeleza kwamba walisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo kabla ya washambuliaji kutokomea kusikojulikana.

Taarifa za uhakika kutoka Simanjiro zinaeleza kwamba mbunge huyo pamoja na dereva wake wote wamenusurika baada ya gari lao kushambuliwa kwa risasi wakati wakiwa jimboni humo.
Jino kwa jino
 
Back
Top Bottom