Pre GE2025 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Pre GE2025 Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Inasemekana kuwa mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Ole Sendeka amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Simanjiro.

Amekimbizwa hospitali katika juhudi za kupambania maisha yake.
Taarifa zaidi zitakujia baadae.
Hakuna alie salama..!!

---

Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuliahambulia gari lake kwa risasi mapema leo jioni hii.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wameeleza kwamba walisikia milio ya risasi ikishambulia gari hilo kabla ya washambuliaji kutokomea kusikojulikana.

Taarifa za uhakika kutoka Simanjiro zinaeleza kwamba mbunge huyo pamoja na dereva wake wote wamenusurika baada ya gari lao kushambuliwa kwa risasi wakati wakiwa jimboni humo.

View attachment 2948550

Watakuwa siyo askari wa CCM hao kwa maana wao risasi 3 huwa zinatosha sana ... !
 
Amewakosea nini wale jamaa!!?

Huwa hawashambulii TU Bure wale jamaa!!Kuna kitu kafanya!!

de 'levis uko wapi !!?utupe clue!!?

Watu wanafikiri hata Lisu alishambuliwa kwa kuonewa!hapana !Kuna miiko ya kimfumo aliikosea ya wale jamaa ukiivuka TU wanakuijia hata kama wengi wataona unaonewa lakini lazima Kuna mambo utakua ulishaonywa lakini ukashupaza shingo!!

Itakua haikua safe process,tagert atakua alishtukia ndio maaana hawajafanikiwa kwa asilimia mia!!

Matukio ya wakubwa kupigwa risasi nchi hii hayajaanza Leo;-

RIP IMRAN KOMBE

LIVE LONG TUNDU LISU

LIVE LONG OLESENDEKA!!
 
labda anapinga ardhi ya wamasai kuporwa kupewa mwarabu awinde, wamasai wanafurumushwa na serikali kupisha ujenzi wa hoteli ya mwarabu ina trend dunia nzima isipokuwa tanzagiza tu ndo watu labda hawajui …
Hizo ripoti ni mwiko kutangazwa hapa nchini, ukitangazwa uhalisia unaitwa mchochezi.
 
Acha wamalizane wenyewe kwa wenyewe CCM ni mafiii ya Asubuhi kabisa Laana za mababu mitume na manabii ziwe juu yao
 
Back
Top Bottom